AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

MADRASATI Riyaadhwa ni madrasa ya mchanganyiko ambayo ipo njia panda ya Chamwino na Area C; muasisi wa madrasa hii pamoja na Msikiti wake ni mhisani Bwana Khalipha Abdallah (Hongera). 

Madrasati Riyaadhwa ilianzishwa Novemba 20, 1994 ikiwa na wanafunzi 6 wakiwa ni watoto wa muasisi Bwana Khalifa Abdallah (Hongera) hadi sasa madara hii ina wanafunzi 205; wavulana 155 na wasichana 50. 

Madrasa ina mwalimu mmoja ambaye ni Alhaj Juma Athumani akisaidiana na wanafunzi waliofikia kiwango cha juu cha elimu. 

Aidha, yupo Ustadh Sharif Ahmad ambaye huja kila mwezi kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya ufundishaji wa fani za juu. 

Masomo yafundishwayo katika madrasa hii ni Qur’an na tafsiri yake; swarfa, Hadith, Fiqh, Tawhiid, Tasaufi, Balagha, Tarekhe na Mantiqi. 

Malengo ya madrasa hii kwa sasa na ya baadaye ni kutoa mafunzo ya Kiislamu, uendeshaji wa Ibada, kujenga na kuanzisha bweni, kuanzisha shule ya seminari, maktaba, zahanati na kitengo cha ufundi chereheni (ushonaji) na useremala. 

Pia uanzishwaji wa matawi mawili ambayo ni Mar-wa likiwa Dodoma mjini na Sakami (Riyaadhwa B) likiendeshwa na walimu watatu. 

 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita