|
|
|
Malalamiko mengine yaliyotolewa na wanafiki wale ni kuswali swala kamili bila kupunguza katika Hija, kupiga mahema Minna na kutoza Zaka ngamia - mambo ambayo wakati wa mtume (s.a.w.) wala Abubakr na umar hayakufanywa. Kuhusu kutopunguza swala Khalifa alipoulizwa alisema nimefanya hivyo ili wakazi wa maeneo hayo wasidhanie kuwa kupunguza swala ndio utaratibu.80 Ama kuhusu mahema ni suala la maendeleo na kwa watu wa leo ni jambo halina msingi kabisa. Kwa vile mahema na nyumba za kitalii zinatumika sio Mna tu bali hata Makka. Ama kuhusu farasi kutozwa au kutotozwa Zaka wakati wa Mtume na makhalifa wawili wa mwanzo yaweza kuwa uchache wao na kushiriki kwao kwenye vita. Wakati wa Khalifa uthman na baada ya mfululizo wa vita hali ya uchumi ya Waarabu ilibadilika na Khalifa aliona ni Busara Zaka pia itolewe kwa farasi kama ilivyo kwa ngamia.81 Sababu hasa ya chanzo cha ghasia hatimae kumuua Khalifa Uthman hazikuanza wakati wa uthman bali zilianza wakati wa Mtume (s.a.w.). Maadui wa Uislamu wakati wa Mtume walikuwa maqureish, Waarabu, Wayahudi, Wapersia na Wakristu wa Kirumi. Baada ya kutekwa Makka koo na makabila mengi yalisilimu, lakini walisilimu kwa nia mbali mbali ambapo hapa hatutazitaja. Linalothibitisha hili ni kule kuukana Uislamu kulikotokea mara baada ya kufa Mtume, uasi ambao uliikumba karibu Arabia yote. Wapinzani hawa walishindwa nguvu wakati wa Abubakr halikadhalika wakati wa Umar. Lakini haiyumkini kuwa walikuwa wameridhika na ustawi wa uislamu. Kwa hiyo hili ni kundi moja ambalo miongoni mwao walitokea wapinzani. Kundi la pili la wapinzani linatoka kwa wanafiki ambao njama yao ya kumuua Mtume ilitajwa kwenye Qur’an na hila zao kubainishwa mwaka wa 9 wa Hijria na hiki kilikuwa kipigo kikubwa kwao. Kubadilika kwa sera ya kuwataja wanafiki bayana na Mtume kukatazwa kuwaombea na kuwazika na kutotambulika katika jamii ya Waislamu kulistawisha chuki dhidi ya viongozi wa Waislamu. Kifo cha Mtume kiliwagawa Waislamu katika makundi matatu. Ukoo wa Mtume(Ahlul Bayt), Muhajirin na Answar. Pamoja na kuwekwa sawa hali hii wapo walioendeleza vikundi vyao moyoni na pale upinzani ulipochukua umbo la kuonyesha makosa serikalini. Bado lilikuwepo tatizo la mtu binafsi. Wapo Waislamu waliojiingiza katika upinzani kwa maslahi yao binafsi. Mfano mzuri ni Muhammad bin Abu Bakr na Muhammad Hudhaifa. Wayahudi nao hawakusahau kutolewa kwao Madina na hata huko Khaibar walikohamia bado walitozwa nguvu na kulazimika kulipa Jizya. Makundi yote haya yaliungana kwa kujuana na kutokujuana kwa kusimamisha upinzani dhidi ya Khalifa Uthman na serikali yake na hatimae kumuua. Fitna za Abdullah bin Saba Pamoja na makundi mengi haya, kiongozi wa udhia wote huu ni Myahudi aliyekuwa mkazi wa Yemen aliyejulikana kwa jina la Abdullah bin Saba. Saba hakuwa anataka Uislamu, na alipanga mpango wa kuudhuru Uislamu mbinu aliyotumia ni kuingia katika Uislamu na kuupiga vita Uislamu kutoka ndani. Kwa kutumia hali ya mazingira ya wakati ule alitunga na kuhubiri imani zisizokuwemo katika Uislamu ambazo ni kila Mtume aliacha "Wasi" (administrator) mtawala (mrithi wake katika ujumbe wake) na wasi wake alikuwa ndugu yake, kwa mfano Mtume Mussa alimfanya Haruna kuwa "Wasi" na Mtume wasi wake ni ndugu yake ali. Na ali alikuwa mtu pekee aliyehalali kupewa Ukhalifa. Saba alifikia kiwango cha kusema kuwa makhalifa watatu waliotangulia Abubakr, Umar na Uthman sio wa halali. Namna pekee ya kurekebisha mambo ni kumuondoa Khalifa Uthman madarakani: (i) Akafundisha kuwa ni ajabu kuamini kuwa Nabii Isa atakuja kutoka mbinguni ili afuate Uislamu na kuupigania dhidi ya maadui na kuamini kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.) hatarudi. Saba aliamini na kufundisha kuwa Mtume Muhammad kuwa ni mbora kuliko Mtume Issa na kwa kuwa Yeye Muhammad ndie Mtume wa mwisho basi atarudi. (ii) Hali kadhalika alianza kutoa tafsiri potofu za aya za Qur’an ili kuhalalisha imani zake.82 Kwa hiyo mbinu moja aliyoitumia ni kuhubiri imani ptofu hizo. ali alimtaka aache maskhara haya lakini hakukubali. Hivyo katika ukhalifa wake Ali alimchoma moto saba, 83 katika mpango wake huu sabaa alichagua maeneo yaliyokuwa imara kijeshi, Kufa, Basra, Syria na Misri kama vituo vya kueneza shughuli zake. Madina hakupata wafuasi, hivyo alikwenda Basra na kuendesha shughuli zake za upinzani dhidi ya Serikali. Gavana wa Basra Abdallah bin Amir alimwita na kumhoji kwa sababu hii Sabaa aliogopa akaondoka Basra na kuwacha wafuasi wake chini ya uwongozi wa Hakim Hublah adui wa Gavana. Kutoka Basra alikwenda kufa ambako alipata wafuasi wengi. Gavana, wa
Kufa Sa’d bin Al As alimwita Saba na kumuonya juu ya udhalimu anaoufanyia
Uislamu. Hatua hii ilimfanya ahame Kufa aende Damascus ambako hakufanikiwa
lakini alimteua Ashtar kuwa naibu wake na kuacha maelekezo kuwa ujumbe
wake uendelee chini chini na yeye akahamia Misri.‘ Ambako kwa kuwa Gavana
wa Misri Abdallah bin Sarah alikuwa katika vita vya Warumi, Saba alipata
muda wa kupandikiza fikra zake potofu akapata wafuasi wengi na kuweza kuwasiliana
na vituo vyake vya kufa na Basra. Wafuasi wa uasi huu, walitumia mikakati
mingi ya kujiimarisha walijionyesha kuwa ni wacha Mungu na kushawishi watu
waunde malalamiko dhidi ya Maafisa wa Serikali, Magavana na Khalifa. Walitawanya
barua za kuonyesha udhalimu wa serikali hali ni madai ya uzushi. Barua
hizi zilitumwa kwa wafuasi wa Saba nao wakawa wanazisoma hadharani. Walionyesha
kuwa Ali Talha na Zubair Maswahaba maarufu kwa wakati ule waliwaunga mkono84
ili kuunda taswira ya kuonyesha kuwa kweli serikali ina matatizo.
|
YALIYOMO
Tahari
Kupokelewa kwa malalamiko ya Waislamu: Masheikh wasubiri ukweli wa Mkapa Afariki baada ya kutokwa damu nyingi: Yadaiwa hakuwa na sh. 4,000 Nyumba ya Wakfu iliyoporwa yarejeshwa Kamanda Gewe atakiwa amkamate Daniel Sheikh awasambaratisha walevi Liwale Msikiti wavamiwa na kuvunjwa milango, madirisha Msikiti wa Mwinyimkuu wafanya sensa Njaa hakuna, tunategemea kula silaha Mabaraza yawatetee Waislamu - Sheikh Bafadhil Hali ya Uislamu Lukulunge, Kongwa inatisha Waislamu Kondoa waagizwa kuyatunza magazeti ya ANNUUR Sabato ni ya Waisraeli, Mungu alikwishaiondoa
Tume ya kubadili Katiba Kenya: Waislamu kuwakilishwa Waislamu Msonge waomba wanusuriwe Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|