|
|
|
VIONGOZI wetu hutoa kauli zinazopingana kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar. Kwa upande mmoja viongozi hao hutuambia hakuna mtafaruku wa kisiasa Zanzibar, mambo ni shwari kabisa. Kwa upande mwingine viongozi hao hao wanaeleza kwamba matatizo ya kisiasa ya Zanzibar yatatatuliwa na Wazanzibari wenyewe! Hapa mtoa hoja SHOKA SHAMTE wa Pemba, Zanzibar anajaribu kuonyesha kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 ndio mzizi wa matatizo yote ya visiwa hivyo. Anadai Muungano nao ukaja pigilia msumari kuisulubu Zanzibar. ZANZIBAR ilipata uhuru wake kupitia uchaguzi uliofanyika 1963. Wakati huo ikiwa chini ya himaya (Pretectorate) na serikali iliundwa kutoka mwezi Desemba 1963 na Januari 12, 1964 Mapinduzi yalifanyika, serikali ilipinduliwa na Mzee Karume akawa Rais wa Zanzibar kupitia mapinduzi, wakati huo Tanganyika ikawa chini ya chama cha TANU. Wengi hawajui, hawaambiwi ukweli wa hali ilivyokuwa baina ya Desemba 1963 na Januari 12, 1964. Lakini kwa ufupi na ufasaha zaidi hali ile ile imejitokeza tena baada ya uchaguzi wa 1995, kundi moja linahisi limeonewa katika uchaguzi na moja linahisi ndilo lililoshinda, hivyo haki ya kuunda serikali linayo. Nazungumzia hiyo kwa sababu kumekuwa na desturi ya kupeana madaraka ya juu katika kile CCM wanachokiita mambo yote nyeti Hivyo, wakati Zanzibar inatimiza miaka 35 ya mapinduzi bado hali ya kisiasa Zanzibar haijakomaa. Pia kuna suala la Muungano. Wazanzibari bado hawajui haswa kwa nini Zanzibar imemezwa bila ya wao kupewa nafasi ya kueleza msimamo wa Zanzibar juu ya Muungano. Roland Brown ambaye ndiye aliyezitunga "Aricles of Union" za mwaka 1964 aliwahi kuwaambia Bw. Joseph Warioba mwaka 1982 pamoja na Mh. Pius Msekwa. Bw. Warioba wakati huo akiwa mwanasheria mkuu na Mh. Msekwa mkuu wa mkoa wa Tabora Juni 15, 1982 kwamba "Some two or three days after the revolution, they were approached to do what was then described as highly secretive work. The President started that it has been decided that there should be a union between Zanzibar and Tanganyika ... he did not a federation" Sasa iweje Muungano uliopitishwa siku tatu baada ya mapinduzi halafu isemwe kuwa Muungano ni utashi wa Wazanzibari wenyewe? Huo ulikuwa ni mwanzo tu wa kuimeza Zanzibar kwani baadaye Karume alikuja kutanabahi na akaanza kupinga maamuzi fulani fulani. Wakati umefika tuache kuburuzana
badala yake tujenge tabia ya kukubali udhaifu na kuurekebisha kwa manufaa
ya wote si mtu binafsi. Wazanzibari wenyewe waachiwe kuamua ni Muungano
au aina ipi ya serikali wanayoitaka kwa manufaa ya Zanzibar.
Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
WAISLAMU wametakiwa kutumia fursa ya kufufuliwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha dini yao, kujiendeleza kiuchumi na kujenga umoja madhubuti miongoni mwa Waislamu wa nchi hizi. Wito huo umetolewa na Sheikh Mohammed Amana wa Taasisi ya Islahil Islamiya ya Mombasa. Sheikh Amana ambaye alikuwa akitembelea mkoa wa Arusha hivi karibuni ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali za Tanzania, Kenya na Uganda kwa kuurejesha uhusiano wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Ili kunufaika na ushirikiano huo, Sheikh Amana amewataka Waislamu wa Tanzania, Kenya na Uganda kuiangalia historia yao ya EAMWS na kuifufua upya. Sambamba na wito huo, Sheikh Amana ametoa mapendekezo kadhaa juu ya kuboresha elimu kwa Waislamu. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na muhtasari mmoja kwa madrasa zote pamoja na kuwa na utaratibu wa kuwapima wanafunzi kwa mitihani ya aina moja. Aidha, amesema ni lazima waumini waandae utaratibu wa kuwatunza na kuwapa motisha waalimu na wanafunzi wanaofanya vizuri. Wakati huo huo, Sheikh Amana amewataka Waislamu kuiunga mkono Bakwata ili iweze kutekeleza majukumu yake. Alisema kwamba yeye binafsi asingependa kuona Waislamu wanaikashifu Bakwata, bali waikosoe, waielekeze na kama wapo viongozi wabovu wawang’oe kupitia taratibu zilizowekwa na Katiba ya Bakwata. Kwa upande mwingine, amewataka viongozi na Masheikh ambao wamekuwa vikwazo vya maendeleo ya Waislamu waache kung’ang’ania madaraka bali waheshimu matakwa ya waumini. Sheikh Mohammed Amana aliikumbusha Bakwata kwamba miongoni mwa majukumu yake ni pamoja nakuweka taratibu nzuri za kukusanya na kugawa zakati. Kuwajua na kuweka mipango mizuri ya kuwahudumia wajane na mayatima pamoja na kuangalia huduma za jamii kwa ujumla miongoni mwa Waislamu. |
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|