AN-NUUR 
Na.179 Shaaban  1419, Desemba 11 - 17, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mafundisho ya Quran: 

Kutoa Sadaka kwa siri -3 

Al-Baqarah aya ya 272 

Kinachojitokeza katika aya hizi ni kuwa kwanza mtu mwenyewe hufanya uchaguzi wa ama wema au ubaya na ndipo Allah humuwafikisha katika uchaguzi wake huo. Katika aya ya kwanza mbali na Allah kutoa nafasi sawa kwa wanadamu wote ya kuongozwa kwa njia ya ilhamu kwa kueleweshwa mema na maovu, (Na naapa kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza; kisha akaifahamisha ouvu wake na wema kwake), wanadamu wote wamepata fursa ya kuletewa Mitume ambao wamekuja na vitabu ili kuwafahamisha uongofu pamoja na kuwakumbusha yale ambayo tayari wameshafahamishwa kwa njia ya ilhamu. 

Iwapo binadamu ameshafahamishwa wema na uovu na akaletewa Mtume akiwa na kitabu kumkumbusha hivyo huyu anaweza kusema kuwa amepotoshwa na Allah? au mtu huyu ana haki ya kusema kuwa Allah hakutaka kumuongoza? 

Aya ya pili inaelezea uongofu wa Allah na hamna anavyoongoka mtu. Kama ilivyo kwa aya iliyotangulia, Allah anamuwafikisha kuongoka yule ambaye ameletewa uongofu na akaupokea na kisha akaufuata. Na hii ndiyo maana ya kumuongoza yule "aliyeelekea kwake." Ama kwa upande wa nani awe Mtume na nani asiwe hilo Allah hulifanya mwenyewe hata kabla ya mtu anayehusika kuzaliwa. Mitume wote huzaliwa Mitume ingawaje wenyewe hawajifahamu hadi wanapodhihirishiwa na Allah wakati unapofika. Mitume wengi pamoja na kuwa na sifa tofauti na watu wa jamii zao walijifahamu kuwa wao ni Mitume walipotimia miaka 40 na kutangaziwa hivyo na Allah Mwenyewe au Malaika Jabril (a.s.) 

Kwa kuwa aya tunayoendelea nayo (272) imo katika mtiririko wa kutoa inakamilika kwa kuelezea mambo mawili ya msingi: 

-mtu anapotoa mali yake huwa ni kwa manufaa yake binafsi na siyo anapoteza bali atarudishiwa kwa malipo yaliyo bora zaidi kuliko hicho kidogo alichokitoa. 

- Mtu anapotoa anatakiwa afanye hivyo kwa lengo moja tu ambalo ni kumridhisha Allah Ambaye ndiye aliyetoa agizo hilo. Kutoa kwa matarajio mengine yasiyo ya kupata radhi za Allah kutampelekea mtoaji kuwemo hasarani. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Maoni
Waislamu tunakusudiwa kufanywa watumwa wa nani?

Wananchi waingiwa na hofu kuhusu silaha

Serikali yagwaya kwa wafugaji nguruwe 
Na Muhibu Said

Hakuna njama za kupindua Bakwata - Sheikh Yahya

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:: VOYEURISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Tathmini: Miaka 37 ya uhuru wa Tanganyika
Na Maalim Mwalimu

Adabu katika swala

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo: Batendi hakumuelewa Mkomidachi
Na Ally Said

Muhammad (s.a.w.) katika Unabii wa Isaya  (a.s.)
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa, Korogwe

Ijue SUA Madrasa Moro
Na Mussa Ally, Morogoro

Kiteto wakosa darsa kwa kupinga Ramli

Ustadh ayeyuka na saruji ya Msikiti mjini Arusha

Akina mama Muheza waungana kufanya Daawa
Na B. Mwakangwale

Wanafunzi Waislamu Mbeya wapata uongozi
Na B.  Mwakangwale

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 2
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzima ni nyembamba,  waionao ni wachache - 2
Na Yasin Valerian Massawe

Waandishi andikeni ukweli - Kamati
Na Mwandishi Wetu

Sheikh Jongo  aichachamalia Uwawaru
Na Badru Kimwaga

Waamriwa kurejesha Mali ya Mirathi
Na Njuki  A.

Waislamu Mlimba Moro mashakani
Na Q. Mataita

Sayansi na Teknolojia 
[Ielewe Modem yako] 
 
Mafundisho ya Quran

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Futari ya Tende] 
 
Tangazo
Vitabu na Mihutasari ya Maarifa ya Uislamu
 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita