|
|
| Je,
hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? (jibu)
NDUGU Mwinjilisti Dettu katoa mashairi yake kwa Anwani: Yesu Mwokozi wa Dunia (sisitizo). Jibu: Ndugu Mwinjilisti elewa hawa Mitume kwanza na ahadi aliyopewa babu yao Ibrahimu. Isaka ni mlolongo mpaka kwa Yesu katika ule uhamisho wa Babeli (Mt. 1:1-17). Ishmaeli ni mlolongo mpaka kwa Muhammad (s.a.w.) katika maseyidi kumi na mbili kwa mama Hijiri (mjakazi wa Sara). Mungu anamwambia Ibrahimu; katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa (Mwa 12:1-3). Ibrahimu wakati anataka kuaga dunia alimuomba Mungu nani atarithi baada ya kuondoka kwangu maana uliniahidi jamaa zote za dunia watabarikiwa (Mwa 15:1-3). Ndipo Mungu alipomjibu katika (Mwa 15:4-6). Mungu anamwambia Ibrahimu "atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi". Je! Isaka au Ishmaeli aliyetoka katika viuno? Jibu ni Ishmaeli maana Isaka ni mtoto wa ahadi (Mwa 18:9-12). Kwa Ishmaeli soma Mwa 16:2-4. Halafu Mungu anasema, "Ishmaeli atakuwa kama Punda-Mwitu kati ya watu mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake nae atakaa mbele yao ndugu zake wote" (yaani kuanzia Isaka mpaka Yesu) Mwa 16:10-12. Kisha Mungu anasema kwa Isaka. "Sara atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka nami nitafanya agano langu "imara" kwake kuwa agano la "milele" kwa ajili ya uzao wake ni Israeli sio watu wote kama ahadi ya Ishmaeli kuwa ya watu wote. Mungu anasema, "Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha nami nitamuongezea sana sana atazaa maseyidi kumi na wawili nami nitafanya awe "Taifa Kuu" Mwa 18:20. Ndio maana hata kabla ya kuzaliwa Yesu utabiri wa Ibrahimu ulitimia kama aya hizi hapa chini zinavyojieleza: "Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa "watu wake" na dhambi zao". Mat 1:21. "Nawe Bethlehemu katika nchi ya Yuda Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda kwa kuwa kwako atatoka mtawala atakayewachunga "Watu wangu Israeli". Baada ya kuzaliwa Yesu; kweli alisema kama ahadi ilivyo: "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli". (Mat 15:24) "Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako, na wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao". (YN 17:9) "Ataweka kondoo mkono wa kuume na mbuzi mkono wa kushoto" (Mat 25:31-33). Atamjibu Petro; Ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha Utukufu wake, ninyi mtaketi katika viti kumi na viwili mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Aliagiza wanafunzi wake: Katika njia ya mataifa msiende wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea wana kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mat 10:5). Aliwasisitiza: "Lakini watakapowafukuza katika mji huu kimbilieni mwingine, kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo Mwana wa Adamu (Mat 10:23). Akazidi kuwaasa: "Mwanafunzi hampiti mwalimu wake bali yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake" (Mat 10:24). "Msiwape mbwa kilicho kitakatifu wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao wakageuka na kuwararua". (Mat 7:6). "Si vema kutwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa". (Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kukiokoa kilichopotea) Mat 18:11. Yesu anasema; Jitieni nira yangu mjifunze kwangu" (Mat 11:29-30) Sasa ndugu yangu Mwinjilisti wewe unajifunza kwa nani mpaka useme Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu? Alipoonekana na wale wanafunzi kumi na mmoja kabla ya kupaa alisema: "Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; Lakini kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu" LK 24:49. Na wala sio kama Mathayo alivyoandika katika Mat 28:19-20 au Marko katika Mk 16:15-18 au Yohana katika YN 20:23. Na ushahidi wa hayo utaupata maana hata katika Matendo ya Mitume imeandikwa hiyo tu ya Luka soma MDO 1:4-5: Kuhusu Sheria na Amri: Mwinjilisti Bunga kazungumzia sheria nyingi na baadaye akagawanya tena kama Kanisa lilivyomuamuru; Lakini amejisahau kuwa hapaswi kuwa Msabato; maana hayuko huko yeye na yeyote yule; soma habari za kuifuta siku ya Jumamosi baada ya wale waliopewa siku hiyo kuasi (yaani Wayahudi) "Msilete tena matokeo ya utabili uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya wa Sabato kuita makutano siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. (Isa 1:13). Kwa maana ameinena siku ya Sabato mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote na hapo napo, Hawataingia rahani Mwangu, Basi kwa kuwa neno hili limebakia kwamba wako watu (yaani wewe) wataingia humo na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia (yaani Wana wa Israeli) kwa sababu ya kuasi kwao. (Waeb 4:4-6) Ukiendelea aya ya saba aweka tena siku fulani. "Na kwa yakini mmekwisha kujua (khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya kuihishimu) Jumamosi, Basi tukawaambia "Kuweni Manyani wadhalilifu". Qur 2:65. Mbona sheria za milele hazifuati ndugu Dettu? Kama vile sheria ya kutawadha, Mungu anasema niya milele (Kut 30:17-21). Yesu pia alisisitiza wakati anafundisha kutawadha kuwa amewapa "kielelezo" na mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda. (YN 13:5-17) Ndugu yangu Dettu Injili ya Paulo, Imani itendayo kazi bila matendo 2 Tim 2:8 kwa kumfata Paulo soma (Gal 2:16). Lakini Je! Paulo anaongozwa na nani? Soma 1 The 2:17-18 "Lakini sisi ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu, kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam mimi Paulo mara ya kwanza, na mara ya pili na "Shetani" katuzuia. Paulo hana Roho Mt (Gal 3:15). Alikupata kwa hila 2 Wak 12:16. Mwinjilisti anatenga sheria za Mungu na Musa wakati Musa alikuwa anaongea na Mungu moja kwa moja na Torati si utungo wa Musa bali ni maneno ya Mungu kupitia Mtume wake Musa, na Yesu alizifuata sheria hizo hizo: (Mat 5:17-20) Sikuja kutangua wala kupunguza (Yesu anasema). "Toa sadaka kama alivyoamuru Musa (Mat 8:4). "Imeandikwa nini katika Torati? Fanya hivi nawe utaishi" LK 10:25-28. Anasema Yesu kaichukuwa Dhambi ya Ulimwengu YN 1:29. Na bado unabatizwa kwa maji? Yohana Mbatizaji alisema, Mimi nabatiza kwa maji kwa ajili ya Toba Mat 3:11-12. Toba ya nini tena wakati Yesu kaondoka na dhambi zote? Yesu katumwa kuhubiri habari njema LK 4:42-43. Mbona Yesu aliogopa kufa? YN 7:1 "Yeye aliyenitia mikononi mwako (Pilao) yuna dhambi iliyo kubwa zaidi" (YN 19:11). Huo sio mpango wa Mungu kumuua Mtume wake bali ni Wayahudi kumsingizia kuwa kajifanya Mwana wa Mungu YN 19:7. Sisi tunayo sheria na kwa sheria hiyo amestahili kufa kwa sababu, alijifanya kuwa Mwana wa Mungu; sheria hiyo imo kwenye Torati Kumb 21:22-23. Ndugu Dettu "Haki yako isipozidi hiyo ya Waandishi na Mafarisayo...) Mat 5:20. Ndugu Dettu, nani kachukuwa msalaba wake Mt 27:32. Simon Mkirene au Yesu? Mat 19:16-17. "Waache watoto waje kwangu" Mat 19:14-15. "Alisikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu (Waeb 5:7). Baada ya kwenda kuomba kule kwenye bustani ya "Gethsemane" machozi yalikuwa kama damu (LK 22:44). "Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa" (EZE 18:20) Kumb 24:16 "Mababa wasiuwawe kwa ajili ya watoto wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao. (Wosia) Ndugu Waislamu Biblia hizi zinabadilishwa kupunguzwa au kuongezwa maneno kama Masheikh, Hekalu vinaondolewa, naomba mzihifadhi hizo ili kizazi kijacho kisipotoshwe. (Inaendelea wiki ijayo). |
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|