AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai

Wamchangia mama Chuki sh. 30,000 
  

Na Mwandishi Wetu 

WANAWAKE wa Kiislamu wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro, wamemtaka Rais atoe kauli na kuunda Tume kuchunguza kwa kina vurugu zilizotokea Mwembechai ambazo zilisababisha kuuawa watu wanne na wengine kadhaa kujeruhiwa. 

Wanawake hao walitoa kauli hiyo katika kongamano lao lililofanyika siku ya Jumapili Oktoba 4, 1998 kijijini Mudio tarafa ya Masama Mashariki wilayani humo. 

Kauli ya pamoja ya wanawake hao ilifuatia maelezo ya mtoa mada mmoja katika kongamano hilo aliyeeleza kwa kirefu kadhia ya Mwembechai iliyopelekea polisi kuua raia mwezi Februari mwaka huu. 

Kwikwi za vilio zilisikika hapa na pale baada ya mtoa mada huyo kukumbusha kuwa pamoja na kuwepo dalili zote zinazoashiria kukiukwa Katiba ya nchi, Rais hajazungumzia chochote hadi hivi sasa. 

Wanawake hao waliazimia mwishoni mwa kongamano hilo kutorudia makosa ya kuwarejesha madarakani watu wanaowapuuza baada ya kuwachagua. 

Aidha, walichanga shilingi 30,000 kwa ajili ya pole kwa mama Chuki anaeendelea kumuuguza mwanawe aliyejeruhiwa kwa risasi katika kadhia hiyo. 


‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’

Na Kassim Msuya 

SHEIKH Abeid wa Msikiti wa Manyema Jijini, amesema katika khotuba ya Ijumaa ya Oktoba 2, mwaka huu kuwa serikali pamoja na taasisi zake haiwezi kuzuia rushwa nchini. 

Akiwakhutubia waumini waliofurika kuswali sala ya Ijumaa Msikitini hapo, Sheikh Abeid alisema wakati ambapo taasisi za serikali ndizo zingetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita zenyewe zimekuwa mstari wa mbele katika kupokea, alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni mahakama na polisi. 

Sheikh Abeid amesema, inachofanya serikali ni kuwadanganya wananchi kuwa inapambana haiwezi wakati watendaji wake ndio wanaoongoza kwa ulaji rushwa. 

Amesema sababu kubwa zinazopelekea kuongezeka kwa matendo ya upokeaji rushwa ni mifumo ya maisha iliyoundwa na wanaadamu na akaongeza kuwa hakuna chama chochote kitakachoweza kutokomeza rushwa hapa nchini. 

Akasisitiza kuwa ni Uislamu pekee ndio unaoweza kumaliza tatizo hili kwani Uislamu umeweka namna ya kuzuia kutokea kwa matatizo kama hayo kabla ya hayajatokea. 

Alitoa mfano kuwa, Mtume (saw) siku moja alimtuma mmoja katika wafuasi wake akakusanye zakat alipo rudi akamkabidhi Mtume fungu moja la zakat na kumwambia Mtume (saw) kuwa hili fungu lingine ni la kwangu. Mtume (saw) akakikema kitendo kile na kumwambia anadhani kuwa angekuwa nyumbani kwake angepata fungu lile? Jibu likawa hapana, kwa hali hiyo Mtume akakilaani kitendo kile na kukifananisha haiwezi. Baada ya kunukuu hadithi hiyo, Sheikh Abeid alisema matendo kama hayo yapo mengi na yamekuwa ndio mtindo wa maisha. 

Sheikh Abeid aliendelea kusema leo hii nyumba za Wakfu zinageuzwa mabaa akatoa mfano nyumba iliyotolewa Wakfu na Hajat Aziza Omar na kusema kesi ya nyumba hiyo imeendeshwa kwa misingi isiyoeleweka mpaka hukumu ikatolewa bila upande wa Waislamu kujulishwa mpaka baada ya miezi mitatu kupita. 

Sheikh Abeid alimalizia khotuba yake kwa kuwataka Waislamu kupiga vita rushwa ya namna yoyote ile kwani Uislamu umepinga kila kinachopelekea katika utoaji au upokeaji rushwa. 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita