|
|
| Kufuatia
kusailiwa makampuni husika:
Wananchi waingiwa
na hofu kuhusu silaha
Wananchi wengi wamelitafsiri zoezi hilo la usaili kama ni ruhusa ya kimya kimya inayotolewa na serikali ya uuzwaji wa silaha mitaani kama bidhaa ya kawaida. Baadhi ya wananchi walioongea na gazeti hili wamesema kuwa iwapo ni kweli serikali imedhamiria kuruhusu mpango huo basi amani ya nchi iliyodumu kwa muda mrefu itakuwa imechimbiwa kaburi. Wamesema jukumu la serikali hii ni kuondoa kero zinazowasumbua wananchi, lakini kama kero yenyewe iliyoonekana na serikali ni uhaba wa silaha za kuuana basi wangewaacha wananchi wakaendelea na kero hiyo. Aidha, wengine wameshangazwa na hatua hiyo ya serikali kwa kuhoji ni kwa vipi serikali ipuuze maoni ya wananchi wake walioichagua. "Kama serikali ni ya watu, ilichaguliwa na watu kwa ajili yao, vipi wenye serikali yao wapuuzwe na wachache walio madarakani kwa maslahi yao, amesema kwa uchungu mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Daudi mkazi wa Mwenge Jijini. Kwa mujibu wa gazeti moja litokalo kila siku la Alhamisi (jana) Desemba 10, mwaka huu, imeripotiwa kwamba maofisa wa jeshi la polisi tayari wameshakutana na makampuni yaliyotuma maombi ya kuagiza na kuuza silaha nchini. Aidha, gazeti hilo lilimkariri Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Ameir Mohammed kukiri kupokea mapendekezo kuhusu kampuni zilizopendekezwa kuendesha biashara hiyo. "Sasa serikali inatupeleka wapi kama sio kwenye kuuana", amedai mzee mmoja huku akiwa ameshika nakala ya gazeti hilo mbele ya ofisi ya gazeti hili Kariakoo jijini. Nchi yetu hivi sasa inakabiliwa na matatizo mengi ya kijamii kama vile kuota mizizi kwa rushwa, uchumi tegemezi, chuki za kidini, miundo mbinu mibovu; ukapa na matatizo mengine yanayotishia umoja wa kitaifa. Katika hali hiyo, wananchi wanaitarajia serikali yao kutafuta namna
ya kuyatatua matatizo hayo badala ya kujishughulisha na mambo ambayo hayana
maslahi yoyote kwao.
Serikali yagwaya kwa wafugaji nguruwe Na Muhibu Said IMEELEZWA kuwa serikali inaendelea kuwakodolea macho wafugaji na wauzaji wa nguruwe Jijini Dar es Salaam. Mazizi na mabucha ya nguruwe yamekuwa yakichipuka kama uyoga kila kukicha bila ya wahusika kuchukua hatua zozote kuzuia michupuko hiyo. Maeneo mbalimbali ya Jiji hivi sasa yamekumbwa na migogoro ambayo huenda yakazusha mapambano baina ya wananchi kutokana na kero ya nguruwe. Katika hali inayoonyesha kuzembea kwa wahuisika Ofisi ya Serikali za Mitaa Yombo Kisiwani, Jijini Dar es Salaam imeendelea kusita kumwamuru mkazi mmoja wa eneo hilo, Bw. Shayo kuondoa nguruwe wake anaowafuga eneo ambalo wakazi wake wengi ni Waislamu licha ya ofisi hiyo kupokea malalamiko ya kero zinazotokana na nguruwe hao. Uamuzi juu ya mgogoro baina ya mfugaji huyo wa nguruwe na waumini wa Masjid Tahiyyatu wa Yombo Kisiwani, awali ulipangwa kutolewa Jumatano ya Desemba 9, mwaka huu, kufuatia kikao cha kutatua mgogoro huo kilichofanyika Jumamosi ya Desemba 5, mwaka huu katika ofisi hiyo iliyopo mtaa wa Mamboleo ‘B’ Kata ya 14 - Temeke eneo la Yombo Kisiwani, Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, sababu ya msingi ya kutotolewa uamuzi huo mpaka sasa kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali bado haijafahamika. Lakini taarifa za juu juu zilizopatikana katika kikao kilichokaa kwa mara nyingine tena katika ofisi hiyo chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa wa eneo hilo, Bw. M.H. Futo, zimebaini kuwa uamuzi huo umepangwa kutolewa Jumamosi ya Desemba 12, mwaka huu. Aidha, wakati ofisi hiyo inasita kuchukua hatua hiyo, Mwenyekiti huyo wa serikali za mitaa eneo la Yombo Kisiwani, Bw. Futo alikieleza kikao hicho kuwa ofisi yake tayari imekwishapokea barua kutoka kwa mkuu wa wilaya inayopiga marufuku nguruwe kufugwa katikati ya mji. Katika kikao hicho pia, mfugaji huyo wa nguruwe Bw. Shayo pamoja na upinzani aliouonyesha , alihitimisha maelezo yake kwa kuwaomba radhi waumini wa Msikiti huo kwa kero wanayoipata na kuwaomba wampe muda wa mwaka mmoja aweze kuwahamisha nguruwe wake. Awali waumini wa Masjid Tahiyyatu waliilalamikia ofisi hiyo kuwa tangu Bw. Shayo awalete nguruwe wake eneo hilo wamekuwa wakikerwa na harufu ya wanyama hao. Pamoja na harufu hiyo, waumini hao pia walilalamika kuwa Bw. Shayo amekuwa akiachia kuzagaa ovyo kinyesi cha wanyama hao, hatua ambayo imekuwa ikiwaathiri wakazi wa eneo hilo. Mbali na kero hizo, waumini hao pia walidai kuwa wamekuwa wakipata taabu sana wakati wa kuswali kwa kuathiriwa na harufu ya wanyama hao hasa wa zizi kujengwa karibu na Msikiti wao. Mwandishi wa habari hizi ambaye amekuwa akihudhuria vikao hivyo, alifika eneo hilo na kushuhudia zizi hilo limejengwa nyumba ya tano kutoka Msikitini hapo. Aidha, kutokana na kuzagaa ovyo kwa kinyesi cha wanyama hao, maji ya kisima kilichopo katika bonde lililopo eneo hilo ambayo pia hutumika kwa kutawadhia Msikitini hapo yanahofiwa kuingiwa na najisi ya wanyama hao. Waumini hao walipinga ombi la Bw. Shayo la kuomba apewe muda wa mwaka mmoja kuwahamisha nguruwe wake kwa maelezo kwamba kwa kuwa nguruwe ni najisi na ni kero kwao, hivyo hawaoni mantiki ya kustahimili kero ya najisi hiyo japo kwa sekunde moja. "Ikiwa atapewa huo mwaka mmoja wa kusubiria kuhawahamisha nguruwe wake,
je wakizaana na hao watoto nao wasubiriwe tena kwa miaka mingapi?", alihoji
Imamu wa Msikiti huo.
|
YALIYOMO
Maoni Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani? Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha Serikali yagwaya kwa wafugaji
nguruwe
Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo:
Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Muhammad (s.a.w.) katika
Unabii wa Isaya (a.s.)
Ijue SUA Madrasa Moro
Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha Akina mama Muheza waungana kufanya
Daawa
Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata
uongozi
Je, hivi tuendelee kushika amri
za Mungu tena? - 2
Njia ya uzima ni nyembamba,
waionao ni wachache - 2
Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Sheikh Jongo aichachamalia
Uwawaru
Waamriwa kurejesha Mali ya
Mirathi
Waislamu Mlimba Moro mashakani
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|