|
|
|
Siasa ya dini, utaifa na ukabila huharibu bidii ya kujenga taifa Ngurumo No. 635 Jumatano, Mei 3, 1961, bei senti 10 MKUTANO wa waandishi magazeti wa Bw. J.K. Nyerere tangu awe Prime Minister uliofanywa hapo jana asubuhi mjini Dar es Salaam, ulielezwa kwamba yeyote atakayejaribu kuitumia dini, ukabila au utaifa katika mambo ya siasa anajaribu kuharibu bidii ya kujenga Taifa. Na hii si njia ya kuunda upinzani. "Kama ni upinzani uwe ambao unaipinga serikali na kutoa makosa katika mambo kama vile serikali kushindwa kuwapatia raia shule nyingi kama ilivyoahidi au kutokutengeneza barabara ilizosema itazitengeneza au kujengesha hospitali. Upinzani huo usiwe hata kidogo wa kuharibu taifa", aliongeza. Prime Minister akatoa mfano wa upinzani kwa kusema, "kama huko Uingereza kuna upinzani katika serikali ya Malkia, lakini upinzani huo wa wa heshima ambao pia unaimani katika taifa lake". Kuzuia "Hivyo katika taifa changa kama Tanganyika kwa mtu mwenye imani ya demokrasia kama mimi kwa faida ya upinzani, kama kikundi fulani kinajaribu kuleta siasa ya utaifa, kabila au dini, na kama ningekuwa na sheria ya kukitia ndani kikundi hicho, basi ningekitia, laa kama sina, sheria hiyo ingeitunga". Alipoulizwa kwamba ni kwa njia gani Serikali itajaribu kuzuia kuwepo na upinzani, alisema kwamba yeye anafikiri kuwa wale ambao wana imani na demokrasia kwa kujiepusha na upinzani katika serikali, ni haki watoe mawazo si kwa kuieleza serikali ni njia gani izuie upinzani, ilani kwa njia gani upinzani uzuie serikali na wao wenyewe wajiheshimu. Mawazo ya umoja ni kama mageni tu ukilinganisha na mawazo ya ukabila, rangi au dini. Kwa hiyo mtu anayejenga upinzani kwa njia hii anayo nafasi kubwa ya kuvuta mawazo ya raia. Prime Minister akazidi kutia mkazo usemi wake kwa kusema kwamba katika serikali ambayo inaendeshwa kidemokrasia halisi kazi za chama ambacho ni cha upinzani ni kuichangamsha serikali iwe motomoto isisinzie katika kazi yake. Lakini basi hata hicho chama cha upinzani nacho huwa kinashilia nia ya siasa ya umoja na taifa. Sheria itungwe "Ikiwa humu nchini Tanganyika nitaona mtu ambaye anajaribu kutumai vyama ambavyo siasa yake ni ya upinzani ambao unaweza kuvunja umoja wa nchi hii hapa bila shaka huenda nikamtia ndani. "Lakini basi serikali hii ya sasa sheria zake haziruhusu kufanya mambo kama hayo, hivyo nitafanyisha sheria itungwe ili serikali ipate uwezo wa kufanya hivyo", alitamka. Jamhuri Katika maelezo yake hayo, Prime Minister aligusia jambo la Jamhuri na hapo ndipo aliposema kwamba kwa hivi sasa bado haijawaziwa nchi ya Tanganyika kuifanya iwe Jamhuri isipokuwa jambo la kwanza la kuwaza ni uhuru wa nchi hii. Akatoa mfano kwa kutaja Ghana na India akisema nchi hizi zilianza kwanza kufikiria uhuru wake na zilipokwisha kuupata ndipo zikafikiria kuunda Jamhuri. "Kama jambo hili la Jamhuri litafikiriwa itakuwa hapo nchi hii itakapokuwa inatengeneza mabadiliko yake ambayo ni ya mwisho kabisa", alimaliza. Ngurumo No. 635 Jumatano, Mei 3, 1961, bei senti 10 KATIBU Mkuu wa chama cha Wafanyakazi katika Serikari Kuu, Bw. Mahami Rajabu Kundya, M.L.C. wa sehemu ya Singida ambaye hivi sasa yuko Singida anakosimamia katika Lejiko na aliondoka Dar es Salaam akiwa likizo, ameomba ajizulu kuwa Katibu Mkuu wa TUPE. Habari kwa kirefu tumezipata kuwa amepeleka barua mbili kwenye Halmashauri Kuu ya chama hicho cha TUPE anachokiongoza yeye akiomba ajiuzulu. Hakubali Mwenye barua hizo mbili alieleza shida kubwa ambazo zinamkabili wakati akiwa anashughulika na sehemu ya Singida ambayo anaisimamia katika Lejiko. Lakini basi ingawa Halmashauri hiyo kuu ya TUPE aliyoipelekea barua hizo mbili ilikutana hivi majuzi kufikiria jibu la barua hizo, hata hivyo Halmashauri hiyo imependelea kwamba haikubali Bw. Kundya ajiuzulu kwenye chama hicho, isipokuwa aendelee tu kuongoza chama. Akirudi Mwisho Halmashauri hiyo ikaamua kwamba itangojea mpaka yeye mwenyewe
atakaporudi Dar es Salaam ndipo itamkalisha kitako na kumweleza maoni yao
juu ya kukataa kwao yeye ajiuzulu na yey eatoe maoni yake. Huenda ndio
jawabu litapatikana.
|
YALIYOMO
Tahari
Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze: Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri Wenye siasa za kikaburu wasimyumbishe Rais Hatuko tayari kuruhusu viwanja viporwe - Manyema Maoni yetu
DONDOO ZA KISAIKOLOJIA: PEDOPHILIA Uislamu na Mazingira katika
Umoja wa Mataifa
Barua za Mtume (s.a.w.) za Jihad katika
Internet
Rais Mkapa atekeleze hadi yake
kwa hadhari
Mashirika ya Dini yaelekeze
misaada vijijini
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma Ni serikali ipi anayoiwakilisha
Sumaye
Sehemu ya maelezo ya Waziri Mkuu bw. Frederick Sumaye bungeni Zanzibar ni nchi au mkoa?.
Sheikh Bafadhil aamuru kusimamishwa shughuli za African Muslim Agency Moro Vijana Arusha njooni mnione - Alhaj Mollel Waislamu Korelo wazama kwenye ushirikina Waislamu Hanang’ wajenga Msikiti Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
|