|
|
|
WALIPOULIWA Waislamu pale Mwembechai mengi yalisemwa na viongozi wa serikali kuhalalisha unyama na mauaji hayo. Wapo waliodai kadhia yote ile ilichochewa na Balozi za nje, wengine wakaja na kisingizio cha uchochezi wa vyama vya siasa, lakini wengine wakadai ni suala la wakorofi wachache wanaotaka kuvuruga amani ya nchi. Katika ujumla wake, propaganda zote hizo zililenga kupotosha ukweli kwamba kadhia yote ile ilikuwa uonevu na dhulma dhidi ya Waislamu. Lakini baada ya vumbi la propaganda kutulia ukweli umejidhihirisha. Waislamu wote washasema lile lilikuwa la Waislamu wote na ule ulikuwa udhalimu uliofanywa na vyombo vya dola dhidi yao. Hilo limesemwa na Waislamu wa Taasisi na madhehebu zote nchini. Sasa tusirudishane tena nyuma. Tunasema hivyo kwa sababu inaonekana juhudi zipo kutaka kuturudisha nyuma. Wakati Rais keshapokea risala ya malalamiko ya Waislamu kwa mikono miwili, wapo bado watu wanasimama na kutuletea unyeti katika madai ya Waislamu. Tunalosisitiza hapa ni kuwa huko tushatoka. Hakuna unyeti wala kughilibiana. Hapa kuna wananchi Watanzania Waislamu waliodhulumiwa na wanaondelea kudhulumiwa na vyombo vya dola. Ni haki ya wananchi hao kuwalalamikia viongozi wao. Hatua iliyofikiwa ni ya kukusanya ushahidi wa madai ili kumsaidia Rais katika hatua zake za kuyashughulikia. Sasa kama atasimama mtu kwenye jukwaa lake liwe la siasa, gazeti, Msikiti au Kanisa akawashutumu Waislamu basi huo ni ushahidi usiohitaj uchambuzi wa kisayansi. Haraka apelekewe Rais. Yapo madhila mengi ambayo hayajasemwa. Hayo yajumuishwe pamoja na yale ambayo yapo wazi na hayajibiki. Mfano suala la elimu halijibiwi kwa kusema kwamba wanawake na watoto wa wafugaji nao wapo nyuma. Maelezo hayo hayakani kuwepo kwa dhulma, zaidi yataonyesha kwamba wanaoonewa ni wengi. Yanapotolewa majibu ya visingizio kwa madai mazito kama haya, tafsiri yake ni moja tu; kwamba wanaolalamika wasubiri kuona dhulma zaidi. Hatudhani Waislamu wataendelea kulifumbia macho hilo. Wengine wanaotaka kupotosha ukweli ni waalimu wachache waliojitokeza kuzuia haki ya mabinti wa Kiislamu kuvaa Hijab. Hilo hatutarajii tena kuwemo katika risala za kina Alhaj Madabida. Kama Mwalimu anaona ni haki yake kufanya kazi na pengine anajihisi anayo haki zaidi ya wengine, basi ajue kuwa binti wa Kiislamu ni haki yake pia kupata elimu katika nchi yake na kwake kuvaa hijab ni haki yake zaidi. Waalimu hawa wanaoonyesha chuki dhidi ya hijab tunaishi nao mitaani na tunashirikiana nao katika maziko, harusi na hafla mbalimbali. Hatuoni hizo chuki zao huko mitaani tunapokutana. Sasa isije ikawa hawa wapo mashuleni kama mawakala wa madhalimu wenye nia mbaya ya kuendeleza dhulma kisha kuvuruga amani ya nchi yetu. Yawezekana mawazo
hayo si yao, hivyo ni vyema kutizamwa kwa tahadhari wasije wakasababisha
wazazi Waislamu wakajikusanya mashuleni kuleta zogo.
|
YALIYOMO
Tahari
Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai:
Waliouawa ni wanne
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Wakereketwa CCM wawakosha
wauaji wa Mwembechai
Ufugaji holela wa nguruwe
waikumba Dodoma
Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh
ofisini kwake
Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
|