|
|
|
WAISLAMU wametakiwa kutumia mali zao vizuri kwa kufuata maadili ya Uislamu katika maisha yao ya kila siku. Hayo yalisemwa na Sheikh Kisiwa Ally baada ya kutunuku zawadi kwa wanafunzi na walimu katika tamasha la mashindano ya kusoma kwa kuhifadhi Qur’an lililofanyika hivi karibuni katika shule ya msingi Uhuru mjini hapa. Sheikh Kisiwa ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa wa Arusha, alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo lililoandaliwa na taasisi ya Masjidul Hidaya and Islamic Centre Olmatejo. Awali, Sheikh Kisiwa aliipongeza taasisi ya Masjidul Hidaya and Islamic Centre kwa kuandaa tamasha hilo kwa kusema kuwa ni jambo zuri kwani linatoa fursa ya kuwapima vijana juu ya ufahamu wao wa Qur’an na kiwango walichokihifadhi. Aliwaeleza wazazi na wageni mbalimbali waliohudhuria kuwa ni bora wakajizatiti ili kuyakuza mashindano hayo yafikie ngazi za juu kimkoa hadi taifa ili kuweka ushindani mkubwa ambao vijana kutoka madrasa mbalimbali ndani na nje ya mkoa watachuana. Pia aliwataka Waislamu kujitolea kwa hali na mali kutunisha mfuko ili kufanikisha mashindano ya aina hiyo kwa siku zijazo na kuweka mkakati wa pamoja wa kujihimiza madrasa zitilie nguvu suala la usomaji wa Qur’an. Aidha, Sheikh Kisiwa alifahamisha kuwa uongozi wa Manispaa ya Arusha unakamilisha taratibu za kupatikana kwa eneo jipya la makaburi kufuatia kujaa kwa eneo lililopo hivi sasa. Hata hivyo alitahadharisha kuwa eneo hilo jipya liko nje kidogo ya mji wa Arusha, na kwamba usafiri wa kumudu utahitajika ili kurahisisha mawasiliano. Hivyo, aliwataka Waislamu Arusha kujiandaa na michango ya kupata usafiri pindi watakapotakiwa kutekeleza hivyo. Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’an yaliwashirikisha zaidi ya wanafunzi 34 kutoka Madrasatul Hidaya inayomilikiwa na taasisi iliyoandaa na mwanafunzi mmoja kutoka madrasa ya Majengo kitongoji kimoja cha hapa Arusha. Pia wazazi na wageni mbalimbali mashuhuri walihudhuria ambapo ni pamoja na Sheikh wa Wilaya Sheikh Shaaban Juma, Ustadh Yahya Mgeni kutoka Nairobi, Bwana Miraji kutoka Shia Centre na Sheikh Hashim Lema, hao ni baadhi yao tu. Akitoa taarifa fupi, Katibu wa Taasisi hiyo Sheikh Juma Saidi Mndeme alisema azma kubwa ya mashindano hayo ni kuwalea vijana wa Kiislamu waweze kuifahamu Qur’an kwani ndio mwongozo pekee uliobaki na kwamba hiyo Qur’an iweze kutumika kama chombo cha kuwaunganisha Waislamu wa madhehebu zote kwa kuondoa tofauti zao na kuweza kushirikiana kuinua kiwango cha usomaji Qur’an. Jumla ya majaji watatu kutoka baadhi ya Misikiti ya mjini hapa walishiriki kikamilifu katika utafutaji wa washindi. Washindi 16 walipatikana waliohifadhi Qur’an kuanzia juzuu ya kwanza hadi ya kumi na tano. Wote hao walizawadiwa zawadi mbalimbali zikiwa ni pamoja na mshindi wa kwanza wa kuhifadhi juzuu kumi na tano Issa Yahya (15) kutunukiwa baiskeli aina ya Phoenix yenye thamani ya shilingi 75,000, mshindi wa pili wa kuhifadhi juzuu kumi na tano alipata Radio Cassette bendi 4. Zawadi nyingine kwa washindi wa kuanzia juzuu kumi hadi moja ni cherehani aina ya Butterfly yenye thamani ya shilingi 70,000 iliyotwaliwa na Naima Saidi mshindi wa kuhifadhi juzuu kumi. Magodoro, Redio, pasi ya umeme aina ya Philips, kanzu, hijab, saa za ukutani na majiko ya mafuta ya taa. Zikiwemo pia zawadi za jumla kwa washiriki nazo ni tochi, misahafu na saa za mkononi. Kivutio kikubwa katika mashindano hayo kilikuwa ni pale mtoto Gingi Issa Gingi (8) aliposoma Qur’an vizuri na wengi kufurahia. Alishinda katika waliohifadhi juzuu moja na kupata saa ya adhana. Walimu watano nao walitunukiwa zawadi siku hiyo mwalimu wa siku nyingi madrasani hapo, Maalim Juma Haji alipata televisheni aina ya Hitachi inchi 14 yenye thamani ya shilingi 220,000, Mwalimu Mkuu alipata saa ya mkono, Maalim Yasiri alipewa saa ya ukutani, Maalim Adam alipata saa ya mkono na Mwalimu wa kinamama Ustadha Mariam alitunukiwa saa ya mkono. Wakati huo huo, jumla ya fedha taslim shilingi 20,300 zilikusanywa katika tamasha la kusoma na kuhifadhi Qur’an kama mwanzo tu wa kutunisha mfuko wa mashindano yajayo. Akitangaza kima hicho, Sheikh Hashim Lema aliwashukuru wote waliotoa
michango yao na kukaribisha michango zaidi kutoka kwa Waislamu.
WATUMISHI wa Chuo cha Kilimo cha Ukiriguru kilichoo mjini Mwanza wameanza rasmi ujenzi wa Msikiti katika eneo ambalo wamepewa na Utawala wa Chuo. Eneo hilo ambalo limo ndani ya Chuo hicho, kuna Msikiti ambao ni wa zamani mno na tayari kuta zake zina nyufa na baadhi zimeanguka kabisa. Akiongea na ANNUUR, mjumbe mmoja wa kamati ya Msikiti huo alidokeza kuwa wamekuwa katika hali ngumu ya kuuendeleza Msikiti huo. Kwa muda mrefu, wamekuwa wakichangishana kwa kila mwezi kwa kila familia. Amesema kuwa pesa hizo hazitoshi kuanza ujenzi kutokana gharama za vifaa vya ujenzi kuwa kubwa, alitaja kuwa kuna familia arobaini za Waislamu chuoni hapo, kwa kuwa wamelazimika kumuweka Mwalimu wa Madrasa wa kuwasomesha watoto wao imekuwa ni vigumu wao kumudu gharama zote kwa wakati mmoja. Umoja wa ufundishaji Madrasa (UUM) ambao ni mchanganyiko wa vijana ambao wamejikusanya ili kuhuisha elimu katika madrasa mbalimbali hasa za nje ya mji wa Mwanza, makao yako Msikiti wa Memani, Mwanza na wanaendesha masomo mbalimbali hasa Qur’an kwa watu wazima saa za jioni Msikitini hapo. Mwenyekiti wa umoja huo ni Ustadh Shaaban Juma Kondo aliliambia ANNUUR kuwa pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa madrasa za nje ya mji wa Mwanza pia wamekubali kushirikiana na uongozi huo wa Msikiti wa Ukiriguru kujenga Msikiti ho kwa kutoa vifaa vya ujenzi na wao kwenda huko kila Jumapili kufanya kazi ya kawaida kupunguza gharama za ujenzi. Vijana wa UUM tayari wanaendesha madrasa za Usagara, Fela ambapo wanajenga madrasa katika kiwanja kilichotolewa na Muislamu mmoja mkazi wa hapo Fela, tayari wameshatoa vifaa vya kufundishia kwa madrasa za Igogo, Kalunda, Katunguru na baadhi ya madrasa za Mwanza Mjini. Hali kadhalika, wanalipa posho kwa walimu ambao madrasa zao hazina vipato
ili kukidhi mahitaji muhimu ya maisha, wamebuni Sylabasi ya namna ya kusomesha
Qur’an kwa muda mfupi na mtoto kuweza kusoma bila matatizo yoyote. Katika
madrasa ambazo wanashirikiana wao ndio wanaowatungia mitihani kwa mujibu
wa sylabasi zao.
Na Abu Zuberi, Kondoa WAKAZI wa kijiji cha Hamai Tarafa ya Goima wilayani Kondoa wamekuwa na usumbufu wa muda mrefu na adha kubwa ya kutembea mwendo mrefu kuchota maji. Mama mmoja aliyejitambulisha kuwa Mama Bahati ambaye ni mkazi wa kijijini hapo, akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa muda wetu wa uzalishaji unaathiriwa sana na kuhangaika kuchota maji, kwani inawabidi kuamka asubuhi sana na kutumia zaidi ya masaa matatu kwa kuyapata maji hayo. Mwandishi wa habari hizi alibahatika kufika hapo kisimani na kumwona mama Bahati akiwa ndani ya kisima huku kikikanyagwa kwa miguu na kufikia hatua ya kuyachafua hayo maji. Katika kijiji cha Hamai na Songolo, kuna wakazi wasiopungua 3000, wenyeji wake hulima mazao ya mtama, uwele, ulezi na mbaazi. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia vijana wadogo wakitoa huduma za kusafirisha abiria kwa kutumia baiskeli na kwa bei atakayopanga mteja. Serikali katika ilani yake ya uchaguzi ilitoa ahadi nyingi na nzuri. Lakini machungu yanayowapata wananchi vijijini hawana hamu hata ya kuishi. Wakati huo huo, Waislamu wa kijiji cha Songolo tarafa ya Goima wilayani Kondoa, wamewaomba Waislamu kuisaidia madrasa ya Shamsiya iliyopo kijijini hapo kumalizia jengo. Akitoa taarifa hizi, Katibu wa kamati ya ujenzi, Sheikh Rashid Ally alimuelezea mwandishi wa gazeti hili kuwa tangu mwaka 1992 wakati Mufti Mkuu Sheikh Hemed bin Juma bin Hemed alipoweka jiwe la msingi hapakutokea jitihada za kuridhisha kuendeleza jengo hilo. Madrasatil Shamsiya yenye wanafunzi 65, wakiwa na darasa la kina mama wapatao 20 wanasomea ndani ya jengo ambalo halikuwezekwa, hivyo hali ya kuendelea na ratiba ya kusoma wakati wa mvua huwa ngumu, aidha kipindi cha jua kinawafanya wanafunzi kuwa katika hali ngumu ya joto. Ustadh Mohamed Rashidi ambaye ni mwalimu wa madrasa hiyo alimueleza mwandishi wa habari hizi kuwa Waislamu hawana mzuri wa kutoa hata hili jengo la madrasa lilikuwa ni nyumba ya mtu, na hata hivyo, Waislamu wameshindwa kuliendeleza kwa muda wa miaka saba sasa. Pamoja na hali hiyo, wanawaomba ndugu zao wa Kiislamu kuwasadia katika ujenzi wa jengo hilo ambalo limefikia sehemu ya linta |
YALIYOMO
Tahariri Onyesheni ushujaa wa Badri Daniel kuwatimua waumini Msikitini Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu Dondoo za Kisakolojia
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ Njia bora zitakazotusaidia kuwalea
watoto
Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni
I Arusha.
Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)
Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata
Msikiti mpya
Huduma za maji Kondoa haziridhishi
Mnyororo wa imani
Je, Yesu alibatizwa?
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa Sheikh Bafadhil ateuliwa
kudhamini waandishi wa habari Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|