AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2

Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

WAPINZANI wanaposema kuwa Uislamu ulienezwa kwa upanga; Waislamu huja juu na kuwarudi hao wnaoeneza uongo huo, kwa hoja zilizo nzito. Kwa kweli dhana hiyo ni potofu. Kuna dalili na ushahidi wa kutosha kuthitibisha kuwa Uislamu ni dini ya amani na siyo dini ya vita. Amani hiyo ni baina ya binadamu na Muumba wake, na pia, baina ya binadamu na binadamu wenzake. 

Serikali ya Afghanistan nayo imetoa taarifa ya kukataa Taleban kuhusika na mauaji hayo. Na ikaishutumu Iran kwa kuwasaidia wapinzani wa Kishia waliopo katika mji huo wa Bamiyan. 

Kwa vyovyote vile mauaji hayo lazima yashutumiwe. Lakini mbona mauaji hayo yametokea katika hali ya utatanishi? Yasemekana wanadiplomasia hao waliuawa wakati wa harakati za kuuteka mji wa Mazar-I –Shariff, mji wa mwisho mkubwa uliokuwa mikononi mwa wapinzani. Inadaiwa kuwa maofisa hao walikuwa wakiwasaidia wapinzani wa Kishia katika jimbo hilo. 

Hata hivyo, kama walitambulikana kuwa ni maofisa wa ubalozi wa Iran, hapakuwa na uhalali wowote wa kuwaua. Zingalitumika njia za kidiplomasia kuwashughulikia kama kweli walikuwa wakiwasadia wapinzani. 

Mradi kwa kuwa kosa limekwishatendeka na wale waliokufa ndiyo hamekwisha kufa, hawatarudi tena, na nchi mbili hizo ni za Kiislamu na zimekubali kutekeleza sharia za Kiislamu, basi ni lazima watumie sharia hiyo kutatulia mgogoro huo. 

Kwanza wale wanaotuhumiwa kusababisha mauaji hayo wafikishwe katika vyombo vya sharia. Wakionekana kuwa wametenda hilo kwa makusudi wapewe adabu kwa mujibu wa sharia na kama itabainika kuwa mauaji hayo yalitokea kwa bahati mbaya na hayakupangwa, basi wafiwa wapewe fidia kwa vifo hivyo. 

Hakuna sababu ya kutaka kuupalilia uhasama unaoweza kupelekea kuvunjika kwa amani na kukosekana utulivu katika nchi hizo. 

Habari zisizothibitishwa zinasema eti Iran ina nia ya kuishambulia kijeshi Afghanistan. Lakini inasita kufanya hivyo mpaka inahakikishiwe na Marekani kuwa haitaingilia kati kukisaidia Afghanistan. 

Ndiyo maana Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo anakusudia kukutana na Waziri mwenziwe wa Marekani kupata uhakikisho huo. Kama habari hizo zina ukweli wowote inafaa Iran ichukue hadhari kubwa kabla ya kufanya uamuzi wa namna hiyo. 

Isisahau ule usemi maarufu wa Marekani wanaoupenda kuukariri mara kwa mara, kwamba Marekani haina rafiki wala adui wa kudumu bali ina maslahi ya kudumu. 

Inasemekana kuwa Iraq kabla ya kuivamia Kuwait, kwanza iliomba ridhaa ya Marekani, na ilipozipata ndiyo ikajiingiza Kuwait. Baadaye Marekani ikaigeuka Iraq na kuunda umoja wa kijeshi wa nchi mbalimbali na kuipiga Iraq na kuziharibu silaha za nchi hiyo. 

Marekani ilikuwa ikitafuta kisingizio cha kuziharibu nguvu za kijeshi za Iraq kwa vile zilikuwa ni tishio kwa Israel. 

Kabla ya hapo Israel ilikwishaishambulia Iraq kwa kisingizio kuwa Iraq ilikuwa ikitengeneza silaha za nyuklia. Na kumbe hata Israel yenyewe ilikuwa ina silaha za aina hizo. Na wala Marekani haikuona haja ya kuunda jeshi la kuipiga Israel kwa kitendo chake hicho. Kama ni uhalifu kwa nchi za Mashariki ya Kati kuwa na silaha za nyuklia, basi Israel inazo silaha hizo? 

Huko nyuma Marekani ilikuwa na ushirikiano mkubwa na Iran ilipokuwa chini ya utawala wa Shah. Lakini tokea kufaulu kwa mapinduzi ya nchi hiyo na kutangaza kufuata mfumo wa serikali ya Kiislamu, Iran ikageuka ni adui mkubwa wa Marekani. 

Uhasama huo umekuwa ukiendelea hadi hivi leo. Marekani imekuwa mara kwa mara ikidai kuwa Iran inasaidia ugaidi wa kimataifa na kwamba inataka kumiliki silaha za nyuklia. 

Je! Iran haioni kuwa kutafuta ridhaa ya Marekani kuishambulia Afghanistan kuwa huenda ukawa ni mtego wa kutaka kuzivunja nguvu za kijeshi za nchi hiyo, kwa vile, machoni kwa Marekani ni tishio kwa usalama wa Israel? 

Kiongozi wa juu kuliko wote nchini Iran Bwana Ali Khamenei amekaririwa akisema kuwa nchi yake haitaishambulia Afghanistan. Na sisi hatuna sababu ya kuyatilia mashaka maneno yake hayo, hasa kwa vile kiongozi wa nchi tu, bali pia ni kiongozi wa kidini na tena ni mwanachuoni mwenye kutegemewa. Ikiwa Allah (sw) anasema: " na suluhu ni kitu bora", (An Nisaa 4:128). Kwa nini hatutafuti suluhu, tukafuata kile kilicho bora? 

Muislamu wa kweli ni yule anayeifuata Qur’an Tukufu kwa vitendo na siyo kuisoma tu kama nyimbo! Qur’an inasema: " Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala msizozane, msije mkaharibikiwa, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri". (Al Anfaal 8:46). Waislamu tuzinduke! Tusiziangamize nguvu zetu kwa Smikono yetu wenyewe. 


Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’

Na Mwandishi Wetu 

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayotawala katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikidai kila inapopata fursa ya kujinadi kuwa inaongozwa kwa kanuni na sheria. 

Lengo lake ni kuitaka dunia ielewe na kuamini hivyo. Ndiyo kusema kwamba CCM inaongoza Tanzania kwa kufuata na kutii katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama. Katiba ambayo katika sehemu ya kwanza juu ya haki ya kuishi, kifungu cha 14 inasema: "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata toka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria". 

Kwa msingi huu, serikali imekula kiapo cha kulinda uhai wa kila raia wake kwa gharama yoyote ile. Ndiyo maana tukawa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi (Usalama), Mahakama na vyombo vinginevyo. 

Serikali yoyote isiyokuwa ya kiimla huweka utaratibu ambao watuhumiwa hukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria bila kujali ukubwa wa kosa wanalotuhumiwa kwalo. 

Hata kama mtu amediriki kumlenga mwenzake risasi na kumuua kama mnyama, bado hukamatwa kama mtuhumiwa wa mauaji na kufikishwa mahakamani kama mtuhumiwa. Wakati wote huu kabla ya kesi kusikilizwa na hukumu kutolewa mhusika huendelea kujulikana kama mtuhumiwa. 

Rejea Katiba 13 6(b) "Ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo". 

Mtu yeyote atakayemuua au kumchukulia hatua mtuhumiwa kabla ya kesi kusikilizwa na hukumu kutolewa huchukuliwa hatua endapo yupo katika nchi iliyostaarabika ambayo kweli inaongozwa kwa kanuni na sheria. 

Ndiyo maana akina Mladich wa Bosnia na akina Akayesu wa Rwanda wanapewa nafasi ya kusikilizwa katika mahakama za kimataifa japo upo ushahidi wa wazi kuwa wamehusika na mauaji ya maangamizi (genocide) katika nchi zao. 

Mfano wa nchi zilizostaarabika katika nyanja hii ya utawala wa sheria tumeupata hivi karibuni pale Waziri mmoja wa nchi moja huko Ulaya alipojiuzulu kufuatia kuteswa na polisi kwa binti mmoja wa Kinigeria ambaye alifariki. 

Hapa kwetu Tanzania ni jambo la kutilia mashaka endapo matendo ya viongozi wa CCM wanaotawala sasa yanalingana na kauli zao kuhusu utawala wa sheria. 

Suala la mauaji ya Mwembechai la Februari 13 mwaka huu ni moja tu ya sababu za kuwa na mashaka haya. Hii ni kwa sababu kila kiongozi wa serikali aliyepata fursa ya kuongelea jambo hili kuanzia Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani hadi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wametetea mauaji yale bila aibu wala woga wowote. 

Hawakuonesha kujali katiba wala kanuni za sheria zilizopo nchini. Hata wale Maaskofu ambao wanaamini kwambaa moja ya sheria kuu za Mungu ni kuwa "usiue" na kuwa "ukihukumu utahukumiwa" katika hili walikuwa pamoja na wale walioua! 

Katika nchi zingine zenye demokrasia, vyombo vya habari husaidia sana serikali kubakia kwenye mstari kwa kuandika mambo kwa ukweli na umakini. Jambo hili husaidia serikali kujirekebisha pale inapopotoka na kuipa fursa kufahamu maoni ya watu (public Opinion) juu ya masuala mbalimbali yanayojitokeza nchini. 

Hapa kwetu baadhi ya vyombo vya habari vimejaa unafiki ambao badala ya kusaidia taifa hili huenda ukalibomoa. Baadhi tu ya vigezo vya unafiki huu ni jinsi suala la mauaji ya Mwembechai lililochukuliwa kama kisingizio cha kuwasakama Waislamu hali ambayo pia ilijitokeza katika mkasa wa kupigwa mabomu balozi za Marekani za Dar es Salaam na Nairobi. 

Mara JWTZ itapambana na Mujahidina, mara mashirika ya Kiislamu yanafadhili magaidi, mara Osama bin Laden ana benki Dar es Salaam na mfano wa hayo. 

Wimbi la unafiki wa baadhi ya vyombo vya habari lilijitokeza wazi zama za serikali ya awamu ya pili. Mfano ni pale ambapo mara kwa mara zilitolewa takwimu kulimlinganisha Rais Ali Hassan Mwinyi (The People’s President) na Baba wa Taifa Julius Nyerere juu ya suala la kusamehe watu waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifo na mahakama kuu kama ile ya Rufaa. Vichwa vya habari kama vile "Mwinyi aliua wengi kuliko Nyerere" vilikuwa vikitanda magazetini kila mara. 

Ni vigumu sana mtu kuelewa lengo mahususi la habari hizi. Tunaweza kudhani kwamba mwandishi anataka wasomaji wawabaini ni nani kati ya Marasi hao wawili wa zamani anahuruma zaidi kwa watu wanaostahili kunyongwa. Lakini pia huenda atataka wasomaji wajue kuwa Ali ni Muislamu na Julius ni Mkristo. 

Au labda mwandishi alitaka wasomaji wajue kuwa Rais aliyetumia zaidi kifungu cha 45 .1 (a) cha katiba ya nchi ni Nyerere. Kifungu hiki kinasema hivi Juu ya uwezo wa kutoa msamaha: 

" Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo: Kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote " 

Huu ni unafiki kwa sababu mtu yeyote anayetetea kifungu cha 45.1(a) hawezi kuvinyamazia vifungu vingine vinavyoambatana na hivi kama kile cha 14 na 13. 6(a). 

Tunaweza kuviacha vyombo vya habari vyenye mtazamo huo kwa vile vinao uhuru wa kuamua nini waandike na nini waache. 

Swali hapa ni je, serikali nayo inao uhuru wa kuchagua sehemu fulani ya katiba na kuacha kuitekeleza sehemu nyingine? Kimsingi ni kuwa serikali iliyowekwa madarakani na wananchi haina mamlaka ya kuibeza achilia mbali kuivunja katiba. 

Katiba inaonyesha wazi kuwa hapana mtu au chombo kingine mbali na mahakama chenye uwezo wa kutoa adhabu ya kifo kwa Mtanzania yeyote. Yeyote atakayekiuka hili amevunja Katiba na anastahili kufikishwa katika vyombo vya sheria ili akaeleze sababu za kuivunja katiba. Akipatikana na hatia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. 

Kutokana na ukweli huu, serikali inayokubali wananchi wake wauliwe kwa vigezo vya wananchi wenye hasira inakwenda kinyume si tu na katiba bali pia ahadi ilizotoa wakati wa kuomba kura. Kwa Rais na Mawaziri wa serikali hiyo pia wanaenda kinyume na viapo walivyo kula vya kuilinda katiba. 

Ni jambo la kutisha sana kuwa pamoja na kuongezeka kwa idadi ya Watanzania wasio na hatia inayostahili kuuawa wanauliwa kila uchao kwa jina la wananchi wenye hasira bado serikali haijatoa tamko wala msimamo wake kukomesha mauaji haya. 

Ni kizazi gani tunachokilea ambacho kinamponda mawe mtu na kisha kumchoma moto hadi kufa kwa kisingizio cha kuiba shilingi kumi, au kupora saa au pochi au hereni? 

Ni wananchi gani hawa wenye hasira wanaomshikilia bango kibaka hadi akate roho lakini hawajaweza kuhoji wale wanaokula kodi zao, waliofilisi Urafiki, Textile, Sungura Textile, KAMATA, UDA, UFI, Tanganyika Parkers, Printpak n.k.? 

Ni wananchi gani hawa wenye hasira ambao hawawezi kuwahoji wale walioihujumu nchi na kuzorotesha maendeleo yao hadi kuambiwa eti leo hii wanaishi Tanganyika badala ya Tanzania? 

Na wananchi gani hao wenye hasira ambao mabinti zao wanalazimika kuwa machangudoa na vijana na ndugu zao wanalazimika kuwa vibaka kwa sababu ya mipango duni ya maendeleo na huduma lakini hawawezi kuwahoji wale wanaohusika? 

Serikali ingepaswa itambue kuwa hili ni wimbi la mauaji na athari zake ni kubwa. Kwanza kuwajenga wahusika waone kuwa maisha ya mtu hayana thamani. Pili kuwajenga wahusika kuona wepesi wa kukanyaga na kutembea juu ya maiti. Haya yanapatikana Afrika Kusini, Palestina, Israeli, Rwanda, Burundi, Bosnia, Cosovo, nk. Japo kila mmoja katika hao anayo sababu yake ya kufika hapo lakini wote wanakumbwa na tatizo la roho ngumu za raia wao ambao hawajali wala kuogopa siyo tu kuua bali hata kuuliwa. 

Sisi hapa Tanzania ni bora tuuwahi udongo ungali maji. Tuwaone wale wanaojichukulia sheria mkononi na kuwaua wenzao kama wakosaji au kama wauaji. Polisi ni lazima wawalinde raia badala ya kuwalinda viongozi kama wanavyofanya sasa. 

Kama serikali imeweza kuwaweka polisi katika Msikiti wa Mwembechai kuanzia Februari hadi leo Oktoba 1998 kwanini ishindwe kuweka polisi katika maeneo yanayoongoza kwa vitendo vya uhalifu. 

Kuna dhana eti wananchi wanaouliwa wanapopelekwa polisi huachiliwa kwa hiyo bora wahukumiwe kifo na raia wenzao. Je, polisi hawa wanafanya kazi kwa matakwa yao au ya nchi ? Je, Wizara ya Mambo ya Ndani imechukua hatua gani kukabiliana na tuhuma hizi? 

Kwangu mimi wananchi wenye hasira ninaowafahamu ni kama wale wanaopatikana kule Indonesia ambao walisimama kidete kumwondoa Rais Suhato kwa madai ya kuhujumu uchumi wa nchi. Wengine wa mfano wa hawa ni wale wanafunzi (Taleban) waliokatisha masomo yao ili wakaikomboe nchi yao yaani Afghanistan. 

Hawa wa kwetu ningependa watambulike kama wauaji kwa mujibu wa katiba ya nchi na magazeti yote na yeyote anayeendelea kuwatambua kama wananchi wenye hasira achukuliwe hatua za kisheria. 

Ni wajibu wa CCM na serikali yake kuwaondolea wananchi wa Tanzania kero zote ambazo baadhi yake zinapelekea vijana wengi kukimbilia mijini na hatimaye kujihusisha na vitendo vya kihalifu. 

Maisha ya vijijini ni lazima yaboreshwe katika nyanja za mawasiliano, shule, maji, hospitali n.k. Mito iliyopo mikoani itumike katika shughuli za umwagiliaji ili kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji. 

Ni lazima serikali ipambane na wale wanaondelea kulihujumu taifa hili kwa kutumia madaraka yao. 

Ikumbukwe kwamba uhai ni mali ya Mungu Muumba hakuna awaye yeyote anaweza kutoa uhai. 
 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita