|
|
|
Na Kassim Juma TUME ya Jiji Kanda ya Kinondoni imetoa amri ya kusimamisha uuzaji wa nyama ya nguruwe katika maeneo mchanganyiko. Amri hiyo ya Tume imo katika barua yake ya Septemba 29, 1998 iliyosainiwa na Bw. E. B. Paul kwenda kwa mmiliki wa bucha moja iliyopo Hananasif Mkunguni Kinondoni. Aidha, barua hiyo imemtaka mmiliki huyo kumuona Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo kwa ajili ya kile ilichokieleza kuwa kupata maelezo na ufafanuzi zaidi. Amri ya Tume ya Jiji imefuatia malalamiko ya wananchi wa kata ya Kinondoni dhidi ya mmiliki wa Pork Butcher nyumba Na. AN 381. Hata hivyo, imedaiwa kuwa licha ya kuwepo amri hiyo ya Tume ya Jiji, hadi kufikia Oktoba 6, 1998 mmiliki huyo alikuwa bado akiendelea na biashara hiyo. Baadhi ya wananchi waliofika katika ofisi ya gazeti hili wameahidi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa amri hiyo. Wamesema wametoa muda kwa Tume ya Jiji kuhakikisha amri hiyo inatekelezwa, vinginevyo wametishia kuchukua hatua mikononi. Uuzaji na ufugaji wa nguruwe holela umeibua malalamiko sehemu mbalimbali Jijini. Hata hivyo, malalamiko hayo yamekuwa yakikumbana na maelezo ya jumla
jumla au kimya kizito kutoka kwa wahusika.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri
Mkuu ni ya Waislamu
Kuchomwa nyumba za wananchi
Maoni Yetu:
Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume
Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu
Marekani
Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie
mauaji ya Mwembechai
‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’
Makala ya Kimataifa
Afghanistan washindi dhidi
ya uvamizi karne zote
MAKALA:
Tujikwamue na janga la utwaghuti
MAONI:
MAKALA:
Tufuate Uislamu kwa vitendo
na siyo kwa maneno -2
Tusihalalishe mauaji ya
raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’
Historia ya sayansi na tiba
Msiwageuze watoto ombaomba
MAKALA YA JAMII:
Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana
na serikali
Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 Mwembechai wageuka Hame,
Bado walindwa na polisi
Waislamu Moro waendelea kusaidia
wagonjwa
Mjadala wa Katiba ya Shirikisho
kuzinduliwa Dar Jumapili
Walimu wa dini Tanga wapokea
Baiskeli
Mafundisho ya Quran
Chakula na Lishe
|