AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
MAKALA ya JAMII
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad
Usijishushe hadhi kitaaluma
Na Sheikh Aboubakar Mwilima

Tunashindwa kuvumilia kuona juhudi kubwa inayofanywa na Profesa Kaisi ya kumzushia Mtume Muhammad (s.a.w) na kumsingizia aibu asizokuwa nazo. Baya zaidi ni pale anapojaribu kupotosha hadithi za Mtume ili awaridhishe Wakristo wenzake. Hatushangazwi na mwenendo na malezi hayo ya Kanisa ya kuzua na kuandika yasiyokuwapo. Mwenendo huo ni dhidi ya maadili ya kidini na uandishi wa kitaaluma.Katika toleo la Msema kweli Na.030 la Septemba 27, 1998, Profesa Kaisi amezua uongo eti Hadithi Na.1404 katika Sahihi Muslim Juzuu ya II, Mtume (s.a.w) aliwahimiza maswahaba wake kubakana waume kwa waume, baada ya kukosa wanawake kwenye vita vya AUTAS. Hadith hiyo inasimulia kisa cha swahaba mmoja aliyeishi mbali na msikiti wa Mtume (s.a.w) pale Madina. Pamoja na umbali huo alikuwa hachelewi au kupitwa na swala yoyote. Kwa tukio hilo Mtume (s.a.w) alielezea ubora wa kutembea hatua nyingi kwenda Msikitini, kwani kunampatia thawabu nyingi huyo mwenye kuswali. 

Kuhusu vita vya AUTAS, ambavyo vimeandikwa katika vitabu karibu vyote vya Hadithi za Mtume (s.a.w); hamna, tena hamna habari ya maswahaba wa Mtume kubakana waume kwa waume, wala kuhamasishwa na Mtume. Kwa kutojua au chuki yake tu, Mtume hakushiriki vita hivyo. Jeshi la Waislamu liliongozwa na Abu Ameir na Abu Mussa Ash’ariy na walipata ushindi dhidi ya makafiri. (Rejea Taju Jamiul-Usuli Fii Ahadithi Rasuli - Juzuu 4 uk.433-34). 

Profesa Kaisi alijaribu tena kuzua uwongo katika Hadithi Na.1456 - Muslim Juzuu Na.I, uk.335: Hadithi hii inasimulia juu ya mtu aliyesahau kutekeleza swala yake, au alikuwa amelala wakati huo wa ibada; basi Mtume (s.a.w) alisema kuwa mtu huyo atawajibika kuswali swala hiyo mara tu atapokumbuka au kuamka ikiwa alikuwa amelala. Wasimulizi ni Qatada na Anas bin Malik (R.A). 

Kuhusu Hadithi Na.139 - Bukhari Juzuu ya 6: 

Hadithi hii imesimuliwa na Abdullah (r.a.) ambaye alisema: 

"Tulikuwa tukishiriki katika vita vya Jihad vilivyoendeshwa na Mtume (s.a.w) hatukuwa pamoja na wake zetu. Kwa hiyo tulimwambia Mtume (s.a.w) "Je tujihasi?" Lakini Mtume (s.a.w) alitukataza kufanya hivyo. Papo hapo akatuamuru kuoa japo kwa kuwapa wanawake hao nguo kama mahari yao; na kisha akasoma aya hii: 

"Enyi mlioamini msiharamishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msiruke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka". Qur-an Sura (5:87). 

Hii ndoa ya muda iliitwa Mut’a; iliruhusiwa katika siku za mwanzo za Uislamu, kisha baadae katika vita vya Khaibar iliharamishwa. 

Katika Hadith hiyo tuliyoinukuu hapo juu hamna kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w) kuhalalisha liwati, au kuhamasisha maswahaba wake wafanye hivyo. Ubaya wa kulawitiana umeelezwa vizuri sana ndani ya Qur-an Sura (7:80-84). 

"Na tulimpeleka Luti. Basi (wakumbushe watu wako alipowaambia kaumu yake. "Je mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieni yoyote kwa (jambo chafu) hilo katika walimwengu!" 

"Ninyi mnawaendea wanaume kwa kuwa ndio mnaowatamani badala ya wanawake! Ama ninyi ni watu wafujaji." 

"Na hayakuwa majibu ya kaumu yake isipokuwa kuambizana wafukuzeni katika mji iwenu, maana hao ni watu wanaojitakasa (hawataki haya machafu tunayoyafanya. Basi nawatoke. Wanakalia nini?" 

"Basi tukamuokoa yeye (Luti) na watu wake isipokuwa mke wake, alikuwa miongoni mwa waliokuwa nyuma (wakaangamizwa) 

Na tukawamiminia mvua kubwa (ya adhabu). Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa waovu (hao). 

Tumenukuu aya hizi chache za Qur-an Takatifu ili kuwa mfano wa tegemeo la Mtume (s.a.w) katika kulipitishia hukumu suala hili la liwati katika Uislamu na jamii nzima ya kibinadamu. Aya nyingine nyingi zimo ndani ya Qur-an, bali hizi zatosha kutolea hoja. 

Msimamo wa Uislamu juu ya suala zima la liwati: 

1. Wanaolawitiana wapigwe kwa mawe hadi wafe; wala pasiwe na ubaguzi kwamba huyu ana ndoa na yule hana. 

2. Mtume (s.a.w) Amesema: "Wataokutwa wanafanya matendo ya Kaumu Luti, basi muueni mtenda na mtendewa. (Abu Dawud, Tirmidh n.k.). 

3. Baada ya Mtume (s.a.w) kufariki, maswahaba wake walitekeleza hukumu hii ya kuwaua mashoga hao. Abubakar, Ali na wengineo waliwaua na kuwachoma moto, au waliwapiga kwa mawe tu hadi kufa. 

Bila shaka Profesa Kaisi kaona uongo wake unavyopingwa na kumbukumbu sahihi za maisha ya Mtume na Maswahaba wake walivyokuwa waadilifu katika mambo ya dini na jamii kwa ujumla. 

4. Adhabu hiyo imetolewa kwa waovu hao kwa vile wanakiuka maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu. Rejea Qur-an Sura 26:165-166; na Sura Al-Ankabut 29:30-31. 

5. Maimamu Bukhari, Nasai, Tirmidh na wengineo wamemripoti Mtume Muhammad (s.a.w) kuhusu suala la liwati kwamba alisema hivi: 

(a) Mwenyezi Mungu Mtukufu hatamwangalia mwanaume anayemlawiti mwanaume mwenzie, au kumlawiti mwanamke". (Nasai, Tirmidh) 

(b) Watu watatu hawatakubaliwa shahada zao "Lailaha illa llahu" - mabaradhuli wa kiume, mwanamke msagaji na anaesagwa, na Imam muovu (Tabraniy) 

(c) Watu saba Mwenyezi Mungu Mtukufu hatawaangalia Siku ya Kiyama, wala kuwatakasa, na atawaambia waingie motoni pamoja na wanaoingia humo. Mtenda na Mtendewa mpiga punyeto kwa mkono wake, anayemwingilia mnyama, anaemtenda mwanamke, anaemwingilia mwanamke na binti yake, pamoja na mzinzi anaemzinia jirani yake mkewe, na mtu anaemuudhi mno jirani yake hadi kufikia kumlaani. 

(d) Mwenyezi Mungu, Malaika na wanadamu wanawalaani walawiti ina kuwakasirikia. 

6. Kuhusu Qur-an Sura 4:16 - Profesa Kaisi anakosoa Qur-an eti inaruhusu watu kulawitiana na kusamehewa tu. Tofauti na Taurati inayotoa adhabu kali ya waovu hao kuuliwa. Naomba asome aya 17 ya sura hiyo hiyo ili aelewe masharti mawili yanayotolewa na Mwenyezi Mungu Mwenyewe ili waovu hao wapokelewe toba zao. Kwanza ikiwa kosa hilo wamelifanya kwa ujinga na pili ikiwa wakishatambua kosa lao watubie haraka sana. 

7. Suala la kuoga janaba - hata kwa walawiti ni amri. Janaba ni hali anayoipata mtu ikiwa atatokwa na manii, au kuingilia au kuingiliwa katika njia mbili za mbele au nyuma kwa kuzini au kulawiti, au kutoa manii kwa mkono (masterbation) atapaswa kuoga janaba. Usipofanya hivyo huwezi kuswali, kusoma Qur-an, kuigusa, kuichukua au kuingia nyumba ya ibada na kadhalika. 

8. Madhara ya Liwati kwa jamii na mtu binafsi: 

Ni kosa la kuharibu maumbile ya kibinadamu 

Kulawiti kunaharibu vijana, kwani ni matamanio yaliyovuka mipaka ya ubinadamu kwa uovu wake 

Kulawiti kunawadhalilisha wanaume wanaotendwa hivyo 

Kulawiti kunawaharibu wanawake, hukimbia waume zao, huharibu njia za uzazi. 

Kulawiti kunaharibu wanaume kupoteza dhamana yao ya kuwa na familia na kuzikimu ipasavyo. 

Kulawiti kunapunguza kuzaliana, wanaume hukacha kuoa wanawake. 

Kulawiti hueneza maradhi mabaya ya kaswende, kisonono, tego na sasa ukimwi. Na huyo mwenye kulawitiwa hufikwa na zahama kubwa. 
 

 Itaendelea toleo lijalo. 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita