|
|
|
Ndugu Mhariri WAKATI Waislamu wa Tanzania wakisherehekea uzawa wa Mtume Muhammad (s.a.w.) mwezi Julai, 1998 aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo iliyofanyika kitaifa mjini Bagamoyo alisema Waislamu wa Tanzania ni watu ambao hawana dira, wasio na malengo ya muda mrefu, wenye uadui miongoni mwao, wasio na upendo wala kuhurumiana na wasiofanya lolote la maendeleo yao ila kazi yao ni kulalamika tu na kusingizia serikali kwamba inawapiga vita, wakati inatoa haki sawa kwa wote. Na pia akawataka Waislamu waige mfano wa aliowalita ndugu zao Wakristo, kwani wao wanaishi kwa upendo na kuhurumiana tofauti na Waislamu. Tokea wakati ule mpaka leo nimekuwa nikifuatilia na kuutafuta huo upendo wa Wakristo ili upate kuuiga. Katika jitihada za kutafuta upendo huo kwa bahati mbaya sikuuona bali nimefanikiwa kuona chuki tena zilizokubwa kabisa kati ya Wakristo na Wakristo. Kwa zaidi ya miaka 30 sasa Wakristo wa madhehebu mawili (Anglinana na Roman) wamekuwa wakichinjana wao kwa wao huko Ireland na jitihada kubwa zimefanywa kuuondoa mgogoro huo bila kufanikiwa. Hii inadhihirisha wazi kuwa watu hao hawana upendo na kuhurumiana. Je huu ndio upendo tunaotakiwa kuiga Waislamu toka kwa Wakristo. Pia Wakristo wao kwa wao wamepigana na hata kuuawana Arumeru, Arusha kwa sababu zisizo za msingi, lakini huu ndio upendo tunaotakiwa tuige Waislamu wa Tanzania. Vile vile gazeti la Wakristo wenyewe pia linatuthibitishia wazi kukosekana kwa upendo baina ya Wakristo, katika gazeti moja la dini ya Kikristo linatoka wiki mara moja, katika toleo lake la Jumapili Desemba 20-26, 1998 katika ukurasa wake wa mbele ilitolewa taarifa iliyopewa kichwa cha habari "Walutheri Mwanga wafanya ibada chini ya ulinzi wa polisi". Hii imetokana na mgogoro wa KKKT Dayosisi ya Pare na Mwanga. Kwa mujibu wa taarifa hiyo mgogoro huo ulianza muda mrefu na umeshindikana kupatiwa ufumbuzi hata baada ya kikao cha usuluhishi. Tunamuuliza Profesa, je watu wenye upendo, wanaweza kuishi na kuwa na migogoro inayopelekea kufikia hatua ya ibada kusimamiwa na polisi. Je, upendo ni kuamrisha majeshi yamiminie nchi nyingine mizinga na makombora bila kujali maangamizi ya roho za watu na uhai? Clinton Mkristo kafanya hayo kisha anachukua Biblia ana kwenda Kanisani. Ukweli ni kuwa hakuna watu wenye upendo kama Waislamu, na ndio maana tatizo la Muislamu mmoja ni tatizo la Muislamu yeyote yule. Anapopata tabu Muislamu mmoja ni tabu ya Waislamu wote. Hatuwezi kupata mwongozo kwa asiye na mwongozo. Na F.M. Abdulrahmani,
Kweli wapo waliosoma hawakujua Ndugu Mhariri NIMESIKITISHWA na kauli ya Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana Bw. Paul Kimiti alipokuwa anakabidhi bendera kwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia. Bw. Waziri anaposema yeye amesoma na ametembea sana, anatushangaza sana ndio mana tunajiuliza kama kweli amesoma, je amejua? Kwa sababu kusoma sio kujua, kwani kuna waliosoma lakini hawakujua. Huenda yeye ni miongoni mwa hao. Wengine wamesoma hadi darasa la saba na wengine la 12 lakini hawajui kusoma wala kuandika majina yao. Iweje afurahie kumwona mwanamke yuko uchi? Ndio maana tunapata wasiwasi waziri anaposema hiyo ni hali ya kawaida na kuwaambia wale wasiopenda hali hiyo kuwa sio wasomi. Hivi usomi ni kukaa uchi? Je ndio kwenda na wakati huko? Mimi naona huko si kwenda na wakati bali ni kupitwa na wakati. Omari Mohamed
Kongamano Newala laleta mafanikio Ndugu Mhariri KWA mara nyingine tena naomba unipokee gazetini kwako, ili niweze kupongeza uongozi wa Umoja wa Wanawake wa Kiislamu nchini kwa jitihada zao za dhati ambzo wamezionyesha baada ya kuandaa kongamano hapo Newala, na hatimaye kushiriki wenyewe pamoja na usumbufu waloupata Mola atawalipa Insha-Allah. Kutokana na mafunzo ambayo yaliyotolewa na wahadhiri kutoka Dar es Salaam, Dodoma, Lindi na Masasi katika kongamano hilo, pale Novemba 10, 1998 washiriki wa kongamano hilo wasiopungua 2000 walinufaika na mafundisho yote ambayo yaliandaliwa kwa makusudi maalumu ya kumpandikiza mwanamke katika imani ya dini kamili. Ukweli ni kwamba ukikutana na baadhi ya wanawake mjini hapa, wanaonyesha kiwango kikubwa cha kumuamini Mola wao kikamilifu siyo kwa Riya. Vile vile kongamano liishe wamekuwa wakihangaika madukani kutafuta vitambaa bora na nadhifu rasmi kwa hijab, kiasi ambacho kimepelekea bidhaa hiyo kuwa adimu hapa mjini na vitongoji vyake. Nawaomba wafanyabiashara waelekeze macho yao kusini kwa kutupelekea vitambaa hivyo, ili wanawake watekeleze amri ya Mwenyezi Mungu aliyoitoa katika Qur’an sura ya Al-Hazaab aya ya 59 kuwa: Ewe Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako na wake wa waaminio, wateremshe ju yao shungi zao, hivyo inaelekea zaidi wajulikane na wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni msamehevu mrehemevu. Mola awe radhi nayi. Amiina Muhammed Hakika Machellah,
Tuchukue tahadhari Ndugu Mhariri HUU ni ukiwa mwezi mtukufu (Ramadhani) imejitokeza hali isiyo nzuri Misikiti hasa wkati wa "futuru" wafungaji wananunua "juice" na vitu vingine vya kufungulia bila tahadhari. Mbali na hilo kuna vijana hao wanauza "juice" ni wachafu na yaelekea wengine si miongoni mwa Waislamu. Hivyo, naomba Maimamu Misikitini wawajue hao wauzaji wa "juice" na kuwepo idadi maalum ya wauzaji hao. Tutalazilaumu nafsi zetu tusipochukua tahadhari. Ndugu Mhariri NAOMBA nitoe maoni yangu katika gazeti lako lenye kupenda na kutetea haki na kufichua dhuluma na maovu. Katika wilaya ya Masasi kuna wafuasi wa madhehebu ya dini, na dini mbalimbali. Na mara zote wamekuwa wakifanya shughuli zao na mahubiri mbalimbali tena hupita kutangazwa kwa kipaza sauti mji mzima. Lakini inapotokea kwamba Waislamu wanataka kufanya mahubiri ambayo pengine hutokea mara moja kwa miaka kadhaa, basi huwekewa vikwazo vingi, pamoja na kucheleweshewa au kunyimwa kabisa kibali. Tumewahi kushuhudia wanafunga virango na kuondoka bila ya kuzungumza lolote baada ya kunyimwa kibali. Na leo hii tunashuhudia mamia ya watu wakiondoka katika eneo maalum lililoandaliwa kutoka hapa mjini na vijiji mbalimbali vya wilaya hii bila kupata (kusikiliza) mahubiri hayo ambayo yangetolewa na msafara wa Sheikh Said John. Madai yaliyotolewa ati mkuu wa wilaya hayupo ameenda mkoani - Mtwara na ameagiza kibali kisitolewe hadi atakaporudi. Sasa je hawa Waislamu wote hawaaminiki wamekuwa wahuni? Akiwemo Sheikh wa Bakwata wa mkoa, au yeye amelidharau neno la Mungu au yeye amekuwa bora kuliko Mungu hata kuzuia ujumbe wa Mungu usifikishwe hadi atakapo yeye? Kwa hakika hii ni dharau ya kuidharau dini ya Kiisamu na ni ubaguzi dhahiri unaofanywa na viongozi waliochukuwa dhamana ya kuwatumikia wananchi wote kwa usawa chini ya katiba ya nchi. Masoud A. Omar,
Sumaye rudisha pesa hiyo Ndugu Mhariri NIMESIKITISHWA sana na hatua ya Mheshimiwa Waziri Mkuu Bw. Frederick Sumaye kukopa kitita cha pesa kutoka mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi wa vima vya chini. Nimesikitishwa kwasababu Bw. Sumaye kutokana na ngazi yake hahusiki kabisa na mfuko huo. Na zaidi kiasi cha mkopo ni kikubwa mno kuweza kurejesha. Nina wasiwasi; pesa hii ndio basi mwenzetu kajichukulia chake mapema? Kinachouma zaidi ni kwamba wafanyakazi wenyewe ambao ndio wenye mfuko huo, hawajaweza kukopeshwa si tu mkopo unaofanana na huo bali hata kiasi kidogo tu cha kuweza kukimu maisha yao ya uzeeni. Hata kupata pesa zao tu walizokatwa pia huwa ni kwa mbinde na masumbufu ya muda mrefu. Bw. Sumaye ameorodhesha msururu wa mali aliyonayo kabla ya kutaja mkopo aliopata. Mimi nasema hivi mali aliyotutajia ilitosha kabisa kuendesha maisha yake mbali ya marupurupu anayopata na atakayopata baada ya kuondoka kwenye "uhondo" alionao. Vipi Bw. Sumaye ameshindwa kuwaonea huruma wafanyakazi walio chini yake ambao maisha yao ni ya kubahatisha. Bw. Sumaye rudisha pesa hiyo ya wafanyakazi. Abdul Rauf Kimaro,
|
YALIYOMO
Tahariri Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa Id el Fitr Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM Barabara za Tabora zimepitwa na wakati Jicho la
Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya!
Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani Taarifa ya Kamati juu ya yaliyotokea Mwembechai Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika Kuongezeka kwa ajali za barabarani Njia ya
uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 4
Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao Kesi nyingine Mwembechai yaahirishwa Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|