AN-NUUR 
Na.184 Ramadhan 1419, Januari 15 - 21, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waislamu turejee kwa Allah

NINAJIKINGA kwa Allah dhidi ya (shari) ya shetani. Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Huruma. Sifa Njema zote ni stahiki Yake Allah na ninamtakia Rahma na Amani Zake (Allah) mja Wake Muhammad bin Abdullah pamoja na jamaa zake, masahaba zake na wale wenye kuufuata mwenendo wake mpaka siku ya Hukumu. 

Enyi vijana wa Kiislamu, enyi walinzi wa Uislamu, Dini hii ya Allah ipo katika hatari ya kuangamizwa (hatari) inayotokana na viongozi madhalimu na vibaraka wa tawala za kikafiri. Viongozi hao wanasaini mikataba inayopelekea kuufuta Uislamu katika nyoyo zenu, kuupokonya Uislamu toka katika mikono yenu na kukishusha hadhi Kitabu cha Allah (Qur’an) na kubaki kuwa ni (kitu cha) pambo tu na (kuwa ni kitu cha) kusomwa katika mikusanyiko tu (badalaya kuwa ndio mwongozo kwa Waislamu na wanaadamu wote kwa ujumla). 

Enyi ndugu zangu, Jiokoeni kwa kumcha Allah ipasavyo, na fanyeni juhudi zenu zote kutafuta radhi za Allah. Hii ndiyo namna (pekee) ya kuleta utukufu katika Ummah wa Waislamu. 

Enyi Ummah wa Waislamu, Shikamaneni sawasawa na maneno ya Allah (katika Qur’an Tukufu) na Sunnah ya Mtume Muhammad (s.a.w.). Ving’ang’anieni viwili hivi (Qur’an na Sunnah) na vitumieni kupambana na shetani na wafuasi wake, na ufanyeni mwenendo wenu kuwa kama mwenendo wa masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.). Allah anasema katika Qur’an Tukufu: (Al-Shuura 42:46, 47, 48). 

Enyi Waislamu, Maamrisho ya Allah ni mengi, na kabla sijaanza ninapenda kusema kuwa ninapingana na yale aliyoyasema Khatibu wa Ijumaa katika Msikiti huu leo. Amelinganisha hali ilivyokuwa wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.) na uvamizi wa Israel (katika ardhi ya Waarabu) pale alipoulinganisha uvamizi huo (wa Israel) na uamuzi wa Mtume Muhammad (s.a.w.) alipowasamehe Maqureish (watu wa kabila la Mtume) kutokana na maovu yao baada ya (Mtume Muhammad (s.a.w.) kuitwa Makkah. Kwa kweli hii sio kauli ngeni kutoka kwa huyu Khatibu wa leo hii ambaye ni Katibu wa Al-Awqaf ambayo ni Wizara ya Masuala ya Dini katika serikali ya kisaliti ya Palestina. Hawa ndio wale waliojitokeza kuibusu mikono na miguu ya Bw. Clinton wakati Rais huyo alipoitembelea Gaza hivi karibuni. (Khatibu) huyu ni kiongozi wa wanafiki. Ninaikana hotuba yake hiyo ya leo! 

Mapambano kati ya haki na batili, (mapambano) kati ya halali na haramu ni moja kati ya kanuni za Allah katika ardhi hii ili Allah apate kutenganisha haki na batili, na kuziweka batili pamoja. Ni kanuni pia ya Allah kuiwezesha haki kushinda baada ya hayo, kuwa (Allah) apate kuithibitisha Haki na kuubainisha upotevu ingawa madhalimu watachukia. (Hawa) ni sawa na wale walioiuza Palestina kwa Wayahudi na wanaendelea kutaka kuiuza kwa Wayahudi sehemu ya ardhi iliyobaki. Jambo hili si la ajabu kwa vile baada ya kuiuza (kuitelekeza) dini yao (Uislamu) haiwi ajabu kwao kuiuza ardhi yao wenyewe kwa maadui zao. Tunaimani kuwa wakati sasa umefika kwa Haki (Uislamu) kutawala tena; Allah anasema katika (Al-Hujj 22:40). 

Enyi Waislamu, Lazima mfanye juhudi kuziokoa nafsi zenu kutokana na maangamizi kwa kujitahidi kurejesha imani juu ya (kuyakubali na kuyafuata) mafundisho ya Uislamu na Sheria za Allah (s.a.w.). Makafiri na wanafiki wanapigana kuuzuia Ukhalifa usirudi. Allah anaeleza juu yetu kuwa (Qur’an 3:110) hivyo basi jiokoeni nafsi zenu kutokana na maangamizi ambayo yatatokea ikiwa (mtaendelea) kufuata dhana za kikafiri kama vile demokrasia, kutafuta ‘muafaka’ wa dini (mbalimbali) na kumnyenyekea Clinton. 

Enyi Waislamu, Amsheni hamasa katika nafsi zenu, boresheni imani juu ya Allah na zikumbukeni ahadi zenu kwa Allah (s.w.) kuwa hamtaikubali dini (nyingine) yoyote isipokuwa Uislamu na hamtafuata utamaduni wowote isipokuwa utamaduni wa Kiislamu. Ndiyo sababu inatupasa kufanya juhudi kuihuisha amana hii (ya kuukubali kuufuata Uislamu tu) katika Ummah wetu, na inatubidi tufanye juhudi kuanzisha mapambano ya kisiasa dhidi ya makafiri, wanafiki na viongozi (wasio waadilifu) wa Ummah huu. Ni lazima tupambane kwa ajili ya imani yetu ya Kiislamu. 

Enyi watu, enyi vijana wa Kiislamu, Ukhalifa kati ya Uislamu unawaunganisha Waislamu wote na (wala) sio mabunge ya Kiarabu tu; unailinda ardhi yote ya Waislamu, ndio ambao huendesha jihadi ya kuuneza Uislamu ulimwenguni kote; na ndio ambao huufanya Ummah wa Waislamu kuwa ni wenye nguvu kiasi cha kusikika na kuheshimika katika medani za kimataifa. Ni dola hii ndiyo inayoulinda Ummah usiharibiwe. (Lakini) hawa Makhatibu wa Misikiti walioteuliwa (na serikali) na hawa viongozi wasio waadilifu katika ulimwengu wetu wa Waislamu (kamwe) hawataunusuru Ummah huu. 

Enyi Waislamu, (Hebu) sasa isikilizeni Hadith ya Mtume Muhammad (s.a.w.) iliyosimuliwa katika Bukhari na Muslim yenye kuzungumzia hazina ya mafuta ambayo ni stahiki ya Waislamu na sio ukoo wa (mfalme) Sabbah (huko Kuwait) au ukoo wa Saud (huko Saudi Arabia) na mawakala wa Kiarabu. Hadithi hii inaizungumzia hazina hii ya Ummah wa Waislamu ambayo ndiyo sababu ya mashambulizi dhidi ya ardhi ya Waislamu. Mtume Muhammad (s.a.w.) amesema katika hadithi hii, "jambo ninalolihofia zaidi kuliko yote (kwenu) ni hii hazina itokayo ardhini", kisha masahaba wakamuuliza: "Ee Mtume wa Allah ni nini hiyo?". Mtume (s.a.w.) akajibu: "Ni ula la maisha", kisha masahaba wakamuuliza tena: "Hivi inawezakana vitu vizuri vikaambatana na mambo mabaya (ikimaanisha mafuta na hazina nyingine toka ardhini ni vitu vizuri sasa ni vipi vilete mambo mabaya!) Mtume alikaa kimya kwa kitambo kirefu na kisha akasema: "Vitu vizuri vitaleta mambo mazuri tu lakini yule anayepinga vitu hivyo ataleta mambo mabaya. 

Hivyo, viongozi wenu wakiwataka kufanya uhaini, kuwapiga vita ndugu zenu (Waislamu), kuukumbatia "Usekula (Secularism)" badala ya Uislamu, basi mambo mabaya hutokea. (Hebu) tazameni ni jinsi gani viongozi wenu wanakutakeni kuiachia Palestina ichukuliwe na Wayahudi. Walikutakeni kuuachia mji wa Asqalan. Mjii huu ulivamiwa mwaka 1948 ambapo Israel ilianza kuutawala. 

Mafuta ni bidhaa ya thamani lakini watu wa Ghuba hawayatumii mapato yatokanayo na mafuta kwa mujibu wa maamrisho ya Allah; wanatumia mamilioni kwa mamilioni kwa (kucheza) kamari na mambo (mengine) yasiyo ya halali; hawayatumii mapato hayo kuwalisha ndugu zao (wenye njaa) au kuikomboa ardhi ya Waislamu; hivyo hazina hii imewaleta madhila matupu, vita na mauaji. Na katika Hadithi (nyingine) ya Mtume Muhammad (s.a.w.) kuhusu Iraq, Mtume (s.a.w.) alisema: "Itafika siku watu wa Iraq watakuwa katika adha kubwa na hakuna atakayeweza kuwasaidia". Kisha masahaba wakamuuliza, "kutoka kwa nani?" Mtume Muhammad (s.a.w.) akajibu; "Kutoka kwa Wayunani (nchi za Magharibi). Lakini atatokea Khalifa mwisho wa kipindi hiki ambaye kiasi kikubwa cha pesa kisichokuwa na idadi. Tunataraji kuwa Khalifa huyu atakuja baada ya madhila na maovu yaliyotuzinga hivi leo, Khalifa huyu atakuja kutawala baada ya hawa viongozi wasio waadilifu. 

Tunamuomba Allah aharakishe kurudi kwa huyo Khalifa (kuifanya dini hii (Uislamu) itawale kila nyanja ya maisha, kuueneza Uislamu ulimwengu mzima, kuwaunganisha Waislamu kuwa kitu kimoja (ulimwenguni kote), na kuikomboa Al-Aqasa na maeneo mengine yote ya Waislamu yaliyovamiwa. Amina. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa 

Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd 

Ubungo yakumbwa na ukame 

Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema 

Dondoo za saikolojia 
Na. Abu Halima Sa Changwa 

Waislamu turejee kwa Allah 

MSADAT yazidi kutia moyo Tanga 

Mjue Usama bin Ladin 

MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI 

Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu 

Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii 

Hakuna Magharibi wala Mashariki: Uislamu ni ubinaadamu 
Na Abubakari S. Marwillo 

Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma mjini 
Na Abu Zuberi, Dodoma 

Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat - Tabata Kimanga 
Na B. Mwakangwale 

Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui 

Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana 

Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake 

Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma 

Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti 

Mnyororo wa imani-2 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Kutoka magazeti ya zamani: 
Wanaoshitakiwa kwa uhaini kortini leo 

Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa Kanisa la Walokole 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Masjid Nurania yaswaliwa Ijumaa 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Jabal Hira kutoa mafunzo ya Kompyuta Morogoro 
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Internet ni nini?] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Thamani ya mlo wa Uyoga] 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita