|
|
| Ubungo
Yakumbwa na ukame
WAKATI Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Jijini (DAWASA) ikiwahakikishia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam juu ya kuwepo maji ya kutosha, wakazi wa maeneo ya Ubungo kwa muda wa mwezi sasa wamekumbwa na ukame mkubwa. Ukosefu mkubwa wa maji umejitokeza zaidi Ubungo Kibangu ambako wananchi wamekuwa wakihangaika huku na kule kusaka maji. Maji yaliyokuwa yakipatikana kwa mgao siku tatu kwa juma, hivi sasa hayapatikani tena ambapo wananchi hulazimika kutumiakj visima vilivyochimbwa baadhi ya maeneo. Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia akina mama kadhaa wakihangaika saa saba za usiku kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamelalamika kuwa huenda ukosefu huo wa maji unasababishwa kwa makusudi na baadhi ya wahusika. Wamedai kuwa hawaoni sababu ya msingi kwa eneo lao kukosa maji wakati wenzao wa maeneo ya Mabibo na Manzese hawana tatizo kama hilo ilhali bomba wanalotumia ni hilo hilo moja ambalo huingiza maji jijini toka mto Ruvu. Bwana Alawi mmoja wa wakazi wa eneo hilo alimdokeza mwandishi wa habari hizi kuwa bomba wanalotumia hilo ndilo hilo linalopeleka maji maeneo ya katikati ya jiji ambako hakuna shida hiyo. Aidha alisema wakati wao wako katika ukame, kiwanda cha pombe cha Kibuku
kilichopo kando ya bara bara ya Morogoro kimeendelea kupika pombe kwa wingi
kwa kutumia maji yanayosambazwa na bomba hilo.
Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema
Habari kutoka Arusha zimeeleza kwamba wiki iliyopita takriban Masheikh, wazee maarufu na Maustadhi wote mjini hapo walikusanyika kula chakula kilichoandaliwa na Bw. Felix Mrema kwa lengo la kuwafuturisha waungwana hao. Katika hali isiyo ya kawaida, inasemekana kwamba magari kadhaa yaliyokodiwa yalikuwa yakipita katika maeneo ya Misikiti kuwachukua waumini waliopata mwaliko. Baadhi ya waumini wamedai kuwa walihudhuria futari hiyo kwa kughilibiwa na Masheikh wao. Wamedai kwamba Masheikh hao waliwaambia kwamba Bw. Felix Mrema yu karibu kusilimu na hivyo kwenda kufuturu kwake ni kumpa nguvu. Waumini wamekuwa wakiwahoji Masheikh na Maustadh waliohudhuria futari hiyo kuelezea uhalali wa futari hiyo. Suala hilo limekuwa likiulizwa kwa kuzingatia kwamba muandaaji sio Muislamu. Baadhi ya waumini wamedai kwamba futari hiyo ni ishara ya kuanza kwa msimu wa tenda kwani 2000 inakaribia. Miongoni mwa Masheikh wenye heshima zao ambao walikataa kuhudhuria futari hiyo ni pamoja na Sheikh Mohamed Ahmad Anzuwan na Maustadh wa Msikiti wa Kijenge. Mialiko ya futari inakuja wiki moja tu baada ya gazeti moja la kidini kuripoti Sheikh aliyeshutumu tabia iliyoota mizizi miongoni mwa Waislamu ya kuhamanika na kula. Baadhi ya watu waliohojiwa na gazeti kuhusiana na hali hiyo, wamedai kuwa ni makosa kuwalaumu Masheikh kuitikia mialiko hiyo kwani ni kawaida kwa kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani kukirimiana. Hata hivyo, wamekuwa na wasiwasi na uhalali wa kuitikia mialiko ya wasio Waislamu na viongozi wa siasa. |
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|