AN-NUUR 
Na.185 Shawwal 1419, Januari 29 - Februari 4 , 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa
 

WAISLAMU Jijini wamekamata mali ya Wakfu iliyoachwa na marehemu Hajat Aziza Omar ambayo iliporwa kwa njia za udanganyifu na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Zakaria (Mkristo) miaka sita iliyopita. 

Mali hiyo ambayo ni nyumba Na. 58 iliyopo Mtaa wa Somali Gerezani Jijini Dar es Salaam, ilirejeshwa kwa Waislamu baada ya Khitma na Dua iliyosomwa mahali hapo Jumapili iliyopita. 

ANNUUR ilishuhudia umati wa vijana kwa wazee uliohudhuria dua hiyo ambapo mwishoni mwa 

hafla hiyo Waislamu hao waliingia ndani ya nyumba hiyo na kuanza kuitwaharisha ambamo walikuta maboksi kadhaa ya kondomu na chupa za konyagi zilizoashiria nyumba hiyo ilivyogeuzwa Danguro . 

Akitoa historia fupi ya nyumba hiyo ya Wakfu, mhadhiri wa hafla hiyo kwa niaba ya waliohudhuria hapo, alisema kwamba kabla ya kifo cha mmiliki wa nyumba hiyo Hajat Aziza uliandikwa wasia ambao ulithibitishwa na mahakama ya Kariakoo kwamba nyumba hiyo imetolewa Wakfu kwa Waislamu na Masjid Mwinyi uwe mdhamini wake. 

Baada ya kufariki dunia Hajat huyo mwezi Mei 1991 miezi minne baadaye (Septemba 13, 1991) wadhamini walitoa tangazo la mirathi katika gazeti la Uhuru lililokuwa gazeti pekee la kila siku wakati huo kwa lugha ya Kiswahili. 

Mhadhiri huyo aliendelea kueleza kuwa tangazo hilo halikupingwa na yeyote mpaka siku 90 kisheria zilipokwisha. 

"Daniel alianza utapeli wake kwa kutoa tangazo la mirathi kwenye "Government Gazette" ambalo halisomwi na watu wa kawaida; hapa ndipo alipoanza udanganyifu wake", alisema mhadhiri huyo. 

Ilielezwa kuwa baada ya tangazo hilo alipeleka "madai" yake mbele ya Mahakama ya Kisutu ambako alifanikiwa kuidanganya mahakama na kupewa haki ya kurithi nyumba hiyo. 

ANNUUR imefahamishwa kuwa Daniel alishirikiana na mtu mwingine anayeitwa Pius Kipengule waliweza kuwazunguka wasimamizi wa Masjid Mwinyi na kufanikiwa kupora nyumba tangu wakati huo ambapo waliigeuza na kuwa baa hali ambayo iliwakasirisha hata majirani walio karibu na nyumba hiyo. 

Mama mmoja ambaye hujishughulisha na biashara ya mama ntilie mtaani hapo aliliambia gazeti hili kuwa alikuwa akiona uchungu jinsi uovu ulivyokuwa ukiendelea nyumba hiyo wakati alimfahamu mwenyewe marehemu Hajat Aziza kwa ucha Mungu wake. 

"Kila mwaka mfungo sita alikuwa akisoma ziara (Maulid Nabi) watu walikuwa wakijaa mtaa huu mzima", mama huyo alimweleza mwandishi wa habari hizi. 

Aidha, alisema ameshangazwa na jinsi Daniel ambaye ni Mkristo alivyovamia nyumba hiyo na kurithi wakati Bibi huyo alikuwa Muislamu na hakuwa na mtoto wala ndugu wa nasaba. 

"Nimezaliwa mimi hapa mtaani mpaka napata akili namkuta bibi akiwa peke yake na nyumba yake alikuwa akiita Wakfu", ameeleza mama huyo anayekisiwa kuwa na umri wa miaka isiyopungua 45. 

Alimtuhumu Bi. mkubwa mmoja Mkristo mtaani hapo kwamba huenda alikuwa akishirikiana na "waporaji" hao. 

Aliyekuwa mjumbe wa nyumba kumi wa mtaa huo Bwana Haruna Said Muchunguzi ambaye hivi sasa anaishi maeneo ya Kigogo akieleza kwa mwandishi njama za Daniel kupora nyumba hiyo, alisema yeye alimsaidia marehemu pale alipoibiwa nyaraka zake za nyumba. 

Bwana Muchunguzi ambaye alikuwa mfanyakazi wa Bandari wakati huo, amesema baada ya wizi huo wa nyaraka kutokea walipiga ripoti kituo cha polisi Msimbazi na kumtaja waliyemtuhumu (Daniel Zakaria). 

Ameeleza Bwana Muchunguzi kuwa polisi Msimbazi ilitoa hati ya kukamatwa (RB) Bw. Daniel ambaye alikimbia tangu wakati huo hadi alipofariki bi kizee huyo ambapo aliibuka na kudai nyumba hiyo ni yake. 

"Alifukuza wapangaji wote, majirani wote waliojitokeza kumpinga aliwaweka ndani (polisi), mimi na Bwana Semvua tu ndio hakuweza", ameeleza Bwana Muchunguzi alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa ANNUUR nyumbani kwake Kigogo jioni ya Jumanne wiki hii. 

Aidha, Bwana Muchunguzi amesema suala la nyumba za Hajat Aziza Omar walilifikisha kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye amesema walimkabidhi baadhi ya nyaraka za nyumba za bibi huyo. 

ANNUUR ilijaribu mara kadhaa katika kipindi cha wiki moja iliyopita kuwasiliana na Bwana Daniel kuhusiana na mkasa huu hata hvyo katika hali ya kutatanisha haikuweza kumpata katika maeneo anakopatikana. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Kama hakuna haki watu watachukua sheria mkononi 

Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa 

Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 

Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa 

Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel 

Sheikh awasambaratisha walevi Liwale 

Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha 

Mjue Usama bin Ladin -2 

Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa 

Njaa hakuna, tunategemea kula silaha 

Parole kwa mbinde! 

Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil 

Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha 

Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR 

I.P.C yatakiwa kujitangaza 

Kutoka magazeti ya zamani 

Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa 
Na Muhibu Said 

Waislamu wachoma moto nguruwe 

Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa 

Waislamu Msonge waomba wanusuriwe 

Sayansi na Teknolojia 
[PELEKA FAX NCHI ZA NG’AMBO BURE! – (2)] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na Lishe 
[Mwongozo wa mlo wa kila siku] 
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita