|
|
|
2:6 Khalifa umar aliteua magavana kumi na tano kama ifuatavyo: Khalifa Uthman alibadilisha magavana wakati wa upinzani, lakini kwa kiwango kikubwa walibaki wale wale. Khalifa Ali alikusudia kufanya mabadiliko lakini katika kufanya hivyo ndio ikapelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe. Uteuzi wa viongozi ulizingatia sifa za viongozi ambazo kwa mujibu wa mfumo wa kisiasa wa Kiislamu ni kama zilivyokwisha elezwa ispokuwa wakati wa Ukhalifa wa Ali palikuwa machafuko ya wenyewe wenyewe. i). Khalifa alikuwa ndie mkuu wa majeshi. Aliamuru vita vipiganwe au visipiganwe, alisaini mikataba aliteuwa maamiri jeshi na kupeleka maelekezo katika uwanja wa mapigano Abubakar na Ali waliongozwa mapigano kama Mtume alivyofanya, lakini Khalifa Umar na Uthman hawakujaaliwa fursa hii lakini wamekufa mashahidi kwa kuuliwa na wapinzani. ii). Khalifa alikuwa ndie mwanasheria mkuu wa serikali. Alisikiliza kesi na kutoa hukumu na yeye ndie aliyekuwa mahakama ya rufaa. Mikoani waliteuliwa majaji walioendesha hukumu ya niaba yake. iii) Halikadhalika Khalifa alitumia mapato na matumizi ya serikali na mipango ya maendeleo ya Dola. 3. Marupurupu ya Khalifa Abubakar alipochaguliwa kuwa Khalifa aliendelea na kazi yake ya biashara alipokuwa anakwenda sokoni kuuza nguo alikutana na Umar na Abu Obaida ambao walimkataza. Ndipo shuura ikakaa na kuamua kuwa apewe kiwango maalum cha posho kutoka katika Baitul Mali kiasi cha kumuwezesha kuishi maisha ya kawaida. Zaidi ya kasma hii hakuruhusiwa kuchukua zaidi.31 Hata hivyo Khalifa Abubakar alirudisha kwenye Baitul Mali posho yote aliyopewa kutokana na maelekezo yake alipokuwa anafariki Dunia.32 Katika Ukhalifa wa Umar mishahara ilipangwa kwa wafanyakazi na viongozi wa serikali. Hivyo Khalifa Umar na Ali walichukua posho zao ila Uthman alitumia pesa zake kwa vile alikuwa na uwezo wa kiuchumi. 4. Hadhi ya Khalifa Khalifa ni muwakilishi wa Mtume na alifanya kazi zote alizofanya Mtume isipokuwa ya kuplea wahyi tazi ambayo ilikwisha sitishwa. Hivyo alihitajika na aliheshimika na kuthaminiwa sana katika jamii. Kazi ya kuongoza swala za kila siku, swala za Ijumaa Idi mbili Hija ziliongeza kuheshimika na kuthaminika kwa Khalifa. Kutajwa kwa Khalifa katika kuhutuba katika majimbo na anapokuwa hasomi khutuba yeye mwenyewe kwa sababu yeyote ile kumeongezea kuimarisha nafasi ya khalifa katika jamii. 5. Khalifa na utungaji sheria Khalifa kama ilivyokwisha onyeshwa sio mtungaji wa sheria kama ilivyo kwa marais wa leo na mabunge yao. Khalifa ni mtekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu. Halikadhalika ni msimamizi mkuu wa sheria za Mwenyezi Mungu. Katika kipindi cha Ukhalifa vyanzo vya sheria vilibakia Qur’an, sunna na ijma na baadae Umar Khalifa wa pili aliongeza Qiyas. Kwa hali hii ufalme katika Dola ya Kiislamu ulibaki kuwa ni wa Mwenyezi Mungu. Siku za mwanzo za ukhalifa kuliundwa tume ya sheria (Ofisi ya Mufti) ilipotokea haja tume hii iliitwa na kupitisha uamuzi. Tume ya sheria ya Khalifa ilifanya kazi kwa kutegemea vyanzo vya sheria vilivyotajwa katika masuala ya kawaida maamuzi ya tume yalikidhi haja. Lakini yalipotokea masuala yasiyo ya kawaida na yenye umuhimu wa kitaifa ilikaa majlis ya Answar, Muhajirin, wawakilishi wa Aus na Khazraj na kupitisha maamuzi; kwa mfano baada ya kutekwa kwa Iraq na Syria wapo maswahaba waliotaka ardhi igawiwe kwa askari waliopigana. Majlis iliyojumuisha ansar, Muhajirin na watu mashuhuri watano watano kutoka makabila ya Aus na Khazraj ilifanyika kuamua suala hili. Baada ya mjadala mrefu Khalifa Umar alifanikiwa kuwaelewesha wajumbe wa majlis kwa kunukuu aya nyingi kuthibitisha kuwa katika ardhi hata vizazi vijavyo vina hisa kwa hiyo ardhi isigawiwe kwa askari waliopigana lakini waachiwe wenyewe waliotekwa na kodi itakayotokana na ardhi hii wagawiwe askari katika mfumo wa kiinua mgongo cha kila mwaka.33 Hivyo ni dhahiri mkono wa Khalifa haukuwa juu ya sheria bali chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu, kwa namna hii haikuwezekana kupendelea kundi au mtu yeyote au kuipinda sheria kwa kumpendelea kundi au mtu fulani. Hivyo kulikuwa na usawa kamili mbele ya sheria, hali kadhalika katika masuala ya kodi kulikuwepo usawa na haki za kiraia. Hali hii ilipelekea mshikamano miongoni mwa waumini, uhuru wa maoni, haki katika jamii na kubwa kabisa ni kuwavumilia wafuasi wa Dini nyingine. 6. Khalifa na Mahakama Kabla ya kuangalia suala la mahakama katika Uislamu, tuanze na matazamo wa Uislamu juu ya Uhalifu, makao au hatia. Makosa katika Uislamu yapo katika mafungu matatu: (1) Makosa yanayomuhusu Mwenyezi Mungu kama vile uzinzi, ambao adhabu yake ni bakora mia moja, kumsingizia mtu kuzini, ambako adhabu yake viboko themanini, kuritadi adhabu yake ni kifo, kunywa vileo adhabu yake viboko themanini, wizi ambao adhabu yake ni kukatwa mkono na unyang’anyi au ujambazi ambao adhabu yake ni kukatwa mkono na miguu. Makosa haya yanajumuishwa katika istilahi moja kuwa ni al-Hadd. Khalifa hawezi kusamehe makosa haya. Kazi yake ni kutekeleza hadd (adhabu). Kwa wasio Waislamu makosa haya husameheka endapo atasilimu. (2) Makosa dhidi ya mwanadamu yanayohitaji fidia (al-qisas) mengi ya makosa haya kama kuuwa, kuumiza, kumtukana mtu n.k makosa haya yanaweza kumalizwa kwa makubaliano kwa mujibu wa sheria lakini Khalifa hana mamlaka ya kusamehe ila aliyekosea. Hali kadhalika makosa haya hayahesabiwi kuwa makosa dhidi ya serikali. (3) Yapo baadhi ya makosa kama, uasi (Rebellion), kula mali ya umma yamehesabika kama makosa dhidi ya serikali. Kwa kuizingatia haya, kazi za Khalifa kimahakama ni za aina tatu. Kwanza kuhakikisha kuna amani katika himaya yake, maendeleo kwa tabaka zote za watu na kuwalinda wanyonge mbele ya wenye kujiweza. Pili ni kutekeleza adhabu, kuratibu na kutekeleza haki za wanaodhulumiwa. Na tatu ni kuteua mahakimu wa kusimamia haki. Mahakimu hawa walikuwa watu wazima, waadilifu, waliobobea katika sheria ambao kazi zao ni pamoja na kuhukumu kesi, kusuluhisha magomvi, kurudisha amani za watu, utawala na ulipaji wa zaka, utekelezaji wa usia, utekelezaji wa adhabu, kusimamia mipango ya ndoa, mirathi, Talaka, na haki za wanyonge. Katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa wote, tangu wakati wa Ukhalifa wa Abubakar ilianzishwa ofisi ya mufti au taasisi ya mufti au tume ya uchambuzi wa sheria. Ofisi hii ambayo kwa Kiarabu iliitwa IFTA ndio pekee iliyoruhusiwa kutoa uchambuzi wa kina wa Fatwa za mamlaka mbali mbali. Hakuruhusiwa mtu mwingine kutoa uchambuzi wa sheria. Walioteuliwa wakati wa Abu bakar kushika wadhifa huu ni Umar, Ali, Uthman, Abulrahman bin Auf, Ali bin Kaab, Zaid bin Thabit na Abu Huraira - Mufti hawa walisaidia kuwafahamisha watu kuhusu sheria na kuwashauri bila malipo. Serikali ilifanya hivi ili kupunguza makosa kwani kwa kujua sheria watu walijizuia kufanya makosa. Itaendelea toleo lijalo
|
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|