|
|
| Dondoo
za Saikolojia
Hoja kengeza Na Abu Halima Sa Changwa HOJA kengeza ni hoja ambayo haina mantiki, lakini mtu naikubali kwa sababu tu wengi wanaikubali, au imesemwa na mtu ambaye anadhaniwa hawezi kukosea. Mara nyingine anayeikubali hoja hiyo huona uwezekano wa kutokuwa na mantiki kwa hoja hiyo. Hebu angalia taswira iliyoambatanishwa hapa. Unaona paka na kofia kwa pembeni. Unaweza kumfanya paka huyo akaivaa hiyo kofia kwa kuiangalia taswira hiyo huku ukiwa umefanya makengeza. Ukifanya makengeza unaona paka wawili na kofia mbili. Unaweza kuipeleka kofia ya upande wa kulia hadi kichwani kwa paka wa kushoto. Paka anakuwa kavaa kofia. Hivi ndivyo ambavyo hoja kengeza inavyoonekana kama ya kweli japo si ya kweli. Mfano mzuri wa hoja kengeza ni ile hesabu ya ajabu isemayo 1 + 1 + 1 = 1 (badala ya 3). Mamilioni ya watu wanalifanya jawabu liwe moja, japo shuleni walifundishwa ni tatu, na kompyuta zote zitasema tatu. Lakini kwa vile wameamua kuangalia hesabu hiyo kimakengeza. Lakini kwa vile wameamua kuiangalia hesabu hiyo kimakengeza, watang’ang’ania tatu, ana ni kwa ajili watu wengi wanaamini hivyo, na ni kwa sababu hata Watakatifu wanasema hivyo. Cha kushangaza ni kwamba, wengine wanaoamini hesabu hii ni Maprofesa. Qur’an inasema: Sema: Yeye Mungu ni mmoja (112:1) Wala usiseme watatu. Juzuieni itakuwa
bora kwenu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mmoja tu, ni mbali na utakatifu
wake kuwa ana mwana. Ni vyake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.
Na Mwenyezi Mungu ni mlinzi wa kutosha.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao Maoni
Dondoo
za Saikolojia: Hoja kengeza
Makala ya mtangazaji
Makala
Tanzania
tuna sera gani kuhusu kanda
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Teknologia
Makala na habari
Mwinyimkuu
kufanya sensa ya waumini Magomeni
Wazazi
Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Tuwaige
Wangazija, 'tutafanikiwa'
Serikali
imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Muhadhara
waunguruma Geita
Fuateni
Sharia ya Allah - Sheikh
Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu Mafunzo
ya Qur'an
Chakula na lishe
|