|
|
|
BINAADAMU yuko katika ncha ya kujiangamiza yeye mwenyewe, kwa sababu amepoteza mambo muhimu ya ubinadamu wake, ambayo ni muhimu pia kwa maendeleo yake mazuri. Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, ubinadamu ni nini? Ubinadamu siyo kula na kunywa kama anavyoweza kufikiria mtu na wa akili za kawaida. Maana halisi ya ubinaadamu ni binaadamu kumjua Mwenyezi Mungu na nafasi yake katika dunia hii. Kinyume cha hivi dunia itaangamia kupoteza ubinaadamu ni hatari inayoshinda bomu la Atomic au bomu lolote lile liwayo. Watu walio wengi wanaitazama dunia ya Magharibi kama ni dunia yenye maendeleo makubwa. Lakini dunia ya Magharibi si lolote si chochote. Hali hii inatokana na sababu kuu ya kimsingi. Serikali mbalimbali ya nchi hizi zinakubali sasa kuwa zimeshindwa kabisa kuwafanya binaadamu au raia zao kuwa binadamu. Hakuna duniani nchi zinazofanya madhambi sawa na nchi za Magharibi sawa na madhambi ya kaumu ya Lutti kama katika nchi hizi. Hata serikali nyingi nyingine zimefikia hatua ya kuhalalisha madhambi haya na kuona kuwa ni mambo ya kawaida. Viongozi wa nchi hizi bado wanayo fikra kuwa madhambi haya chimbuko lake kubwa ni mipangilio mibaya ya uhuru. Wanajaribu kuazima baadhi ya fikra kutoka nchi za Mashariki ili kurekebisha uchumi wao. Lakini yote haya hayaonyeshi mafanikio yoyote. Nchi za Mashariki zilidhani kuwa fikra nzuri za kumjenga binadamu awe binadamu ni fikra za Max. Fikra za Max ziliandikwa na Mayahudi na mwenyewe Max alitumika kama chombo tu cha kufikiria hayo yaliyokusudiwa. Fikra za Max hazikuwa na matokeo yoyote mazuri kwa binadamu. Nguvu za serikali ndizo zilizokuwa zinatumika ubinadamu. Watu wengi walipoteza maisha yao na nchi hizo mpaka leo hazina mafanikio yoyote ya maadili wala ya kiuchumi. Kwa yote Umax umeshindwa kabisa katika ulimwengu wa fikra. Fikra hiyo inaweza kudumu katika utawala wa kiimla tu na jamii iliyoharibika; jamii isiyojua zuri wala baya; halali wala haramu; kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Mitume, Pepo, Moto na maisha baada ya kifo. Urusi ndiyo iliyokuwa baba na mlezi wa fikra hiyo. Mlezi huyu alijigamba kuwa ndiye mwenye nguvu na uongozi bora baada ya Marekani hapa duniani. Alifanikiwa kuambukiza fikra hiyo katika uongozi wa nchi za dunia ya tatu. Ebu tazama ukweli, Urusi na marafiki zake wameanguka mwereka wa mende. Hawana chakula cha kuwalisha watu wao wala fedha za kuendeshea serikali zao. Hawana jipya watakalofanya la kuwaokoa binadamu ambao hivi sasa wako katika mashaka makubwa. Upo ushahidi wa kutosha kuwa ulimwengu umekuwa unatawaliwa na kuendeshwa kwa urongo na itikadi potofu. Leo ulimwengu upo katika demokrasia na uchumi huria. Hizi zote ni fikra za Wagiriki, Warumi na kwa ujumla nchi za Magharibi. Fikra zote hizi hazifai kwani zinamwondoa binadamu kutoka katika ubinadamu wake. Sababu; hazitambui mipaka ya Mwenyezi Mungu; uhalali na uharamu wa mambo; na ndizo nchi zilizo na sera kuwa dini na siasa ni vitu viwili tofauti. Huu ni upotofu na ni maangamizo makubwa kwa ubinadamu. Inatosha kutamka kuwa zamu ya Uislamu na Waislamu walio safi kwa Mwenyezi Mungu umefika. Mwenyezi Mungu analithibitisha hili katika sura ya tatu, aya ya 110, kwa kusema: "Nyinyi ndiyo ummah bora kuliko ummah zote zilizodhihirishiwa watu ulimwenguni, mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu". Waislamu wakitenda kinyume cha aya hii, basi tutapoteza sifa ya kuwa ummah bora; hivyo kuwa makafiri moja kwa moja. Kinachotakiwa hivi sasa ni kujiepusha kabisa na makafiri, kwani makafiri hawana malengo mazuri kwetu. Qur’an tukufu ambao ndio mwongozo wetu sahihi unatufahamisha: "Enyi mlioamini! Mkiwatii baadhi ya wale waliyopewa kitabu, watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Uislamu wenu". (3:100). Uislamu ni lazima uonekane katika jamii kwani bila hivyo watu walio wengi wataupaka doa na hawawezi kuukubali kirahisi. Kama pia tunataka maisha yetu yote, kutoka utotoni mwetu hadi kifo chetu, ni lazima turudi katika Uislamu wa umbile la mwanzo. Tusiuchanganye na itikadi za utaifa na fikra za watu siyo miongoni mwa wana wa chuoni wetu. Na Mtume (s.a.w) ametuchagulia mambo mawili na tukifungamana nayo hatutapotea. Mambo mawili haya ni Qur’an na Sunnah zake. Qur’an na Sunnah za Mtume wetu zinawapa heshima binadamu, hivyo inatosha kusema Qur’an na Sunnah ndiyo ubinadamu. Marekani na Urusi hawawezi kumtayarisha wala kumfanya binadamu awe binadamu. Sababu sera zao zinao upungufu mkubwa wa ubinadamu. Uislamu ni kamilifu
na hauna upungufu wowote kinyume kabisa na madai ya hao hao. Tazama aya
ya 70, sura na 17 inayotufahamisha: " Na hakika tumewatukuza wanadamu na
tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri
na tumewatukuza kuliko wengi katika wale waliowaumba, kwa utukufu ulio
mkubwa (kabisa).
|
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|