AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Jicho la Uzalendo

Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 

Na Sompo wa Kahambwe 

MIGOGORO mingi hasa ya kisiasa inayojitokeza katika jamii, mara nyingi vyanzo vyake ni tabia ya utumiaji mbaya wa nyadhifa, sera potofu, upuuziaji wa masuala muhimu, kulindana na kupendeleana. 

Tukiangalia sehemu mbalimbali zenye migogoro duniani ambayo imelipua mapambano ya wenyewe kwa wenyewe, tunaona kwamba zilianza chokochoko za kidogo kidogo, wengi kulalamika kutotendewa haki, wachache kushutumu ukandamizaji wanaofanyiwa au utendaji mzima wa serikali inayo watawala kuwa mbovu. 

Lebanon, Bosnia, Kosovo, Kongo, Rwanda, Burundi n.k. ni matokeo ya fukuto za muda mrefu; kurushiana maneno, vijembe, kejeli na kutambiana. Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio ya vita, mauaji na vifo vya maelifu ya watu wasio na hatia kutokana na migogoro katika sehemu hizo. Ufumbuzi huchukua muda mrefu inapofikia hatua ya mapambano ya silaha. 

Nchi yetu hivi sasa inapita katika mkondo wenye mawimbi ya migogoro mikubwa inayotishia usalama wa wananchi na raia wake. 

Ipo mikwaruzano ya kidini baina ya Waislamu na Wakristo na baina ya Waislamu na serikali. Upo mtafaruku wa kisiasa unaotokana na chama fulani kuendelea kung’ang’ania kuongoza bila kujali maoni na maamuzi ya wengi. 

Yapo pia madai ya utendaji usioridhisha wa viongozi wa serikali iliyo madarakani. Aidha uoni wa mambo huelezwa kuwatia wasiwasi wanaoongozwa. 

Na vilevile wapo waliokata tamaa kabisa ya kuishi chini ya mfumo huu wa utawala usiojua haki, uadilifu, maadili, haramu wala halali. 

Hizi ni fukuto zilizopo nchini hivi sasa ambazo huenda zikailipua nchi siku za usoni. Bahati nzuri sana wazalendo wengi wameanza kuliona hili mapema. 

Utafiti unaonyesha kwamba kada mbalimbali za wananchi zimekuwa zikijadili hatima ya nchi kadri serikali inavyoendelea kuparamia visiki, miti, magogo, mabonde na maporomoko. 

Wengi wana mawazo kwamba Tanzania chini ya serikali ya CCM itaendelea kujichimbia kaburi. Hoja kuu hapa ni kule kushindwa kwake kutatua migogoro kwa taratibu za muafaka, badala yake kuififisha kinamna. Ubabe, dharau na upuuzaji vimeshika hatamu za maamuzi. 

"Kutokujali yanayowakera wananchi ni maandalizi ya mabwawa ya damu za wahanga wa miongo ijayo", anasema mtaalamu mmoja wa mambo ya siasa. 

Watu wanaposema hili si zuri, lile linakwaza jitihada zetu au linapindukia taratibu zilizowekwa, hapana budi wasikilizwe, kukutana nao na kutafutia ufumbuzi kero yao badala ya kuendesha propaganda na vitisho. 

Inawezekana tukaendelea kujidanganya kwa mbinu hiyo lakini pia inawezekana tukaja hukumiwa na historia kwa uzezeta huo! 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita