|
|
|
Modem inaweza bila ya wasiwasi wowote kutumika kuunganisha kompyuta mbili kwa namna nyingi sana. Tutakazozizungumzia hapa chini ni namna mbili:
Kuunganisha kompyuta mbili zilizo mahali pamoja kwa kutumia modem Tuseme unazo kompyuta mbili na ungependa kunakili faili moja kutoka kwenye kompyuta moja kuingia kwenye kompyuta ya pili. Lakini kwa bahati mbaya huna diskette za kukusaidia kuifanya kazi hiyo; huna vifaa vya kukuwezesha kuziunganisha kompyuta hizo kwa kutumia Direct Cable Connection; na pia huna namna ya kuziunganisha kompyuta hizo kwenye LAN. Kama kompyuta zote mbili zina modem, basi ipo njia nyengine rahisi ya kuziunganisha. Fuata hatua zifuatazo:
X3: Tunaiambia modem ipige simu bila kungojea dial tone. Hiyo ni kwa sababu, modem zetu hatukuziunga kwenye line ya simu yoyote – tumeziunga zenyewe tu kwa hivyo hakuna dial tone. Dial tone huwa inatoka kwenye mitambo ya simu. Kupiga simu bila kungojea dial tone kunaitwa "blind dialing" – ndio maana tukatumia jina "blindial" kwenye hatua ya 3, ingawa haikuwa lazima kutumia jina hilo. Amri ya X3 ndiyo inayoruhusu kufanya blind dialing. D12345: Tunaiambia modem ipige simu nambari 12345. Nambari hiyo bila shaka ni ya bandia tu lakini kwa matumiazi yetu itakidhi haja. Tungeweza kutumia nambari nyengine yoyote ile. Sisi tunachotaka ni kuwa modem ipige simu – basi! Baada ya kompyuta zako mbili kuungana, unaweza kupeleka faili lolot lile kutoka kwenye kompyuta moja kwenda nyengine kwa kutumia HyperTerminal na kuchagua Transfer -> Send File, kama inavyoonekana kwenye Picha 3. Kwenye sehemu ya Filename kama inavyoonekana kwenye Picha 4, andika jina la faili unalotaka kulituma au unaweza kutumia Browse kulitafuta. Kwenye sehemu ya protokali ya Zmodem. Protokali hiyo ni protokali madhubuti sana ya kusafirishia mafaili kwa njia ya modem. Jinsi ilivyo madhubuti, ikitokezea kiungo kati ya modem na modem kukatika kutokana na sababu yoyote ile kabla ya faili halijamalizika kupelekwa, ukijaribu tena kulituma hilo file kwa njia hiyo, basi litaendelea kupelekwa sehemu iliyobaki tu, yaani halitaanza kupelekwa upya.
Ukishachagua Zmodem bonyeza Send na mara nyingi hutahitaji kufanya chochote kwenye kompyuta ya pili – moja kwa moja (automatically) faili hilo litapokelewa na kuwekwa kwenye jalada C:\Program Files\Accessories\HyperTerminal. Kama hukuliona hapo, basi tumia Start-> Find ulitafute lilipowekwa. Kama itahitajika, unaweza kwenye HyperTerminal ya kompyuta ya pili kubonyeza Transfer -> Receive File na uchagua jalada (directory) la kuwekwa faili hilo na kuwa Zmodem ndiyo protokali ya kutumika, na kisha bonyeza Receive. Ukimaliza shughuli zako, kwenye dirisha la HyperTerminal la kompyuta ya kwanza, toa amri ATH ya kukata mawasiliano (Hangup).
Tumeona hapo juu hapakuwa na lazima ya kuwa na line ya simu inayofanyakazi, kuunganisha kompyuta mbili zilizo mahali pamoja. Tumeziunganisha kwa kutumia waya tu wa simu (telephone cord) ambao unakuja pamoja na modem unapoinunua. Kama kompyuta ziko mbali mbali, tuseme moja iko nyumbani kwa rafiki yako na nyengine iko nyumbani kwako, au moja iko Dar es Salaam na nyengine iko Nairobi; hapo hatuna ujanja – itatubidi tutumie mawasiliano ya simu. Njia ya kutumia mawasiliano ya simu ni mufaka sana! Kwa mfano kampuni yako ina ofisi Arusha na ofisi hiyo inataka kutuma ripoti fulani makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Dar. Kama ripoti hiyo imeandikwa kwa kutumia Excel basi ni kiasi cha kulituma tu hilo faili la Excel kwa njia tutakayoieleza hapa chini. Tutautumia mfano huo ili kurahisisha maelezo yetu. Mambo yanayohitajika ni kwa ofisi ya Arusha pamoja na ya Dar, kuwa na kompyuta zenye Windows 95, modem, na line za simu zinazofanyakazi. Utaratibu wa kuunganisha kompyuta hizo ni kama ulivyoelezwa kwenye hatua ya 1 mpaka ya 8 zinazohusu kuunganisha kompyuta zilizo mahali pamoja, isipokuwa kuna tafauti ndogo zifuatazo:
Hitimisho Kwenye sehemu hii tumejifunza kuunganisha kompyuta mbili zilizo mahali pamoja kwa kutumia modem bila ya kuhitaji line ya simu. Pia tumejifunza kuunganisha kompyuta mbili zilizo mbali mbali kwa kutumia modem na mawasiliano ya simu. Katika njia zote mbili tumeweza kuona jinsi ya kusafirisha mafaili kwa kutumia protokali ya Zmodem. Tumejifunza kuwa kumbe modem hazitumiki kompyuta na Intaneti (Internet) tu kwa kupitia mitambo ya wanaotoa huduma za Intaneti (Internet Service Providers), bali hata sisi wenyewe kwa wenyewe tunaweza kuziunganisha kompyuta zetu kwa kutumia modem na tukaweza kupelekeana mafaili moja kwa moja badala ya kuepelekeana diskette kwa njia ya posta. |
YALIYOMO
Tahariri Kingunge, kweli upo uonevu na dhulma Wananchi wahoji kuhusu polisi aliyeua Arusha Dondoo za Saikolojia
Kona ya Wacha Mungu
Jicho la Uzalendo: Bhabhoo! Muungwana
huyoo!
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) Mafunzo kuhusu funga ya Ramadhani
Marekani ni mtetezi au adui wa haki?:
Umoja wa Mataifa upo upande gani?
Dawa ya ukimwi ni mwenendo mwema
Mwalimu Maif: Mwanamke aliyetumia maisha yake kufundisha Qur'an Wazazi waaswa kutoshabikia maovu Je, hivi tuendelee kushika amri za
Mungu tena? (jibu)
Mapinduzi, Muungano kwa manufaa ya nani? Fufueni EAMWS - Sheikh Amana
Msiitupie lawama serikali - Dk. Omar Baada ya kuvunjiwa nyumba,
kuchomewa vyakula na Serikali: Nzasa sasa wafuturu Maembe
Acheni mifumo mibovu, fuateni Qur'an - Sheikh Kilemile Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|