AN-NUUR 
Na.171 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 16 - 22, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Chakula na lishe: 

Virutubisho vinavyopatikana katika vyakula 

Na Mujahid Mwinyimvua 

KAMA nilivyowahi kusema katika makala zilizopita, mwili wa binadamu (na viumbe vingine hai) ili uweze kukua na kunawili unahitaji vitu vinavyojulikana kama virutubisho au viinirishe. Kwa lugha ya kigeni virutubisho vinaitwa "Nutrients". Virutubisho hivyo vinapatikana katika vyakula mbalimbali. 

Vile vile tulijifunza katika makala za nyuma kuwa, virutubisho vyote hugawanywa katika makundi makuu sita, ambayo ni kabohaidreti (wanga, sukari na nyuzi nyuzi), protini, mafuta, vitamini, maji na madini (minerals). Ili mwili uweze kukua na kunawili vizuri lazima upate virutubisho vyote. 

Chakula (kama cha asubuhi, mchana, jioni au usiku) chenye virutubisho vyote sita hujulikana kama mlo kamili au "balanced deit" kwa lugha ya Waingereza. Kwa vile takribani vyakula vyote tunavipata kwa gharama kubwa (fedha au kazi), swala la uchaguzi wa vyakula haliepukiki. 

Pia unategemea mazoea ya mlaji, radha na sura ya chakula, virutubisho na mambo kadhaa wa kadhaa. 

Ili kufikia uchaguzi sahihi wa vyakula, elimu ya chakula gani kina virutubisho gani ni ya msingi. Makala ya wiki hii inakusudia kukidhi haja hiyo kwa wasomaji wetu. Katika kukidhi haja hiyo, vitataja aina ya chakula, virutubisho vya msingi na virutubisho vya ziada vinavyopatikana katika vyakula hivyo. 

Nafaka: 

Nafaka ni vyakula vya punje punje au chembechembe kama vile mtama, mahindi, ngano, uwele (mawele), mpunga n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula vya nafaka ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni Protini, vitamini (kundi la B) na baadhi ya madini. 

Vyakula jamii ya mizizi na matunda 

Vyakula jamii ya mizizi (starchy roots) ni kama vile viazi (vitamu, mviringo, n.k) mihogo, n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula jamii ya viazi na matunda ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi (dietary fibres). Zaidi ya virutubisho hivyo ni baadhi ya madini, vitamini C (kama chakula hicho siyo kikavu) na vitamini A (kama chakula hicho kinarangi ya njano). 

Vyakula jamii ya maharage 

Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k. Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na madini. 

  
Mbegu za mafuta 

Mbegu za mafuta ni kama vile alizeti, pamba, ufuta, nazi, mawese (chikichi), kweme, maboga, tikiti maji, matango, n.k. 

Virutubisho vinavyopatikana kwa wingi katika mbegu za mafuta ni mafuta, protini na nyuzi nyuzi. Ziada kundi B. (B- Vitamins). 

Nyama/Samaki 

Virutubisho vya msingi katika nyama au samaki ni protini, mafuta na madini ya chuma. Virutubisho vingine ni vitamini vya kundi B na madini (zaidi ya yale ya chuma). 

Ini 

Ini linatupa virutubisho vya msingi vya protini, madini ya chuma na vitamini. 

Maziwa 

Virutubisho tunavyovipata kwa wingi katika maziwa ni mafuta, protini, baadhi ya madini na vitamini. 

Mayai 

Mayai yana virutubisho vya msingi vya protini na vitamini. Zaidi ya hivyo ni mafuta na madini (siyo ya chuma). 

Mafuta 

Mafuta kama chakula yanatupa mafuta kama kirutubisho cha msingi. Zaidi ya hicho ni uwezekano wa kupata vitamini A. 

Mboga za majani 

Mboga za majani hasa zile za kijani zinavirutubisho vya msingi vya vitamini A, C na B, Zaidi ya hivyo ni protini, madini na nyuzi nyuzi. 

Matunda jamii ya machungwa 

Matunda jamii ya machungwa ni machungwa, machenza, n.k virutubisho vya msingi tunavyovipata kutoka katika matunda jamii ya machungwa ni sukari, vitamini A na C. Zaidi ya hivyo ni madini na nyuzi nyuzi. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

 TAHARIRI 
Serikali iwahurumie wananchi wake 

KUCHOMWA MOTO NYUMBA ZA WANANCHI: Nzasa wamtaka Mkapa awaonyeshe pa kwenda 
Na Mwandishi Wetu, Nzasa 

Mishikaki ya nguruwe Moshi yachomwa mbele ya Msikiti 
Na Mwandishi Wetu 

MAONI YETU: 
Je; ni halali kuchoma Kidungu cha mtu? 

Upimaji huu mpya ni wa nini 
Na Mwandishi Wetu 

TANGAZO LA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI 

Ndoa si lengo, ni wasila wa kufikia lengo 
Na Bi. Zuhura Tajiri, Shinyanga 
 
Teknologia:
Jifunze kuunganisha Kompyuta
Na Hassan Omar

Makala:
Nani atakayewahoji Waheshimiwa hawa

Goda Muslim School, Manzese
Na Mwandishi Wetu

Utabiri sahihi wa kuibuka kwa Uislamu
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

Historia ya mgogoro wa Nzasa
Na Mwandishi Wetu

DUMT watoa msaada kwa walioathirika Nzasa
Na Mwandishi Wetu

UCHOMAJI NYUMBA NZASA: Wafadhili wana mchango gani?
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kutoa pasipo masimango 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita