AN-NUUR 
Na.182 Ramadhan 1419, Januari 1 - 7, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Njaa yaikumba Kilwa 
 
  • Maembe yafanywa futari, daku
  • Nyani waipua masufuria jikoni
WAKATI Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye akifanya tathmini juu ya hali ya chakula nchini katika soko la Tandale Jijini Dar es Salaam, njaa kubwa imeukumba mji wa Kilwa na vitongoji vyake. 

Hali ya chakula mjini Kilwa ni mbaya ambapo baadhi ya watu huponea maembe na mizizi ya miti. 

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia baadhi ya Waislamu waliofunga wakifuturu maembe ya kuchemsha nyakati za magharibi. 

Njaa imeathiri maisha ya watu na wanyama na katika baadhi ya maeneo nyani wamekuwa wakivamia nyumba na kuipua vyungu jikoni. 

Maeneo ambayo yameathirika zaidi ni pamoja na Migelegele, Luhatwe, Kikale, Mitole, Njinjo na Nshotike ambako mwandishi alishuhudia makopa ya maembe yaliyoanikwa juani. 

Baa la njaa huenda likasababisha maafa zaidi baada ya msimu wa maembe kwisha, iwapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kuwanusuru wananchi wa wilaya hiyo. 

Kwa miaka miwili mfululizo wilaya ya Kilwa na vitongoji vyake imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na njaa na mafuriko. 

Mwaka 1997 Kilwa ilikumbwa na njaa iliyosababishwa na mafuriko yaliyoharibu mazao na nyumba kadhaa pamoja na kupoteza maisha ya watu wengi. 

Wananchi wilayani hapa wamekuwa wakiilalamikia serikali kwa kutochukua hatua za dharura kuwasaidia kukabiliana na majanga hayo. 

Wananchi hao wamesema viongozi wa serikali huonekana sehemu hizo nyakati za uchaguzi. 

Wakati huo huo, huku wananchi katika baadhi ya mikoa wakiendelea na maadhimisho ya kuukaribisha mwaka mpya 1999 na kuuaga mwaka 1998, mikoa ya Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara iko katika njaa kubwa. 

Taarifa kutoka mikoa hiyo zinafahamisha kuwa kuna uhaba mkubwa wa chakula ambao huenda ukasababisha maafa kwa wakazi walio wengi. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma

Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha

Matokeo ya Darasa la Saba yacheleweshwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi: Wananchi wahoji je, nchi hii ina dini moja tu?

Njaa yaikumba Kilwa

Dondoo za Saikolojia
Na. Abu Halima Sachangwa

Kona ya Wacha Mungu
Mavuno yangu yasiwe...

Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana huyoo!
Na Sompo wa Kahambwe

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897)

Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Imetayarishwa na Africa Muslims Agency

Marekani ni mtetezi au adui wa haki?: Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Na Abu Salim

Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Na Habiba Swedi, Arusha

Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an

Ijue  Madrasa Hudaa Arusha

Wazazi waaswa kutoshabikia maovu

Mzee maarufu afariki Moro

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? (jibu) 
Na Ally Said

Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani?

Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Na Habiba Swedi

Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar

Baada ya kuvunjiwa nyumba, kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Na Q. Mtaita

Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile

Sayansi na Teknolojia 
[Kuunganisha Kompyuta kwa Kutumia Modem

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Saumu na lishe ya mama anayenyonyesha] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita