AN-NUUR 
Na.180 Shaaban 28 - Ramadhan 1419, Desemba 18 - 24, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani’ 

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumiwa kwa kuidhinisha ubabe na udhalimu wa Marekani dhidi ya mataifa mengine. 

Watu wengi waliotoa maoni yao kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq wamesema baraza hilo limeshindwa kuwa na msimamo pale Marekani inapokiuka sheria za kimataifa. 

Wamemlaumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan kwa kushindwa kutoa kauli ya baraza badala yake kuelezea hisia zake binafsi. 

Bwana Kofi Annan amenukuliwa na vyombo vya habari akielezea masikitiko yake juu ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq bila ya kueleza msimamo wa Baraza lake. 

"Hii ni siku ya huzuni kwa watu wa Iraq, ghuba na ulimwengu kwa ujumla, mimi nimejitahidi kwa kiasi kikubwa kuumaliza mgogoro huu kwa njia za amani", Katibu huyo alinukuliwa na kituo kimoja cha televisheni. 

Kauli hiyo ya Bwana Annan imetafsiriwa kuwa Umoja wa Mataifa (UN) haukuruhusu mashambulizi hayo ya Marekani dhidi ya Iraq. 

Kwa mujibu wa matangazo ya vituo mbalimbali vya televisheni, watu wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Iraq kufuatia mashambulizi hayo. 

Aidha majengo kadhaa pamoja na miundo mbinu imeharibiwa vibaya na makombora yapatao 200 yaliyorushwa na majeshi ya Marekani nchini humo. 

Mashambulizi ya Marekani yamefanyika katika mkesha wa mjadala wa maamuzi ya kashfa ya ngono inayomkabili Rais Bill Clinton. 

Mjadala huo ulikuwa uamue Bill Clinton avuliwe madaraka na kushitakiwa au aendelee na Urais wa nchi hiyo. 

Takriban asilimia 52 ya Wamareka hawaridhii kuongozwa na Rais anayesemekana kuliongopea taifa hilo katika kesi yake na Monica Lewinsky. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri
Umaskini unachafua mazingira!

Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume

UWAWARU yafa Rufiji

UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani

Qur’an yachomwa moto Shinyanga

Marekani yadhihirisha Ubeberu wake

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar

Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu

Akheri ya zamani
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC. USA

UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri

Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU

Kuanzishwa kwa UWAWARU

Wasomi Waislamu wawajibike
Na Mwandishi Wetu

Albucasis  936 - 1013 (CE)

Ijue Uhuru madrasa - Morogoro

Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua

MADRASATUL Husseiniyi Shadhily
Na Jamillah Nassoro
 
Hatimaye kesi ya kushambulia kituo nayo yafutwa

Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said

Misikiti yakosa maji ya kutawadhia

Bakwata Tanga haifuati katiba yake

Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 3
Na Yasin Valerian Massawe

Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani

Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga

Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza

200 wamesilimu

Sayansi na Teknolojia 
[Kuiweka Modem kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Mlo wa Daku] 
 
Tangazo 
New Book: The untold story of the Muslim struggle against British Colonialism in Tanganyika. 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita