|
|
|
Alipofika Ufaransa akaanzisha chama cha siri kilichoitwa Jamiatul-Urwal-Uthaq, chama cha Kiislamu kilichopinga ukoloni kwenye nchi za Kiislamu, akawa Mwenyekiti wa chama hicho na akaanzisha Jarida na likiwa na makala 18 lilianza Machi 13, 1984 mpaka Oktoba 16, 1984 jarida hilo lililokuwa likitumwa katika nchi za Kiislamu, lilisimamisha uchapishwaji baada ya vibaraka wa kikoloni katika nchi za Kiislamu pamoja na Uingereza yenyewe kulipiga marufuku na mtu aliyepatikana na nakala la gazeti hilo basi ilitishiwa kuwa angefungwa jela miaka miwili au kulipa faini ya Paundi mia moja. Mwishoni mwa mwaka 1886 akaondoka Ufaransa na kuelekea katika nchi za Kiislamu kwa ajili ya kuhamasisha harakati za Kiislamu. Alipowasili katika bandari ya Kusini mwa Bushrar nchini Iran, mfalme Nasssirdin wa Iran alituma ujumbe kumtaka aende Tehran akamsaidie kuendesha serikali yake na kumuahidi kwamba serikali hiyo itakuwa imeundwa kwa kufuata maongozo ya Kiislamu. Januari 18, 1887 aliwasili Tehran alianza harakati zake, haikupita muda mrefu wakagombana na mfalme Nassirdin na akaondoka Mei 3, 1887 na kuelekea Uingereza kupitia Moscow katika mji wa Walad Kawkaz akatulia kwa muda nchini Urusi na kuhamasisha Waislamu kutokubali muongozo wowote usiokuwa na malengo na taratibu za Kiislamu. Baada ya kutoka Urusi hakwenda tena Uingereza bali alirudi Ufaransa kabla ya kufika Ufaransa aliweka maskani yake kwa muda nchini Ujerumani. Mfalme Nassirdin wa Iran akatuma tena ujumbe na kumfuata Ujerumani kumwomba arejee Iran ili kuweza kuunda dola imara ya Kiislamu, akakubali. Alipofika Tehran alipokelewa na kupewa cheo cha Uwaziri Mkuu lakini hakudumu kwani mnamo mwaka 1890 ukazuka mgogoro kwa mara nyingine baina yake na mfalme Nassirdin alipokuwa anajiandaa kuondoka nchini Iran, mfalme Nassirdin akatuma askari mia tano wakamkamata na kumpeleka Iraq. Alipokuwa Iraq alikutana na Ally Akbar Shiraq na kumsimulia matatizo na misukosuko aliyoipata nchini Iran na kuelezea kuwa mfalme Nassirdin ni kibaraka wa Uingereza, anauhujumu Uislamu na kwa Uingereza ilikuwa na maslahi yake hasa kwa zao la tumbaku ya Uingereza ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa wingi mashariki ya kati baada ya hapo Maulamaa kwa pamoja wakatoa tamko kwamba tumbaku ni haramu jambo lililoipelekea Uingereza kuingia hasara kubwa. Sheikh Jamaldin Afghan alipokuwa Baghdad akaandika makala mbili za kumshutumu mfalme Nassirdin pamoja na vibaraka wengine ya kwanza, iliitwa Ahwal Fans Hadhira na ya pili ni Bilao Faris zote zikiwashutumu Waislamu vibaraka. Baadaye akaondoka na kwenda huko huko kwa wagomvi wake wakuu Uingereza kueneza Uislamu. Mwaka 1892 Sultani wa pili wa Dollat Uthmaniya Abdulhamid akapeleka ujumbe Uingereza kumtaka aende Uturuki ili kuhamasisha nguvu mpya ya umma wa Kiislamu ambao ulikuwa unaanza kutetereka dhidi ya maadui wa Uislamu, Sultan alimwambia: "Mimi nataka kwa juhudi zako kwa kuwa wewe ni mtu muhimu katika umma huu, tuziunganishe nchi zote za Kiislamu chini ya amri moja pasina ubaguzi wa kitaifa tuweze kushinda magharibi katika teknolojia na kuzuia magharibi kutawala katika nchi za Waislamu kwa msaada wa Allah". Jamaldin Afghan akaanza kuandika barua na makala na kuzituma katika nchi za Kiislamu ili kuleta umoja na pia aliendelea na mashambulizi yake dhidi ya serikali ya kifalme ya Iran na zile nchi za Kiislamu zilizoufanya Uislamu kuwa ni dini ya kawaida na si dola, jambo hilo lilimuudhi sana mfalme Nassirdin wa Iran ikabidi atume ujumbe kwa sultan Abdulhamid amzuie na harakati hizo. Jamaldin hakuacha, aliendelea na kuvunja mtandao wa kikoloni katika ulimwengu wa Kiislamu. Kauli yake maarufu siku zote alikuwa akiwataka Waislamu kutojisalimisha kwa makafiri wa pande zote za ulimwengu ambao wanafanya juhudi za kudhoofidha Waislamu siku hadi siku na akisema kwa ukali kuwaambia Waislamu "Enyi Waislamu watukufu amkeni msiupe nafasi udhalili na unyonge, simameni chini ya uongozi mmoja wenye lengo moja". Baada ya hapo akaweka mipango mipya zaidi baada ya kumuona Sultan Abdulhamid anatetereka katika uendeshaji dolat Uthmaniya na kila mara Sultan Abdulhamid alikuwa hatekelezi ahadi anazokubaliana na Jamaldin Afghan mara nyingi alikuwa akitumia kauli yake maarufu kumwambia Sultan Abdulhamid: "Nimekuja kwako ili kupunguza kiapo changu kwako na kukwambia kwamba wewe ni kiongozi wa dola ya Kiislamu Khalifa wetu na Khalifa wa Kiislamu ni mkweli havunji ahadi atoazo Subhanallah, Sultan unachezea imani za umma wa Kiislamu kwa mapenzi ya nafsi yako". Msimamo huo ulipelekea kupata msukosuko na kuzuiwa kutoka nyumbani kwake na mara nyingine kutotoka nje na akawekewa majasusi kumi kumchunguza mahala popote anapokwenda na nini anachoongea. Sultan Abdulhamid katika kutapatapa akawa anamlipa mshahara na akampa nafasi ili kumliwaza na kumsahaulisha wajibu wake katika jamii, lakini yote hayo hayakufanikiwa aliendelea na harakati zake kwa bahati nzuri mfalme wa Japan akatuma ujumbe kwa Sultan Abdulhamid kumtaka ampeleke Sheikh Jamaldin na Maulamaa wengine kwenda kumfundisha Uislamu na kuwafundisha Wajapan dini hiyo, lakini Sultan Abdulhamid hakufanya hivyo badala yake alimtumia mfalme wa Japan zawadi ya kitabu jambo hili lilimuudhi sana Jamaldin Afghan na kumwambia Sultan Abdulhamid kwamba anafanya kosa kubwa mno kuzuia Wajapan wasipelekewe neema hii kubwa ya Uislamu. Mara ya pili likaja kundi la Wamarekani waliosilimu walipokuwa nchini India kiutalii kundi hili lilipokuwa likirejea nyumbani lilipitia Islambul na kumuomba Sultan Abdulhamid amruhusu Jamaldin Afghan na Maulamaa kadhaa kuongozana nao mpaka Amerika kufundisha Uislamu, kwa mara nyingine Sultan Abdulhamid akafanya tena khiyana. Mvutano wake na Jamaldin ukawa unazidi kupamba moto akaongeza majasusi kumdhibiti Jamaldin Afghan. Siku moja Sheikh Jamaldin alipokuwa akitembea na farasi mjini alipotupa jicho nyuma akamuona jasusi mmoja akimfuata lakini jasusi huyo alikuwa hana kipando chochote alikuwa akikimbia kwa miguu kumfuata, kwa bahati mbele kulikuwa na wajumbe wa Sultan wakija akawasimamisha na kuwaambia: "Enyi ndugu mmenipa nyinyi farasa, sasa vipi mnaniwekea jasusi wa kunidhibiti asiye na farasi tazameni sasa ninapokwenda mbio na farasi hawezi kunifikia mwishowe anahema na kuchoka sana, basi mtafutieni farasi ili aweze kufanya vyema kazi yake:. Katika mbinu nyingine Sultan Abdulhamid akamtafuta mwanamke mzuri kutoka katika jumuiya yake na kumtaka Jamaldin amuoe lakini jambo hilo halikufanikiwa na Jamaldin akamwambia: "Ewe Sultan unataka kunioza mwanamke ili nisiweze kufurukuta na kufikia lengo la mimi kuwapo katika ardhi. Dunia hii ni kubwa na nzuri, sina haja hata kutaka uchumba vipi nioe mwanamke". Baada ya kukataa hayo akaweka kizuizi baada ya miezi mitano siku ya Machi 9, 1897 saa 1:13 asubuhi akarejea kwa Mola wake aliyekuwepo wakati akikata roho anasema: "Siku ya Jumatatu asubuhi nilipokwenda kumuona nikamkuta akisema Lo! Lahaillah Lallahillhaulah Lailahaillah mara tatu akaisalimisha roho yake kwa Mola wake. Sultan Abdulhamid akaeneza kwamba Sheikh Jamaldin amekufa kutokana na ugonjwa kansa uliompata kwenye taya baada ya kung’oa jino ambalo lilipelekea kufanyiwa operesheni mara tatu, lakini habari za uhakika zinasema aliuawa kwa kupewa sumu, Sultan Abdulhamid khabari za kifo chake zisitangazwe katika ulimwengu wa Kiislamu, lakini habari zilifika kwa haraka na magazeti ya Misri, Syria, Sham na kwingineko yaakandika khabari hizo. Jeneza lake lilibebwa na mapolisi wanne pamoja na maofisa usalama akazikwa mahala paitwapo Nishantwash mahala wanapozikwa Maulamaa na Masheikh wakubwa. Huyo alikuwa Jamaldin Afghan kauli yake maarufu alikuwa akipenda kuisema kuiambia nafsi yake: "Ewe Daruwesh utakayeondoka duniani unaogopa nini, simama na fuata mambo yako wala usiogope kiongozi yeyote dhalimu. Itakuja siku moja siku hiyo ikiwa mbali na karibu mno, hakika maneno yangu ya kusimamisha dola tukufu ya Kiislamu yatafikia upeo wake. Siku hiyo nitasema nimejuzu kwa jina la Mola wa Arkaba". Kuhusu mambo ya madhehebu alisema: "Mimi ni mwamasishaji wa umma huu mtukufu kuelekea katika ushindi kwa kuwa nimetoka katika mifupa ya umma wa Kiislamu sina haja ya madhehebu". |
YALIYOMO
Tahariri Onyesheni ushujaa wa Badri Daniel kuwatimua waumini Msikitini Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu Dondoo za Kisakolojia
Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ Njia bora zitakazotusaidia kuwalea
watoto
Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni
I Arusha.
Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.)
Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata
Msikiti mpya
Huduma za maji Kondoa haziridhishi
Mnyororo wa imani
Je, Yesu alibatizwa?
Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa Sheikh Bafadhil ateuliwa
kudhamini waandishi wa habari Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|