AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mashairi
 

Ni cheche za Qur'an 

Zaujati nipe peni, nizikutubu khabari, 
Nanitowe shukrani, kwa Mola mtowa kheri, 
Mola mjaze imani, huyu wetu Muhariri, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Ni cheche za Qur'an, gazeti la AN'NUURI, 
Ni nuru ya duniani, kwa wenye kutafakari, 
Na tumuombe Manani, tupate redio Kheri, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Redio ni tumaini dini, ipate shamiri, 
Tuchambue Qur'an, kwa watu kuwa dhahiri, 
Uchambuzi wa kifani, wachukizwe makafiri, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Haya kama ni maoni, aidhani ushauri, 
Baada ya shukrani, twasisitiza khabari, 
Mihadhara mitaani, zitoshelezi khuburi, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Nuru hii ikhuwaini, si kwamba ya makafiri, 
Watekeleza dini, waziachao khiari, 
Amri wazi amini, siwafanyao kiburi, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Haya yote ya Manani, kwa wenye kutafakari, 
Sio kwao wapagani, watu wasio na dini, 
Ndani muwe na madini, tena chimbuko la siri, 
Gazeti la AN'NUUR, cheche za Qur'an. 

Rudi towe shukrani, kwa fitina kukabiri, 
Kazi yahitaji fani, hadi kitu kushamiri, 
Mijini na vijijini, kila wiki twakariri, 
Gazeti la AN'NUUR, cheche za Qur'an. 

Ninaacha hapa peni, niwahi lasiri, 
Swala zetu za jioni, walo shindwa Mapadiri, 
Naliombea amani, gazeti na Muhariri, 
Gazeti la AN'NUUR, ni cheche za Qur'an. 

Shamte 'A' Mpita (Kijukuu cha malenga), 
c/o Lamba Lamba, 
S.L.P. 66563,  AR ES SALAAM. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita