|
|
|
Uchokozi wa Warumi Sehemu ya kaskazini ya Bara Arabu ilipakana na Dola ya Warumi wakati huo ilikuwa ikiitwa Dola ya Byzantine ambayo majimbo yaliyokuwa chini ya himaya yake ni Syria, Palestina na Misri. Jimbo la Syria ndilo hasa lililopakana na Bara Arab. Uchokozi wa wakristu wa Kirumi dhidi ya Dola ya Kiislamu ulianza tangu mwaka wa sita wa Dola ya Kiislamu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.). Uchokozi wa Warumi kama tulivyoueleza katika Sura hii maudhui ya kidato cha tatu; ulifanya mambo matatu. Waliwaua Wajumbe wote kumi na tano waliotembelea makabila na koo zilizokuwa zinakaa kaskazini mwa Syria, ila kiongozi wa msafara Kaaba bin Umair Ghifari aliyeweza kuwatoroka na kurudi Madina na kutoa taarifa hii ya kusikitisha kwa Mtume (s.a.w.). Jambo la pili vile vile ni la mauaji ya Harith bin Umair. Mauaji haya yalifanywa na Shurahbil bin Amr gavana wa Kikristu wa Busra. Mjumbe huyu, (Harith bin Umair) alitumwa kwake na Mtume (s.a.w.). Tukio la tatu ni kuuliwa kwa Farah bin Amral Juzami kamanda wa majeshi ya Kiarabu ya Warumi. Kamanda huyu alisilimu; Caesar aliposikia aliamuru akamatwe. Alipofikishwa kwake alimwambia Aritadi na abaki na kazi yake au abaki Muislamu na afe.61 kuliko kuwa kafiri Farah bin Amral Juzami alikhiari kifo. uchokozi huu ndio uliopelekea vita vya Mutah na msafara wa Tabuk ambao ulikuwa chini ya uongozi wa Mtume Mwenyewe. Katika msafara wa Tabuk adui hakujitokeza. Lakini baada ya msafara huu wa Mtume (s.a.w.) chokochoko zilianza tena kabla ya Mtume hajatawafu aliandaa jeshi ili likabiliane na hali ya mpakani, pamoja na kulipiza kisasi vita vya mutah chini ya uongozi wa Usamah bin Zaid. Jeshi hili lilipokuwa katika maandalizi Mtume akatawafu na safari iliahirishwa. Baada ya majuma matatu hivi tangu kuzikwa Mtume Khalifa Abubakr aliliamuru jeshi hili kukamilisha ujumbe wake. Hivyo likaenda na baada ya siku 40 Usamah alirudi na ushindi mkubwa. Baada ya ushindi Caesar hakuridhika hivyo aliendelea na chokochoko na hasa baada ya ushindi wa Waislamu uajemi, Caesar alistushwa zaidi na akaona vyema aikabili nguvu ya Uislamu. Hivyo aliyavamia majeshi ya mpakani ya Waislamu. Mwanzoni Waislamu walishinda lakini walipoingia Transjordan walishindwa. Kamanda na msaidizi wake waliuawa na wakaliacha jeshi chini ya uongozi wa Ikrimah bin Abu Jahl .62 Habari zilipomfikia Khalifa akaita shura yake na wakakubaliana kutangaza Jihad dhidi ya Dola ya Kikristu ya Warumi .63 Khalifa aliwahamasisha Waislamu kwa kuwaandikia barua. Moja ya barua hizo ni kama ifuatayo: Kutoka kwa Khalifa wa Mtume (s.a.w.) kwenda kwa Waislamu wote wanawake na wanaume wa Yemen. Nawasalimia wote wanaosomewa barua hii. Namshukuru Mwenyezi Mungu anapaswa kuabudiwa. Mwenyezi Mungu ameifaradhisha Jihad na kuwaamuru waitekeleze wakiwa katika hali nzuri au hali ngumu, wanatakiwa wajitokeze kwenda katika jihad kwa mali zao na nafsi zao. jihad ni wajibu na malipo yake ni makubwa. Nawasihi Waislamu mjitokeze kwenda kwenye Jihad dhidi ya Warumi wa Syria. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu; shirikini katika Jihad kwa Ikhilaswi. Hamtakosa moja ya zawadi hizi, ama kufa shahidi au ushindi na ngawira..64 Waislamu walihamasika na kujitokeza kwa wingi. Jeshi la kutoka Madina lilikuwa na Waislamu kati ya ishirini na saba elfu 7 na thelathini elfu 8 Jeshi hili kama mbinu ya kivita ligawanywa katika bataliani nne na kila bataliani ikawa chini ya kamanda mzoefu na kila kamanda alielekea upande wake. Kutoka Madina Abu Ubaidah bin al-Jarrah alikwenda hems. Amr bin al-As alikwenda Palestine, Yazid bin Sufian alikwenda Damascus na Shurahbel bin Hasnah alikwenda Jordan.65 Makamanda hawa walipigana katika maeneo waliyokwenda kila mtu peke yake. Lakini adui aliyekuwa na jeshi lenye zana zote za lazima kwa vita kwa wakati ule lenye askari laki mbili na nusu aliamua kupiga bataliani moja hadi nyingine akianzia Bataliani ya Amri bin Al-As ambayo ilikuwa imezingirwa Khalifa Abubakr alipofahamu mpango huu, aliamuru bataliani zote ziungane na kupigana pamoja. Vile vile alimuagiza Khalid kutoka Uajemi upesi aende Syria kwenye uwanja wa vita. Khalid kama tulivyokwisha muelezea ni Jemadari hodari. Katika muda wa
siku kumi na tano tangu atoke Syria alishinda ngome za Warumi zilizokuwa
Suwa na Tadmur. Kabla habari hazijaenea za kuwepo kwake Syria tayari alikuwa
Damascus. Mwanzoni Warumi waliwatumia wasaidizi wao wa Kiarabu kabila la
Ghassan ambalo lilishindwa vibaya na Khalid katika mapigano yaliyofanyika
Marja Rahit maili 15 kutoka Damacus. Wakati Warumi wanarudi kuilinda Damascus
na kutafuta Khalid upande wa kaskazini, Khalid alibadili njia akapitia
Quraqir na kwa kustukizia akaiteka Busra na kuungana na makamanda wenzie
Palastine ambako majeshi ya Amr al-As yalizingirwa. Jeshi kubwa la adui
lilidhamiria kuwafukuza Waislamu katika nchi yao; lakini makafiri kamwe
hawatamshinda Mwenyezi Mungu hata wakiwa wengi kiasi gani. Kahalid akiongoza
bataliani zote aliwashinda Warumi katika vita vya Ajnadayn Julai na Agosti
634 Jamadil-Awal 12 A.H. na Januari 635 katika vita vya Fahl. Taarifa ya
ushindi wa vita vya Ajnaday ilimkuta Khalifa Abubakr katika kitanda cha
mauti, alishikwa na homa na katika muda wa majuma mawili akafariki tarehe
23 Augosti 634 A.D. sawa na 22 Jamadal-Akhira 13 A.H. akiwa na umri wa
miaka 61. 66
|
YALIYOMO
Tahariri
Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani Qur’an yachomwa moto Shinyanga Marekani yadhihirisha Ubeberu wake MARADHI
YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu Akheri ya
zamani
UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU Wasomi
Waislamu wawajibike
Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua MADRASATUL
Husseiniyi Shadhily
Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said Misikiti yakosa maji ya kutawadhia Bakwata Tanga haifuati katiba yake Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah Je,
hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Njia
ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 3
Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|