AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Sensa ya majaribio 

Wananchi watofautiana na serikali 

Wadai ufujaji fedha umekithiri 

Na Rajab Rajab - Morogoro

BAADHI ya wananchi mjini hapa wameonyesha kutoridhishwa kwao na maamuzi ya Serikali kufanya sensa ya majaribio na kudai kuwa huo ni ufujaji wa fedha unaofanywa na serikali kwa lengo la kuwanufaisha wachache. 

Wakiongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti mapema wiki hii wananchi hao wanawake kwa wanaume wamedai kuwa kama ni majaribio tayari serikali iimekwisha kufanya na kupata uzoefu tangu sensa ya 1978 na 1988, hivyo majaribio hayo hayakustahili kuwapo bali ilitakiwa kutekeleza sensa ya kila baada ya miaka kumi kama ilivyojiwekea. 

"Hatudhani kama serikali yetu imefanya vyema kufanya sensa inayoiita ya majaribio ambayo imetumia mamilioni ya fedha huku wananchi wake wakikosa huduma muhimu kwa kisingizio serikali haina fedha", alisema Bi. Christina Mwaipopo aliyejitambulisha ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro. 

Naye Bw. Mussa Salum Mkeri wa Kiwanja cha Ndege mjini hapa amedai kuwa serikali ina agenda ya siri kuhusu sensa ya majaribio kwani hakuna mantiki yoyote kufanya sensa hiyo wakati sensa kuu ni mwakani. Alisema Bw. huyo bila kufafanua. 

Akitoa mchango wake juu ya sensa hiyo Bw. Hashim Hamza ambaye ni mwanafunzi wa masomo ya uchumi mwaka wa pili IDM - Mzumbe amesema kuwa serikali haikuwa na sababu yoyote ya msingi kuweka sensa hiyo ya majaribio. 

"Sioni kama kulikuwa na ulazima wowote wa kufanyika sensa hiyo, wakati tunatarajia kufanya sensa ya jumla sasa hii hali inachangia kudumaza uchumi wetu kutokana na fedha kutumika ovyo", alisema mwanafunzi huyo. 

Akieleza malengo ya sensa hiyo wakati akiongea na vyombo vya habari hivi karibuni Kamishna wa Sensa hiyo Dk. Damas Mbogoro amesema wanafanya hivyo ili kupata uzoefu wa mazingira hususan mabarabara kutokana na nyingi kuharibiwa na mvua, pamoja na kuangalia maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu. 

Sensa hiyo ya wiki moja inafanyika katika miji ya Iringa, Bagamoyo, Wilaya ya Makete, Wilaya ya Kahama na Kusini Pemba katika Wilaya ya Chache Chake. 

Sensa hiyo itagharimu zaidi ya shilingi milioni 60 ikiwa ni posho kwa maofisa wa sensa wapatao 238 pamoja na vifaa vingine vinavyohitajika katika sensa hiyo. 

Sensa ya Kitaifa inatarajiwa kufanyika Agosti 29,1999 baada ya kushindikana kufanyika mwaka 1997 kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa kipindi kirefu. 
 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita