|
|
| Mishikaki
ya nguruwe Moshi yachomwa mbele ya Msikiti
Na Mwandishi Wetu NYAMA ya nguruwe imekuwa ikichomwa na kuchemshwa hatua chache kutoka Msikiti wa Suni Mjini Moshi na kuuziwa wapita njia. Vibanda viuzavyo nyama hiyo vipo karibu na Ofisi za Mabasi ya Shabaha na imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kutokana na harufu hiyo ya Mishikaki ya nguruwe. Lakini ukaribu wa msikiti kumefanya kero iwe kubwa zaidi. AN-NUUR iliwasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, akadai kwamba washapata habari juu ya kero hiyo. AN-NUUR pia iliwasiliana na Katibu wa Wilaya wa CCM, Bw. Kibaya ambaye alidai kwamba wao CCM wamewapangisha wafanya biashara lakini hawana mkataba wa kuwapangia wauze nini. Mgahawa ambao umekuwa mashuhuri sana kwa uuzaji wa mishikaki hiyo ya nguruwe na zile za kuchemsha unajulikana kwa jina la Kisanga Min-Restaurant - Chekanao - karibu sana na ofisi za mabasi ya Shabaha. Wakati huo huo, biashara ya kuuza nyama ya nguruwe mbichi, mishikaki na ile ya supu imekuwa ikishamiri katika maeneo yafuatayo Jijini Dar es Salaam. 1) Katika barabara ya kutoka Sigara kuelekea Bonde la Msimbazi hadi Vingunguti karibu na nyumba moja ya ghorofa. 2) Katika barabara ya kutoka Sigara kwenda Chang’ombe (barabara ya kokoto) kwenye njia panda karibu na mti mkubwa. 3)Karibu na maghorofa ya Kota za Chang’ombe kati ya barabara inayoelekea Kimanga/Kisukuru na inayoelekea Segerea kutoka kituo cha mwisho cha mabasi ya Tabata/Chang’ombe. 4) Katika Bar moja inayoitwa Angala Bar (Kiti Moto) karibu na Hai Bar iliyoko Tabata. 5) Karibu na Hotel ya Aroma kwenye njia ya miguu inayoelekea Matumbi Bar karibu na reli (sehemu hii inauzwa kila siku). Bisahara hiyo imekuwa ikiongezeka sambamba na ufugaji wanguruwe usiozingatia sheria. Katika kikao cha pamoja cha Misikiti ya Liwiti, Tabata, Kimanga, Kisukuru na Segerea, Waislamu wameitaka Serikali ichukue hatua kabla ya wananchi wakereketwa kuchukua hatua wao wenyewe. |
YALIYOMO
TAHARIRI Serikali iwahurumie wananchi wake KUCHOMWA MOTO NYUMBA ZA WANANCHI:
Nzasa wamtaka Mkapa awaonyeshe pa kwenda
Mishikaki ya nguruwe Moshi yachomwa
mbele ya Msikiti
MAONI YETU:
Upimaji huu mpya ni wa nini
TANGAZO LA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI Ndoa si lengo, ni wasila wa kufikia
lengo
Makala:
Goda Muslim School, Manzese
Utabiri sahihi wa kuibuka kwa Uislamu
Historia ya mgogoro wa Nzasa
DUMT watoa msaada kwa walioathirika
Nzasa
UCHOMAJI NYUMBA NZASA: Wafadhili
wana mchango gani?
Mafundisho ya Quran
|