|
|
|
Watu wa karne ya 15 AD wametuachia magofu mengi ya Misikiti na makaburi katika miji yao. Mnamo katikati ya karne ya 15 AD kwa mujibu tarehe ya Kilwa (Kilwa Chronicle) mtawala wa kienyeji Zanzibar alikuwa Sultan Al Hassan bin Abubakar. Ama karne mbili zilizofuatia, 16-17 zilikuwa kipindi cha hofu na wasi wasi mkubwa kwa Waislamu katika miji yote ya Mwambao kwa sababu ya Wareno waliofika wakti huo ambao waliwanyang’anya Waislamu mali zao na kudai mali nyingi kama kodi, waliopinga, miji yao iliangamizwa na Wareno. Hayo yalitokea kwa mji wa Zanzibar. Wareno sio tu walitaka utajiri, walinuia kuupiga vita Uislamu. Hayo ni pamoja na kujaribu kuwashawishi watawala wa kienyeji kubadili dini na kufuata imani ya Kikristo, ambayo ilikuwa ya madhehebu ya Augustinia. Haya yamehifadhiwa katika vitabu vya historia. Kwa mfano, yalimfia mfalme Muislamu wa mji wa Kilwa walipomwendea Pedro Alvares Cabral mwaka 1500 na Don Fransisco mwaka 1503 AD. Ingawa Wareno hawakufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwatoa wenyeji katika imani ya Kiislamu, misafara ya kibiashara ilizuilika, kwa hali hiyo, hali ya maisha ya Waislamu zikateremka. Misafara ya kibiashara pia ilikuwa na watu waliokwenda huku na kule kutafuta na kufundisha elimu za dini, wote wakaepuka kusafiri. Misikiti haikuendelea kujengwa katika kipindi hicho, baadhi ya viunga vya miji vilihamwa na Misikiti ikawa magofu na kuporomoka kabisa. Hatimaye Wareno walipigwa vita na kuondoshwa kwa msaada wa kijeshi kutoka ufalme wa Oman. Katika karne ya 18 AD hali ilirejea kuwa ya kawaida, ujenzi mpya ukaanza pamoja na jitihada za kutafuta na kuendeleza elimu ya dini. Walimu wa dini walikuja kutoka nchi za Kiarabu, hasa Masheikh wa Kisunni kutoka nchi za kusini ya Bara Arabu, baadhi yao wakiwa ni wafanyabiashara. Pia wakati huo kulikuwa na wimbi la kufufua misingi ya dini lilitokea miji ya Makka na Madina ambako kulikuweko na Masheikh waliopinga Taqlid na kudai kuwa mambo yote katika diin yawe na dailili katika Qur’an na Sunnah. Maarufu katika hao ni Sheikh Muhammad Abdulwahab (1703 – 1792 AD). Kadhalika huu ulikuwa wakati wa kuanza kwa biashara na nchi za Ulaya ambayo baadaye mfalme Said bin Sultan aliiendeleza. Karne ya 19 AD elimu za maarifa ya Uislamu ziliendelea. Watawala wa kifalme kutoka Oman ambao walikuwa wa madhehebu ya Ibadhi walishughulikia dola na biashara hawakuingilia itikadi za Kisunni na Masunni hawakuingilia watu walioitakidi Ushia. Zanzibar ilikuwa sana kiuchumi na kisiasa ilidhibiti karibu mwambao wote na kufanywa kituo kikuu cha biashara yote ya nje hasa mali kutoka bara. Wanazuoni wa miji ya Mwambao walitembeleana kubadilishana elimu na kufanya biashara, walitunga vitabu na kufungua madarasa kubwa kubwa kufundisha elimu ya dini, wengine walikwenda nje kusomesha kama vile Uganda na kwingineko. Kwa hivyo, Zanzibar ikawa pia ni chemchem ya dini. Miji iliyokuwa na Waislamu wengi na dini kuwa na nguvu zaidi, kama Zanzibar, Waislamu wakafikia hatua ya kufuata sharia chache katika Uislamu, zinazohusu ndoa na mirathi na watawala wakiwateua makadhi kushughulikia hayo. Unguja Makadhi wa Kisunni ndio waliokuwa wengi na Pemba Makadhi wa Kiibadhi ndio waliokuwa wengi. Hali ya Zanzibar kibiashara na kiutamaduni iliwavutia sana Wazungu na walikaribishwa na mfalme wa Kioman. Walifuatana na Misheni zao za Kikristo. Hali ya Zanzibar ikazilea Misheni hizo kwa hali ya Mabara ilivyokuwa, haikuwa rahisi Misheni kuanzia huko. Kwa vile Uislamu ushamiri sana Zanzibar, Wamisheni pia walifurahia fursa ya kuanza harakati zao Zanzibar kuendeleza Ukristo, kwa matumaini kuwa wakifanikiwa kubadilisha imani ya Kiislamu Zanzibar itakuwa ni rahisi kuifanya jamii nzima ya Mwambao kuwa ya Wakristo. Mada hii ya shughuli za Wamisheni itaelezwa zaidi, hapa la muhimu nikuwa Wazungu hatimaye walichukua hatamu za dola (ukoloni) wakashika kisu mpini, ikawa Waislamu wameshika kwenye makali. Khatima ya jamii ya Waislamu Zanzibar ikawa katika mikono ya Waingereza. Hal nzima ikabadilika. Elimu zilizoanzishwa na vituo vya Wamisheni na huduma za afya ikawa ni vya lazima katika hali hiyo mpya. Hadi kufikia karne ya 20 ikafifia elimu pamoja na utamaduni wa Kiislamu, Waislamu wakadharauliwa pamoja na dini yao. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri
Mkuu ni ya Waislamu
Kuchomwa nyumba za wananchi
Maoni Yetu:
Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume
Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu
Marekani
Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie
mauaji ya Mwembechai
‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’
Makala ya Kimataifa
Afghanistan washindi dhidi
ya uvamizi karne zote
MAKALA:
Tujikwamue na janga la utwaghuti
MAONI:
MAKALA:
Tufuate Uislamu kwa vitendo
na siyo kwa maneno -2
Tusihalalishe mauaji ya
raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’
Historia ya sayansi na tiba
Msiwageuze watoto ombaomba
MAKALA YA JAMII:
Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana
na serikali
Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 Mwembechai wageuka Hame,
Bado walindwa na polisi
Waislamu Moro waendelea kusaidia
wagonjwa
Mjadala wa Katiba ya Shirikisho
kuzinduliwa Dar Jumapili
Walimu wa dini Tanga wapokea
Baiskeli
Mafundisho ya Quran
Chakula na Lishe
|