|
|
lee mapema wiki ijayo. Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata, Rais pamoja na mambo mengine huenda akazungumzia malalamiko mbalimbali ambayo Waislamu wamekuwa wakiyatoa dhidi ya serikali yake. Utaratibu wa viongozi wa serikali kuhudhuria hafla za kidini ni wa kawaida hapa nchini ambapo katika awamu mbili za mwanzo viongozi wa kitaifa walitumia fursa hizo kujenga mahusiano ya karibu na waumini wa dini mbalimbali. Miaka ya mwanzo baada ya nchi kupata uhuru, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akihudhuria hafla mbalimbali za waumini ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya Idd ambapo kumbukumbu zinaonyesha kwamba mwaka 1970 alihudhuria Baraza la Idd el Fitr katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika Baraza hilo Masheikh walimtakia Mwalimu Nyerere maisha marefu ili kumwezesha kuiongoza Tanzania na hatimaye kufikia lengo la Taifa la kujenga ujamaa. Katika awamu ya pili utaratibu huo uliendelezwa na kustawishwa zaidi ambapo Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alihudhuria hafla hizo ikiwa ni pamoja na kufungua Misikiti na Makanisa sehemu mbalimbali nchini. Katika hotuba zake kwenye hafla hizo, Mzee Mwinyi alikuwa akijibu maombi, madai, malalamiko na tuhuma mbalimbali za wananchi dhidi ya utendaji wa serikali yake. Jumatano ya wiki iliyopita Mh. Rais Benjamin William Mkapa alikutana na Masheikh wa Dar es Salaam ambapo alipokea malalamiko na maoni ya Waislamu juu ya mambo kadhaa. Taarifa zimeeleza kuwa baadhi ya mambo Mh. Rais aliahidi kuyashughulikia mara moja ambapo mengine yaliahirishwa kutafutiwa muda muafaka wa mazungumzo zaidi. Mh. Rais alikutana na Masheikh hao Ikulu alipoandaa futari kwa ajili yao kama ilivyo ada yake kila mwaka. Sheikh mmoja aliyehudhuria futari hiyo ambayo baadhi ya watu wameibatiza na kuiita "ya nguvu" ameliambia ANNUUR kwamba tofauti na miaka ya nyumba futari ya mwaka huu imekuwa na tija kubwa. Kwanza amedai imewahusisha Waislamu toka taasisi mbalimbali, jambo ambalo limeondosha hisia kwamba wapo Waislamu wa taasisi fulani tu wanaotambuliwa na serikali. Pili amesema kwamba zaidi ya futari ilipatikana fursa ya kuongea na Mh. Rais juu ya masuala mazito yanayowagusa Waislamu ambayo Mh. Rais aliahidi kuyashughulikia. Hata hivyo, Sheikh huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini hakufafanua ni masuala gani yalizungumzwa na tija inayotarajiwa. Naye Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma amekuwa akiandaa futari kwa makundi ya Waislamu toka Jumuiya na Taasisi mbalimbali ambapo pia ilipatikana fursa ya kupeana nasaha. Katika moja ya nasaha zake, Mh. Dk. Omar alihimiza suala la umoja miongoni
mwa Waislamu.
|
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|