|
|
UWAWARU
yafa Rufiji
Taarifa kutoka Rufiji zinaeleza kwamba kujitoa kwa Waislamu kulifuatia mkutano wa pamoja wa Waislamu wa Ikwiriri uliofanyika Msikitini mwanzoni mwa wiki hii. Awali, mkutano huo ilikuwa ifanyike siku ya Ijumaa Desemba 11, mwaka huu hata hivyo uliahirishwa kutokana na wahusika wakuu kutohudhuria. Kwa mujibu wa waliohudhuria kikao hicho, muumini mmoja ambaye alifahamika kuwa ni muhudumu wa Msikiti huo huku akititirikwa na machozi alimkabili Sheikh wa wilaya wa Bakwata Kassim Rwambo na kumwambia kwamba hali ya kukosa kujifahamu kwa baadhi ya waumini imesababishwa na yeye (Sheikh). "Yote haya Sheikh umeyataka wewe, tulikuasa usiingie katika mambo hayo ya UWAWARU leo hii Waislamu wa Rufiji tunaitwa makafiri", alisema kwa huzuni muumini huyo. Kusikia maneno hayo, Sheikh naye aliangua kilio ghafla hali iliyowashangaza wengi waliokuwepo Msikitini hapo. Imedaiwa kuwa Sheikh Rwambo ndiye aliyewashawishi Waislamu wa Rufiji kujiunga na UWAWARU kwa kutoa fatwa zinazohalalisha ushirikiano baina ya Waislamu na Wakristo. Hata hivyo, pamoja na fatwa hizo za Sheikh mfululizo wa vikao vya Waislamu ulikuwa ukiendelea wilayani humo kufuatia kuundwa kwa UWAWARU ambapo kikao kingine baada ya kile cha kwanza kilifanyika Jumatano wiki hii. Kikao hicho kiliwahusisha Maimamu wa Misikiti yote ya Ikwiriri na waumini wengine ambapo baada ya mjadala mrefu iliafikiwa kuwa umoja huo unakiuka mafundisho ya Uislamu. Baadhi ya waumini waliojiunga na UWAWARU walidai kudanganywa na Wakristo kuwa iwapo wangeafiki umoja huo wangejengewa hospitali. "Wakatuzunguka tukajisahau, kuanzia sasa tunauvunja umoja huo", alisema Shahara aliyekuwa msemaji mkuu wa viongozi wa UWAWARU upande wa Waislamu. Mwishoni mwa kikao hicho iliazimiwa Waislamu wajitoe UWAWARU na kuwatenga wale wote watakaojinasibisha na umoja huo. UWAWARU iliasisiwa na Wamisheni waliofika wilayani hapo kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbonde miezi miwili iliyopita. Malengo ya umoja huo kwa mujibu wa Mheshimiwa Bakari Mbonde ni kujenga mahusiano mema miongoni mwa wananchi wilayani Rufiji. |
YALIYOMO
Tahariri Umaskini unachafua mazingira! Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani Qur’an yachomwa moto Shinyanga Marekani yadhihirisha Ubeberu wake MARADHI
YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu Akheri ya
zamani
UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU Wasomi
Waislamu wawajibike
Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua MADRASATUL
Husseiniyi Shadhily
Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said Misikiti yakosa maji ya kutawadhia Bakwata Tanga haifuati katiba yake Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah Je,
hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Njia
ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 3
Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|