AN-NUUR 
Na.183 Ramadhan 1419, Januari 8 - 14, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro:

Masheikh wa mjini watupiwa lawama
 
  • Wenye elimu wadaiwa kugombea ukubwa Misikitini 
  • Wengine walumbana kwa tofauti za kiitikadi na ukabila 
  • Misikiti hatarini kugeuzwa maghala ya pamba 
WASOMI wa Kiislamu na Masheikh wa Mjini Morogoro wametupiwa lawama kali kutokana na kujihusisha na mambo ya laghwi mjini huku Uislamu ukiangamia vijijini kutokana na wanavijiji wa Kiislamu kukosa elimu sahihi ya dini yao. 

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Ustaadh Yunus Abdallah katika Msikiti wa Merela Morogoro vijijini alipokuwa akiwahutubia Waislamu wa tarafa ya Merela katika sala ya Ijumaa kufuatia Waislamu kadhaa wa tarafa hiyo kuritadiwa wakisaidiwa na "Sheikh" wao ambaye aliomba msamaha baadaye kwa madai kuwa "alighafirika". 

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili uligundua kwa kadhia hiyo ilitokana na uchache wa elimu sahihi ya Uislamu tarafani hapo. 

Akiuweka wazi ukweli wa mambo, Ustadh Yunus ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa vijana wa Msikiti wa Kiwanja cha Ndege mjini hapa, alisema kwamba wasomi wa Kiislamu mjini Morogoro wana dhima kubwa ya kujibu mbele ya Allah (s.w.) kwani hawatumii vilivyo elimu yao kwa manufaa ya Uislamu na Waislamu kiujumla, badala yake wanaitumia kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo ni hujuma chafu dhidi ya Uislamu. 

"Tumeachana na Qur’an na Sunnah za Mtume (s.a.w.) na kufungua kitabu kipya cha malumbano ya kiitikadi, kitendo ambacho maadui wa Uislamu wanakitumia vizuri kutudidimiza", alisema kijana huyo. 

Aidha, Ustadh Yunus aliwaonya wasomi hao kuwa kuwagawa Waislamu kwa vigezo vya ukabila hasa Ukigoma kwa upande mmoja na Uruguru au "Tuimanye" kwa upande mwingine. 

"Waislamu ni kitu kimoja, si rangi, kabila, jinsia, hali zao kiuchumi au kimaumbile (walemavu na wazima) ndizo zinazotambulisha umoja wao, bali Allah (s.w.) wa pekee", alisema. 

Akiwaelezea matajiri wa Kiislamu wa mjini hapa, kiongozi huyo wa vijana aliwaeleza wazi kuwa utajiri wao hauna mashaka yoyote kwa Uislamu, kinyume chake unawanufaisha wasio kuwa Waislamu kwa kuwajengea mashule na vyuo vikuu. 

Naye Ustadh Mohammed Kisanda akizungumza katika ziara hiyo aliwataka Waislamu wa vijijini kuzama katika elimu sahihi ya Uislamu na akawaonya wasithubutu kuigawa elimu katika matapo mawili (elimu dunia na akhera). 

"Tukipuuza elimu au kuigawa, majengo ya madrasa zetu hata Misikiti si muda mrefu itageuzwa maghala ya kuhifadhia pamba na mpunga", alionya Ustadh Kisanda 



Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa 

ABIRIA waliokuwa wakisafiri katika basi la Champion Bus Service kutoka Kondoa kwenda vijiji vya Mondo, Simba Songolo hadi Soya walipatwa na hasira pale waliponajisiwa nguo zao na pombe kutokana na kupasuka kwa chupa. 

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi mjini Kondoa, wakati kondakta wa basi hilo Bwana Sabiiku alipomwamuru utingo wake aliyejulikana kwa jina la Nuuri kupakia kreti mbili za bia aina ya Safari Lager. 

Katika harakati hizo, kreti moja iliponyoka na chupa kuvunjika juu ya keria ya basi hilo na pombe kuanza kuwaloanisha abiria, kitendo hicho kilaaniwa vikali na Watu waliokuwa ndani ya basi hilo. 

Watu hao walichukuzwa zaidi na kitendo hicho hasa kwa kile mmiliki wa basi hilo ni Muislamu, hata heshima ya mwezi mtukufu hakuna, alidai Bwana mmoja, 

Aidha, Sheikh Suleiman Mhunzi aliitumia nafasi hiyo kwa kuwaeleza abiria kuwa si kwa mnywaji wa pombe aliyelaaniwa hata yule mwenye kuibeba na kutumia kipato chake nao wamelaaniwa vile vile. 

Mwandishi wa habari hizi aliyekuwa ndani ya gari hilo alimsikia kondakta Bwana Sabiiku akimuamrisha utingo wake achukue maji na kufuta sehemu hiyo ya mlangoni hatua ambayo haikusaidia kwani abiria waliokaa mlangoni walikuwa wamelowanishwa. 


Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro
 
 
Na Mussa Ally, Morogoro

CHAMA kipya cha waandishi wa habari wa kujitegemea Morogoro (MFJA) kimemteua Sheikh Mkuu wa Mkoa Sheikh Omar Bafadhil kuwa mmoja wa wadhamini wake mwishoni mwa wiki katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika ofisi za muda za chama hicho zilizopo barabara ya Stesheni mjini hapa. 

Aidha, uliwateua wadhamini wengine wanne ambao ni pamoja na Bwana Idan Hassan Libenanga, meneja wa TTCL Morogoro, Bwana Bendera Mwenyekiti wa bodi ya maji mkoa, Bw. Petro Kingu na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa Bw. Aman Komanya. 

Pia mkutano umemchagua Bw. Boniventura Mtalimbo kama Mwenyekiti wake akisaidiwa na Bw. Thadei Hafigwa. 

Wengine ni Bwana Seraph Kuandika aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu akisaidiwa na Bwana Rajab Rajab. 

Bi. Gladness Mushi alichaguliwa kuwa Mweka hazina akisaidiwa na Bwana Gaudence Masati, wakati Bwana Mussa Ally na Bi. Jamila Malinza walichaguliwa kuwa wajumbe wa kamati hiyo ya utendaji itakayoongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. 

MFJA imeundwa kwa lengo la kusimamia maslahi, kutetea haki, kuwaunganisha na kuwaendeleza kitaaluma waandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Morogoro. 

Wakati huo huo, wito umetolewa kwa vijana wa Kiislamu wenye elimu ya kutosha kujiunga na taaluma ya uandishi wa habari ili kuutetea na kuuendeleza Uislamu na Waislamu kiujumla. 

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waislamu wa mjini hapa walipoongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti kufuatia pengo lililoonekana hasa mjini Morogoro ambapo Uislamu na Waislamu hususan vijijini wanaelekea kaburini kimaendeleo bila ya ulimwengu wa Kiislamu kujua kutokana na ukosefu wa waandishi wa habari wa Kiislamu mjini hapa. 

Hadi hivi sasa waandishi wa Kiislamu mjini Morogoro hawazidi wawili, jambo ambao ni msiba mkubwa kwa ulimwengu wa habari za Kiislamu. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Onyesheni ushujaa wa Badri  

Daniel kuwatimua waumini Msikitini  

Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu  

Dondoo za Kisakolojia  
Na. Abu Halima Sachangwa  

Kona ya WachaMungu   

Jicho la Uzalendo  

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2  

Vipi umoja wetu uwe hatari ?  

MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ   

Marekani si rafiki mwema   

Tunahitaji UN ya Waislamu - 2   

Njia bora zitakazotusaidia kuwalea watoto  
Na Ust. Hashim Rusaganya, Mombasa  

Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni I Arusha.  
Na Habiba Swedi, Arusha  

Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)  
Na Mwapwani Mohammed  

Sheikh Kisiwa atunuku zawadi  

Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata Msikiti mpya   
Na Mwandishi Wetu, Mwanza   

Huduma za maji Kondoa haziridhishi  
Na Abu Zuberi, Kondoa   

Mnyororo wa imani  
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa  

Je, Yesu alibatizwa?  
Na Muhibu Said   

Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama   

Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa  

Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro  
Na Mussa Ally, Morogoro  

Sayansi na Teknolojia  
[Tatizo la mwaka 2000]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Chakula na lishe  
[Mlo wa siku ya Idd] 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita