AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Historia ya sayansi na tiba
Na Dk. Amur A.A. 
(aamur@cc.muchs.ac.tz)

UTUNZAJI wa afya kwa umma likiwa kama suala la afya ya jamii limekuwepo kwa muda. Katika kipindi cha kati (1500 – 1450) wanatiba wa Kiislamu walitoa mchango mkubwa uliokuwa na ufanisi mkubwa kwa Bara la Ulaya ambayo baadaye iliongezea kwenye maendeleo ya sayansi ya utibabu. 

Wasomi hawa wa Kiislamu waliendeleza mafundisho ya kitibabu kiutendaji na kinadharia. Matabibu na waandishi wa mwanzo kama Ibn Sina, El Birun, Al-Rhazi, El Kind na Ibn Thabit walitoa mchango wa kazi zao nyingi bora ambazo zimebaki kuwa shani kubwa mpaka hivi leo. 

Al Khazi alitoa machapisho 237 ambayo yalizama zaidi katika fani ya madawa. Kazi yake juu ya magonjwa na matibabu kwa watoto (Paediatrics) ilimpelekea wasomi kumwita Baba wa fani hiyo. 

Alikuwa mwanazuoni wa kwanza kuelezea dalili za kikohozi/mafua, ndui na surua. Shirika la afya la duniani (WHO) katika shukrani yake kwa Al Rhazi kwa maandishi yake juu ya magonjwa ya ndui na surua yanaonyesha uhalisi na usahihi na vile vile alikuwa wa mwanzo kutoa makala zake juu ya magonjwa yaambukizayo. 

Wakati wa utawala wa Waislamu nchini Spain, Cordoba ilikuwa ni kituo cha mafunzo kwa Ulaya yote. Wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali walikuja Cardoba kujifunza na kufanya utafiti. 

Katika karne ya tisa ambapo maktaba ya Mtakatifu Gall iliyokuwa kubwa kuliko zote Ulaya ilikuwa na vitabu 36. Maktaba ya mji wa Waislamu ya Cardoba ilikuwa na zaidi ya vitabu laki tano (500,000). 

Dhana ya huduma za hospitali iliazimwa pia kutoka kwa Waislamu. Hospitali wakati huo zilikuwa chini ya usimamizi wa Makhalifa kwa makusudi ya ukuzaji afya, kutoa huduma za matibabu, kufanya utafiti na mafunzo. Kila mji mkubwa ulikuwa na hospitali yake iliyokuwa na wodi tofauti za magonjwa ya homa, kuhara damu, macho na upasuaji. Mwaka 930 Ibn Thabit alieneza huduma hizi kutoka mijini mpaka vijijini na magerezani. Mpango ambao ni hivi majuzi tu umeanzishwa na nchi Magharibi. 

Wazo hasa la kuanzishwa kwa Chuo lilitoka kwa Waislamu kwenda Magharibi na kujumuisha athari kubwa katika maendeleo ya sayansi. Mfumo wa ndani wa vyuo vya nchi za magharibi hautofautini na ule wa vyuo vya Kiislamu. 

Kwa mfano maneno/dhana; "Graduate" na "Under graduate" yametokana na istilahi za Kiislamu "Sahib" na "Mutaffaqqin". Katika karne ya 13 Ibn Nafis alielezea mzunguko wa damu kutoka mapafuni na utendaji kazi wa kifiziolojia wa moyo. 

El Birun katika mwaka wa 1052 alitoa kitabu maarufu kwa ajili ya utayarishaji na utoaji madawa. Ibn Sina yeye alielezea kazi ya mlo kamili na athari ya mazingira na hali ya hewa juu ya afya. 

Kazi yake mashuhuri "Al Qumin" ilikuja kuwa kitabu cha rejea mpaka karne ya 19. Kitabu hiki kilijisheheneza katika ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kujaa kwa maji kwenye korodani (busha), uzalishaji sumu, kihamsi cha uso, vidonda na aina kadhaa za homa ya manjano na matibabu yake. 

Ibn Sina aliweka sheria na kanuni za majaribio katika kutibu ambazo bado ni muhimu na zenye nguvu mpaka leo. 

Mtizamo wa mafunzo ya kitabibu unahitaji kubadilishwa upya ili kwenda sambamba na ongezeko la haja ya ubora wa utunzaji afya, suala lililopo la ufikishaji siha huacha mengi yatamaniwayo katika utekelezaji wa hatua za kushughulikia mifarakano, raghba na mahusiano katika utabibu. 

Shughuli yote inaegemea katika uwezekano wa kurudisha siha na kumrudisha tena mtu katika jamii. Wagonjwa hawana budi kumuwezesha daktari kufahamu maisha na tabia za wagonjwa wake. 

Hivyo changamoto ni kuanzishwa kwa mafunzo ya kitabibu ili kuwaelimisha matabibu juu ya maadili na thamani ya fani hii. 

Semina iliyotayarishwa na chama cha madaktari wa Malaysia Juni, 1996 ilizitetea nafasi sita zilizopo katika fani ya Kiisalmu ya kutibu magonjwa ambazo ni: 

Kusudio la matibabu ni kudumisha na kuyapa maisha hali bora zaidi na wala si kuahirisha au kuzuia kifo kisitokee. 

Kielelezo cha Tawhiid chahitaji mtaala ulioanzishwa ambao fani hii ya utibabu hufundishwa. 

Chaguo na mafunzo ya mwanafunzi wa fani hii visisitize zaidi kutoa huduma ndani ya mfumo wa Uislamu wa jamii wa kusaidiana. 

Madaktari lazima wawe viongozi wa jamii ambapo tabia na maadili mema ndiyo iwe mifano kwa wengine. 

Madaktari wajao ni lazima watayarishwe kufanya utafiti na kupanua mipaka ya elimu hii. 

Mfumo wa elimu ya utibabu (wa sasa) lazima umhamasishe tabibu wa kesho kufuata mifano bora ya madaktari Waislamu wa mwanzo. 

Ukweli wa mafunzo ya utatibu huleta shauku kuwa katika ulimwengu huu ukuao kitaaluma mbalimbali, maadili ya utabibu yanapaswa kulenga katika kuongeza kiwango cha elimu na stadi za sayansi ya utabibu kwa mujibu wa maadili, tabia na thamani. 

Nguvu ya maadili ni muhimu sana katika kuboresha matumizi ya afya mpaka kuridhiwa na wagonjwa. Dhana ya matumizi ya Kirazini ya dawa iliyogundulika toka wkati wa utengenezaji dawa wa kipindi cha Medeval na kufikia kipeo cha juu cha utibabu chenye manfuaa kwa mgonjwa. 

Kuanzishwa tena kwa mafunzo ya utabibu chini ya misingi ya maadili ya Kiislamu kutachangia utendaji mzuri katika mfumo wa utunzaji afya kwa kuwa na watu wenye maadili na tabia njema katika taaluma hii adhimu. 

Nidhamu zilizoratibiwa vyema za kitabibu na usambazaji mkubwa wa ujuzi huu kutoka kwa matabibu wa Kiislamu wa mwanzo ni msingi mkubwa wa uzima wa taaluma hii kwa sasa. 

Japokuwa mchango mkubwa wa Waislamu katika fani ya uganga si wenye kutambuliwa, lakini mchango huu ulikuwa na dhana kubwa sana katika mabadiliko na maendeleo ya sayansi ya utabibu. 

Ni ukweli kwamba mpango wa afya kwa umma kwa Waislamu ulikuwepo miaka mia nane kabla ya kuingizwa Ulaya ya Magharibi 
 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita