AN-NUUR 
Na.183 Ramadhan 1419, Januari 8 - 14, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Tahariri 

Onyesheni ushujaa wa Badri 

Dhulma itaondoka mtakapoamua kuiondoa 
  

WIKI ijayo wanafunzi wa kidato cha nne wanaanza mitihani yao ya mwisho. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, wanafunzi Waislamu licha ya kufanya mitihani yao huku wakiwa ndani ya swaumu; lakini pia watalazimika kufanya mitihani hiyo siku ya Eid el Fitr. 

Yaelekea serikali katika kutoa ratiba hii haikufikiria wala kujali hisia za wale ambao watakuwa wamefunga au kulazimika kufanya mitihani siku ya Eid el Fitr. Inawezekana hii ni kutokana na ukweli kwamba serikali haina dini japo inadai kwamba inaheshimu dini za watu. 

Lakini katika kipindi hicho hicho cha kutolewa ratiba hii; serikali hiyo hiyo imetutangazia kwamba imeahirisha kutangaza matokeo ya darasa la saba ili kusiwe na dosari katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi. 

Kwamba lau matokeo hayo yangetangazwa siku chache kabla ya Krismasi wale watoto wa Kikristo ambao wamefeli wasingekuwa na furaha katika sikukuu hiyo. 

Lililo wazi hapa ni kuwa serikali inajali na kuheshimu hisia za Wakristo katika utendaji wake. Haitendi kana kwamba Wakristo hawapo wala haingoji kuombwa au kukumbushwa na Wakristo juu ya yale wayatakayo. 

Wengi watakuwa wanajiuliza ni ujumbe gani huu serikali imekusudia kuwawasilishia Waislamu? Huyu wa kusherehekea Krismasi; kutangazwa mitihani kabla au baada ya Krismasi hakuathiri lolote matokeo yake ya mtihani. Lakini pamoja na hayo serikali inamwambia; "tunakujali". 

Ila huyu ambaye matokeo ya mitihani yake yaweza kuathiriwa na mazingira anayoyafanyia mtihani sasa, hakuna anayejali. 

Yapo mengi ambayo wanafunzi Waislamu wamekuwa wakiyalalamikia huko mashuleni. Kwa hiyo, hili haliwezi kuwashtua sana. Pengine imekuwa ni kheri ili umma upate kufahamu kwamba yale wanafunzi Waislamu wanayolalamikia juu ya uonevu na dhulma dhidi yao ni kweli. 

Hapana shaka wanafunzi hawa wataingia katika vyumba vyao vya mitihani wakiwa mashujaa wa Badri. Mashujaa ambao wamepata bahati ya kushuhudia ule upendeleo wa kutangazwa waziwazi katika kipindi chao. Mashujaa ambao wanaingia kwenye vyumba vya mitihani wakijua kwamba hawana wa kuwajali kama wengine. 

Kama walivyokuwa Mashahid wa Badri karne 15 zilizopita, hatuna shaka tanuri hili la kufanya mitihani ndani ya swaumu na siku ya Eid el Fitr litanoa fikra zao na ushujaa wao wawe wapiganaji hodari wa kuleta ukombozi wa Waislamu. 

Ni kwa mantiki hiyo hiyo hatutarajii yeyote katika wanafunzi Waislamu afuate ushauri wa wale wenye kuifanyia stizai dini ya Allah (s.w.). Wale ambao hudai kwamba katika Uislamu kuna dharura na hivyo kuwataka waache kufunga siku za mitihani. 

Suala la msingi linalopasa vijana wetu walitambue ni kwamba hoja hapa si kufanya mitihani mwezi wa Ramadhani, lakini ule upeo wa ubaguzi, dhulma na upendeleo ulipofikia. Kwamba serikali haioni taabu kuwaambia wanafunzi Waislamu wafanye mtihani siku ya Eid el Fitr yao, lakini hujali kila Mkristo aisherehekee vyema Krismasi yake. 

Kubwa kwa sasa ni umma kushuhudia upendeleo huu na maadhali serikali ina uwezo na mabavu na mwelekeo wake ndio huu, bado tutaendelea kushuhudia mengi. Lakini, je, tushuhudie mpaka lini? Haki haiombwi wala dhulma haiondoki yenyewe, huondolewa. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Onyesheni ushujaa wa Badri 

Daniel kuwatimua waumini Msikitini 

Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu 

Dondoo za Kisakolojia 
Na. Abu Halima Sachangwa 

Kona ya WachaMungu  

Jicho la Uzalendo 

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 

Vipi umoja wetu uwe hatari ? 

MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ  

Marekani si rafiki mwema  

Tunahitaji UN ya Waislamu - 2  

Njia bora zitakazotusaidia kuwalea watoto 
Na Ust. Hashim Rusaganya, Mombasa 

Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni I Arusha. 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.) 
Na Mwapwani Mohammed 

Sheikh Kisiwa atunuku zawadi 

Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata Msikiti mpya  
Na Mwandishi Wetu, Mwanza  

Huduma za maji Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zuberi, Kondoa  

Mnyororo wa imani 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Je, Yesu alibatizwa? 
Na Muhibu Said  

Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama  

Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa 

Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro 
Na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Tatizo la mwaka 2000] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Chakula na lishe 
[Mlo wa siku ya Idd] 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita