|
|
|
Upinzani wakati wa Khalifa wa pili ni maendelezoya upinzani ulioanza tangu wakati wa Mtume, na Khalifa wa kwanza. upinzani huu ulitoka kwa Waajemi na Warumi. umar alishika mamlaka ya kuendesha Dola ya Kiislamu mwezi 22 Jamadi-uth-Thani 13 A.H. sawa na tarehe 23 Agosti, 634 A.C. alipofariki Khalifa wa kwanza. Katika upinzani alioukabili tuanze na upinzani wa Wapeshia. Upinzani kutoka kwa Warumi Katika ukhalifa wa Abubakr sehemu ya himaya ya Waajemi iliyotwa Hira (Kingdom of Hira) ilitekwa na Khalid bin Walid Simba wa Mananni) na kuwa ni sehemu ya Himaya ya Kiislamu. Khalid alipopewa maagizo ya kwenda Syria kwenye bustani ya vita alimteua Muthana bin Harith kuwa kamanda wa jeshi la Waislamu Hira. Kutekwa kwa hira hakukuwapendeza Waajemi hivyo, Wapesia walitumia nafasi ya kutokuwepo Khalid na kutuma jeshi kubwa chini ya uongozi wa jemedari hodari na maarufu wa Wapeshia na mkuu wa majeshi ya Wapeshia kamanda - Rustam. Katika mapigano ya awali Muthana alizidiwa hivyo akaomba msaada kutoka kwa Khalifa Umar na jeshi kubwa likatumwa chini ya ukamanda wa Abu Ubayda. Vita vya Namaraq Mapigano makali yalitokea Namarraq baina ya majeshi ya Persia na ya Kiislamu na katika vita hivyo vya Namarraq Wapersia walishindwa na Hira kurudishwa tena katika mikono ya Waislamu. Kushindwa kwa Waajemi kuliwaongezea chuki hivyo wakakutana tena na Waislamu mahali palipoitwa JASDR kwa mara nyingine, katika vita hivi navyo wapeshia walishindwa. Vita vya Daraja Vita vilivyofuatia ni vita vya Daraja. Vita hivi vilipiganwa kwenye ukingo wa mto Eurphrates. Upande wa Adui uliongozwa na kamanda Bahman askari hodari na maarufu wa kipeshia. Katika vita hivi Waislamu walishindwa. Abu Ubaid aliuawa Muthna alishika mahali pake lakini tembo wa jeshi la Waajemi lilisababisha maafa makubwa kwa upande wa Waislamu. Kati ya askari elfu tisa wa Kiislamu walibakia elfu tatu tu.67 Khalifa Umar alistushwa sana na kushindwa kwa Waislamu hivyo alitangaza Jihad dhidi ya Wapeshia. Aliandaa jeshi la askari wa Mwenyezi Mungu 20,000 na Wapeshia nao waliandaa jeshi la Askari laki mbili hivi. Mahali paitwapo Buwaib ndipo palipopiganwa vita hivi hivyo, vita vyenyewe hujulikana kama vita vya Buwaib. Katika vita hivi wapeshia walishindwa. Wapeshia waliongozwa na Mehran Hamdani na jeshi la Waislamu liliongozwa na Muthanna. Kwa ushindi huu sehemu ya Magharibi ya Dola ya Persia ilikuwa chini ya dola ya Kiislamu. Idadi ya waliokufa upande wa adui katika vita hivi sio pungufu ya laki moja 68 na Waislamu wachache. Kushindwa kwa Wairani katika vita hivi kuliwastua na kulazimika kubadili kiongozi wa nchi. Kiongozi wa himaya alikuwa mwanamke (Malkia) walihisi kuwa jambo kama hilo lilichangia, hivyo alitawazwa ufalme mtoto wa miaka ishirini na moja Yezdgird. Mfalme aliratibu upya majeshi yake na kuongoza ulinzi katika mipaka yake. Kuimarisha ulinzi ulijenga kujiamini miongoni mwa wapeshia na kupelekea kuzuka kwa uasi usiokadirika katika maeneo yaliyokuwa yametekwa. Khalifa Umar alipopata habari za uasi kwa mara nyingine alitangaza Jihad dhidi ya wapeshia. Wapiganaji wa Mwenyezi Mungu wapatao elfu ishirini waliongozwa na Saad bin Abi Waqqas walielekezwa wapige kambi mahali paitwapo Qudisiya. Pia waliekezwa kabla ya mapigano watafute uwezekano wa suluhu ya amani. Hivyo Waislamu walimtumia ujumbe mfalme wa Wapeshia chini ya uongozi wa Asim. Asim alimwambia mfalme kuwa: "Enyi Wapeshia tunakualikeni kwenye njia ya maisha ya Amani (Uislamu). Mkisilimu ni ndugu zetu, tutakuachieni, Qur’an Neno la Mwenyezi Mungu ili mfuate amri Zake. Kama hamkubali tulipeni Jizya. (Kodi ya ulinzi) Na mkikaa njia mbili hizi, ya tatu ni upanga ili tufungue njia ya kueneza ujumbe huu.69 Yezdgird aliposikia hivi aliwatukana wajumbe wale, na kumtwika kiongoizi wa msafara Asim ndoo ya mchanga nae akaipelekea hadi kwa Saad ambae alitafsiri kwa ule mchanga na ishara ya ushindi. Kunyanyaswa kwa Waislamu kuliharakisha vita. Ushindi wa Qadisiya Mfalme Yezdgird alituma jeshi la watu laki moja chini ya uongozi wa Amir jeshi mkuu mwenyewe Rustam akisaidiwa na makamanda wengine maarufu wakiwemo Julinus, Mahran bin Bahram Razi na harmuzan.70 Jeshi hili la adui lilichukua siku sita kufika Qadisiya kutoka Mada’in mji mkuu wa Dola ya Warumi. Walipofika Rustam alianzisha mazungumzo na Waislamu - hivyo alitaka wawakilishi wa Waislamu wazungumze nae. Siku ya kwanza alikwenda Rabi bin Amir na kutoa masharti yale yale matatu aliyopewa mfalme wao - hapakuwa na maafikiano. Siku ya pili Rustam alitaka mazungumzo tena. Safari hii alitumwa Hudhaifah, nae halikadhalika alisisitiza masharti yale yale matatu. Siku ya tatu alitumwa Mughirah bin Shubah. Rustam alimshawishi Mughirah kwa pesa na kusema: "Nadhani ninyi ni maskini na mna njaa, tungewapeni utajiri ambao ungewatosha kwa maisha yenu yote.71 Kusikia maneno haya Mughira kwa hasira alijibu; "Ni kweli tulikuwa maskini, lakini Mwenyezi Mungu amebadilisha hali zetu baada ya kutuletea Mtume na kufuata ujumbe wake. Ametufundisha tumuabudu Mungu mmoja na tutangaze ujumbe wake. Mkisilimu ni ndugu zetu, hatutapigana, kama hamtaki, tulipeni Jizya, la sivyo ; upanga utatoa uamuzi wa mwisho". Maneno haya yalimkarisha sana Rustam
na kuapa kuwa jua tu litapochomoza atawauwa Waislamu wote. Mughirah alirudi
kwenye kambi ya Waislamu na ujumbe huu na kuliopokucha vita vya Qadisiya
vikaanza. Vita hivi vilipiganwa kwa muda wa siku tatu Rustam jemedari wa
Wapeshia aliuawa wapeshia wakachanganyikiwa pamoja na kuwa na jeshi la
tembo, maelfu wakauliwa na hatimaye Wapeshia wakashindwa. kufuatia ushindi
wa Qadisiya Waislamu waliwaswaga Wapeshia na kuteka Babal na Kutha na kuzingira
ngome kubwa maarufu ya Bahrahsher karibu na mji mkuu wa persia Mada’in
) ambayo hatimae ilitekwa. Vita hivi vilikuwa katika mwaka wa 14 A.H. (Juni
637) A.D. Baada ya muda wa miezi michache Waislamu waliona wakamilishe
ushindi wao kwa kuuteka mji mkuu wa persia Madain jambo ambalo walilitekeleza
kwa urahisi kabisa.
|
YALIYOMO
Tahariri Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa Id el Fitr Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM Barabara za Tabora zimepitwa na wakati Jicho la
Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya!
Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani Taarifa ya Kamati juu ya yaliyotokea Mwembechai Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika Kuongezeka kwa ajali za barabarani Njia ya
uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 4
Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao Kesi nyingine Mwembechai yaahirishwa Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|