|
|
|
KIKUNDI cha kina mama wa Kiislamu cha Bi Khadija cha mjini Dodoma kinatarajia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini. Bi Mwanahamisi Abdallah alimueleza mwandishi wa habari hizi kuwa mbali na kutoa msaada kwa wagonjwa, wataweka utaratibu wa kuwazungukia wagonjwa kuwafariji na kuwaombea dua. Hivyo, Bi Mwanahamisi amewaomba Waislamu wote wake kwa waume kushirikiana katika fikra hizi na kazi nzuri ambayo imeusiwa na Mtume (s.a.w.). Wakati huo huo, Imam wa Masjid Qubaa, Sheikh Abdallah Ally amewahusia Waislamu wa Dodoma na kwingneko kuwa wakarimu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa kufuturishana na kusaidiana. Sheikh Abdallah Ally amesema hayo katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani alipokuwa akiwahutubia mamia ya Waislamu waliohudhuria sala ya Ijuma. Sheikh Abdallah alisema tendo la kumfuturisha mtu aliyefunga lina ujira mkubwa sana mbele ya Allah (s.w.) na tendo hilo kila Muislamu analiweza kulifanya kadri ya uwezo alionao kwani alisema hata kumpa glasi ya maji au tende moja inatosha kupata ujira usiokadirika mbele ya Allah (s.w.). Aidha, Sheikh Abdallah amewahusia Waislamu kukithirisha sana kusoma Qur’an na kukhitimisha Qur’an nzima (juzuu 30) na wale ambao hawana kiwango kikubwa cha elimu inawatosha kusoma sehemu yoyote ya Qur’an anayo ifahamu kila mara, na kila siku. Nao waumini wa Masjid Qubaa wamechanga jumla ya shilingi 19,720 kwa wanafunzi wa Bihawana kama gharama za kununua futari na daku kwa wanafunzi 14 wa Kiislamu wa kidato cha nne ambao wapo shuleni wakisubiri kufanya mitihani yao. WAISLAMU wa kijiji cha Hamai, tarafa ya Goima wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma wamefikia kutoa wito kwa ndugu zao wa Kiislamu kuomba msaada wa hali na mali kumalizia jengo la Masjid Bilal na madrasa. Akitoa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Sheikh Ally Hassan Matundu amesema kuwa hatua waliyofikia inahitajika nguvu ya pamoja na Waislamu wengine waliyopo ndani na nje ya mkoa wa Dodoma ili kuweza kukamilisha awamu hiyo ya mwisho ya ujenzi. Mwandishi wa habari hizi alikutana na kamati kuu ya ujenzi na kuweza kupata kiini cha hali iliyofikia kuomba msaada huo. Mratibu wa ujenzi na shughuli za Da’awa Ustadh Rashid Salim Futa alisema, uchumi kwa kipindi hiki umekuwa mgumu sana hapo kijijini. Pamoja na kuwa asilimia 99.5 ya wakazi wa Hamai ni Waislamu, lakini hali ya njaa iliyoikumba wilaya ya Kondoa ikiwemo na kijiji cha Hamai imesababisha watu kujishughulisha na utafutaji wa riziki kwa familia zao. Aidha, Ustadh Futa alisema pia kuwa suala la kujenga Msikiti ni la kheri, hivyo Waislamu wa Hamai wangependa nao washirikishe ndugu zao kupata thawabu hizo. Jumla ya vifaa vifuatavyo vinahitajika kumalizia jengo hilo kama vile saruji tani 10, madirisha 11, mazulia, generator, rangi, dali (ceiling board) na vipaza sauti. Kwa upande wa Madrasati Bilal ambayo ujenzi wake umeunganishwa na Msikiti, wanahitaji vitabu, na mihutasari (syllabus). |
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|