|
|
| Historia:
Form IV
Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Tatu Uthman bin Affan Hadi mwishoni mwa mwaka 26 A.H. mpaka wa Dola ya Kiislamu uliishia milima ya Caucasus (ambayo sasa iko chini ya Urusi). Hizi ndizo fujo za Warumi wakati wa ukhalifa wa Uthman. Ama Wapeshia nao, pamoja na kushindwa vibaya wakati wa ukhalifa wa Al-Faruq Umar bado mfalme Yedzgird aliyekimbilia Balk (sehemu katika Afghanistan) alichochea upinzani mpakani mwa Dola ya Kiislamu na Afghanistan. Khalifa Uthman alimtuma ubaidullah bin Mamar kuzima upinzani huu lakini aliuawa na mahali pake akateuliwa abdallah bin Amir gavana mpya wa Basra kuzima uasi. Amir aliwashinda waasi na kuteka sehemu kadhaa kama vile Hisraf, Gazna, Herat na Kabul. Vile vile aliiteka miji ya Balkh (Afghanistan) na Samarkand, Tashkent, Sajestan, Arghiyan na Turkmenistan Vurugu za wapeshia katika ukhalifa wa uthman zilikwisha baada ya kifo cha mfalme Yedzgird mwaka 31 A.H. alipokusanya jeshi akiwa turkmenistan na kupigana na Waislamu chini ya kamanda Abdullah bin Amir mahali paitwapo Sistan ambapo Yedzgird alishindwa na kutoroka. alipokuwa anakwenda alikoalikwa na mmoja wa watemi wa Kituruki, aliuawa usiku katika kijiji kimoja hata kabla ya kufika alikokusudia kwenda. Vita hivi pia vilipelekea kutekwa kwa Khurasan na Tabrastan. Upinzani kutoka miongoni mwa Waislamu Ukhalifa wa uthman ulichukua miaka 12. Katika miaka sita ya kwanza dola ya Kiislamu iliimarika na mipaka yake kupanuka kama ilivyokwisha elezwa. Katika miaka sita aliyomalizia ukhalifa wake kulikuwa hakuna utulivu, kulizuka miongoni mwa Waislamu malalamiko ya uongo dhidi ya Khalifa na serikali yake. Kiongozi wa kundi hili la wapinzani ni Abdullah Ibn Sanda alijulikana sana kwa jina la Ibn Sanda au Ibn Saba. Ibn Sanda alikuwa Myahudi anaetoka Yemen, alisilimu kinafiq kama alivyosilimu Abdallah bin Ubaidah lakini ibn Saba tangu aliposilimu alikuwa tayari na mpango wake wa kuudhuru uislamu hatua kwa hatua, kundi la wanafiqi hawa lililoongozwa na Ibn Saba lilitumia shutuma dhidi ya Khalifa na serikali yake kuficha unafiq wao kwa sababu madai yao yalikuwa ni ya uongo na pale walipopewa maelezo ya kweli waliyafumbia macho na hawakuyakubali. Tutaonyesha unafiq wao huo katika mbeya mbili; kwanza tutaonyesha udhaifu wa madai yao yaliyozusha uasi na hatimaye kumuua Khalifa na pili, vitendo vyao vilivyokuwa dhidi ya uislamu hivyo kudhihirisha unafiq wao. Sababu zilizowapelekea kuzusha uasi na hatimaye kumuua Khalifa uthman ni kama zifuatazo. Wasabai hawa walidai kuwa Khalifa anapendelea ndugu zake katika kugawa kazi za ngazi za juu kama ugavana. Dai hili halikuwa ukweli wowote. Ni kweli Muawiya ni ndugu wa karibu kwa Uthman, lakini Amir aliteuliwa kuwa Gavana wa Syria tangu wakati wa umar. Halikadhalika Sa’ad aliyeiteka persia aliteuliwa wakati wa umar. Kutokana na malalamiko kdigo dhidi yake aliondolewa kwenye ukhalifa na Umar na nafasi yake ikashikwa na Mughira lakini Umar alidhamiria kumrudishia wadhifa wake Sa’ad. lakini kulizuka kutoelewana baina ya Gavana na Ibn Masud mkusanyaji kodi wa Kufa - Sa’ad akaondolewa na nafasi yake ikajazwa na Walid bin Aqaba. Walid alikuwa ndugu wa karibu wa Uthman, lakini alieteuliwa mwanzoni mwa ukhalifa wake kabla ya tuhuma hizi. Hata hivyo Walid alipopatikana na hatia ya kunywa pombe aliadhibiwa kwa mujibu wa sheria na kuvuliwa ugavana, kama angemteua kwa udugu tu Khalifa angeweza kunyamazia jambo hili. Baada ya Walid Sa’ad bin As aliteuliwa kuwa Gavana wa Kufa lakini wapinzani wa kufa chini yake walipata mafanikio makubwa hivyo akateuliwa Abu Musa Ashari mwaka 34 A.H. ambae hakuwa uhusiano wa damu kabisa na Uthman. Abu Musa alikuwa Gavana wa Basra na malalamiko ya upendeleo yalimfanya aondolewe na mahali pake akawekwa Gavana aliyeteuliwa na wapinzani. Madai dhidi ya Khalifa Uthman Upinzani mkubwa ulitokea Misri ambapo Abdallah bin Sa’ad alieteuliwa badala ya amri bin As. Abdallah hapana shaka ni ndugu wa Uthman lakini mchango wake katika Uislamu ulikuwa mkubwa sana. Ndiye aliyeanzisha jeshi la majini la Dola ya Kiislamu na ushindi wake Afrika ya kaskazini. ushindi huu umeonyesha kuwa Abdallah bin Sa’ad ana uwezo wa kuongoza hivyo Khalifa alikuwa sahihi kumpa ugavana na hapana upendeleo hapa. Hata hivyo wanafiki hawa alipovamia Madina na kudai kuwa hawamtaki Gavana Sa’d; Khalifa alimbadilisha na kumuweka mtu wanaemtaka Muhammad bin Abu Bakr. Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kuwa Khalifa Uthman hakuwa na upendeleo kwa ndugu zake kwa kuwapa nafasi za ugavana. Kama angekuwa nao ni dhahiri asinge waachisha kazi na pale walipokosea kuwachapa. Isitoshe magavana hawa waliteuliwa mwanzoni mwa ukhalifa wake wakati akipendwa kama Khalifa umar. Ni kweli Uthman aliwavua madaraka baadhi ya magavana kama alivyofanya umar kwa manufaa ya uislamu. Dai lingine lililopikwa na wanafiki wa kundi la Saba ni matumizi mabaya ya pesa za Serikali (Baitul mal). Amesingiziwa kuwa anatumia vibaya pesa za serikali na kuwapa ndugu zake. Dai hili silo la kweli kabisa kwa sababu zifuatazo: Uthman alikuwa tajiri mkubwa Arabia hata akaitwa "Ghanir I" (mtu tajiri). Lakini hakuwa tajiri tu lakini anajulikana kwa mchango wake katika njia ya uislamu wakati wa Mtume (s.a.w.) na baada ya Mtume (s.a.w.) wema wake uliendelea katika Ukhalifa wake. alitumia mali yake mwenyewe kusaidia maskini na ndugu zake. Katika ukhalifa wake kwa muda wote wa miaka 12 hakuchukua posho kwa ajili ya ukhalifa wake kutoka kwenye Baitul Mal. Kulikuwa na zogo kubwa wakati Khalifa alipotamka kumpa zawadi Abi Sarh 1/5 ya ngawira ya Afrika ya kaskazini kwa kazi nzito aliyoifanya ya kuteka Afrika kaskazini kama motisha. Jambo hili lilipolalamikiwa na watu, Khalifa alimtaka Sarh arudishe ile ngawira na akafanya hivyo. Vile vile ikasemwa kuwa amemruhusu mpwae Marwan anunue kasma ya serikali ya mateka. Jamb |
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|