AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

UKARABATI wa barabara mjini Tabora unaofanywa na kampuni moja kutoka China umelalamikiwa kuwa hauzingatii wakati na taratibu za mipango miji. 

Akizungumza na gazeti hili wiki hii, mwenyeji mmoja wa mjini Tabora aliulaumu ukarabati huo kwa kusema kuwa umepitwa na wakati. 

"Nauliza swali, hivi vipande vya barabara vinavyotengenezwa Tabora tumeiga nchi gani yenye barabara kama palio la ng’ombe", alihoji mwananchi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Msigara Khalfani. 

Bwana Msigara ameshangazwa na jinsi barabara hizo zinavyokarabatiwa chini ya mwembe na migazi bila ya kuwepo kwa mpango maalum. 

Mzalendo huyo ametoa ushauri kuwa hakuna haja ya kuleta watalaamu kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ambao utendaji wao hautofautiani na wataalamu wa hapa nchini. 

Aidha, amewaomba wahusika wa mipango miji, mjini Tabora wauweke mji huo katika mandhari ya kupendeza kama ilivyo katika miji mingi hapa nchini. 

Tabora ni moja ya miji mikongwe hapa nchini ambapo historia yake inajitokeza zaidi katika harakati za kudai uhuru wa nchi hii miaka ya 1940 hadi 1961. 

Mji huo hadi hivi una kiwanda kimoja tu ambacho huenda kikafa wakati wowote kutokana na uzalishaji wake duni. 

Hali ya maisha ya wakazi mjini ni ya chini sana, vijana wengi wameukimbia mji huo na kwenda mikoa ya kanda ya ziwa na pwani. 

Barabara ya Mwanza ambayo ilikuwa maarufu enzi hizo hivi sasa imechakaa mno kiasi cha kupoteza umaarufu huo. 

Nyumba za matope ndizo zilizo nyingi katikati ya mji huo na pembezoni mwake. 

Wito umetolewa kwa wenyeji wa mkoa huo kutafakari sababu zilizopelekea mkoa huo kusonga nyuma miaka 37 sasa na hatua za kuchukua ili kurekebisha hali hiyo kwa kuzingatia uchaguzi ujao. 

 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita