|
|
|
Virusi vya HIV hupenya
Wananchi wengi wataendelea kuteketea kwa ukimwi kutokana na dhana potofu waliyo nayo kwamba kondomu ni jawabu katika kuzuia ukimwi. Taarifa ya Shirika la Viwango nchini (TBS) iliyotolewa hivi karibuni na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari imewaonya wananchi waepukane na dhana kwamba kondomu zitawanusuru kuambukikizwa ukimwi. Kwa mujibu wa Taarifa hiyo iliyonukuliwa na gazeti moja la kila wiki katika toleo lake la Alhamisi Novemba 19; ukimwi umekuwa ukikua kwa kasi kubwa sana hapa nchini ambapo zaidi ya Watanzania milioni moja unusu (milioni 1.5) wamesha ambukizwa virusi hivyo. Kasi hiyo ya kuongezeka kwa ukimwi imekuwa ikienda sambamba na ongezeko la matumizi ya "Salama" kondom na nyinginezo. Likinukuu taarifa ya T.B.S. gazeti hilo limesema kwamba, "ni rahisi kwa kirusi cha ukimwi kupenya katika kondomu kwa sababu katika darubini za kawaida kondomu zinaonyesha kuwa na matundu ambayo ni makubwa zaidi ya mara 50 ya ukubwa wa kirusi cha ukimwi ambacho hakiwezi kuonekana kwa darubini hiyo hiyo. Mfano wake ni kama mtegemea mchanga usipite kwenye "wiremesh" (waya wa kashata wa dirisha). Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba ukimwi nchini Uganda unapungua kwa wananchi kubadili tabia za uasherati wakati Tanzania kipaumbele kimekuwa katika matumizi ya kondomu. Toka kampeni za matumizi ya kondomu kama kinga ya ukimwi zilipoanza gazeti hili limekuwa likiwatahadharisha wananchi kwamba kondomu si kinga ya ukiwmi kwa sababu; kwanza virusi vya HIV ni vidogo sana kiasi kwamba vinaweza kupenya kwenye matundu ya kondomu. Pili, yaweza kupasuka na tatu kuvuja (spillage), Aidha, tumekuwa tukisisitiza kwamba upo utapeli unaofanyika katika biashara ya kondomu ambapo wananchi hupewa taarifa za uongo. Kwa tamaa ya kuzoa mapesa wafanya biashara wamekuwa wakiwahadaa watu kwamba waweza kumchezea mamba au simba mwenye njaa na wakawa salama ilimradi wana "Salama kondomu" mkononi. Dhana hii ilipotiliwa nguvu na viongozi wa Serikali pamoja na vyombo vya habari soko likazidi kukua. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano ambapo gazeti hili limekuwa likizungumzia hoja hizi na kuonekana wa 1947; ni roho ngapi zimeteketea kwa kufuata dhana potofu ya uzinzi salama. Nani atalipa gharama na fidia ya hasara iliyotokana na kampeni za awali? |
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|