AN-NUUR 
Na.188 Shawwal 1419, Februari 12 - 18 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa 
 
  • Wafufua Al Jamiatul Islamiya fi Tanganyika
WAZEE waasisi wa TAA na kisha TANU wameibuka na kuanza kupigania haki zao zilizoporwa baada ya uhuru. 

Katika hatua yao ya awali wakongwe hao na veterani wa harakati za kumkomboa Mtanganyika wameifufua Al Jamiatul Islamiya Fi Tanganyika (The Muslim Association of Tanganyika). 

Ili kutekeleza majukumu ya Jumuiya hiyo wanadai mali zilizoporwa na kupewa Bakwata wakati wa kuvunjwa East Africa Muslim Welfare Association - EASMWS. Mali hizo ni pamoja na jengo la Mtaa wa Lumumba linalotumiwa na Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa maelezo ya Katibu Mtendaji wa Al Jamiyayatul Islamiyyah Mzee Ally K. Sykes, jengo hilo la Lumumba linalotumiwa na Bakwata wanalihitaji ili kuanzisha shule ya watoto wadogo. 

Taarifa za uchunguzi wa gazeti hili zinaonyesha kwamba Bakwata wanasita kutoa nafasi kwa Al Jamiyyah jambo ambalo laweza kusababisha suala hili kufikishwa mahakamani. 

Kwa muda mrefu sasa Al Jamiyyah wameomba wakutane na Bakwata kuzungumzia suala hili lakini Bakwata wamekaa kimya. 

Utafiti wa gazeti hili umeonyesha kwamba hati zote za umiliki wa jengo hilo ikiwa ni pamoja na shule ya Msingi Lumumba zipo mikononi mwa Al Jamiyyatul Islamiyyah. Hata hivyo haieleweki ni kwanini Al Jamiyyah inaomba sehemu tu inayotumiwa na Bakwata na si jengo lote wakati Wakristo washarudishiwa jengo la Forodhani. 

Al Jamiyatul Islamiyyah Fi Tanganyika ilianzishwa sambamba na TAA mwaka 1933; Katibu wake Mkuu akiwa Kleist Sykes na Rais akiwa Liwali wa Dar es Salaam Shariff Salim Omar. 

Watu wengine katika kamati ya uanzilishi walikuwa Ali Jumbe Kiro, Maalim Popo Saleh, Idd Tosiri na Mzee bin Sudi. 

Wakongwe hawa walikuwa pia waanzilishi wa TAA na harakati za kumkomboa Mtanganyika kwa ujumla. 

Hata hivyo, kwa kuona harakati zilizokuwa zinaendelea dhidi ya Waislamu waliamua kuanzisha mkondo mwingine wa harakati za kumkomboa Muislamu na kuleta maendeleo yake. 

Umahiri wa Kleist Sykes katika uongozi akiwa TAA ulisaidia sana kujiimarisha Al Jamiyyah katika kuyaendelea malengo yake. 

Walipita nyumba kwa nyumba kukusanya sadaka toka kwa Waislamu mwaka 1936 Al Jamiatul Islamiyya walifungua shule yao ya kwanza ya msingi katika mtaa uliojulikana enzi hizo "New Street". Shule hiyo ipo mpaka leo kwa jina la Lumumba shule ya Msingi.  

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Tusirudishane nyuma 

Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai: Waliouawa ni wanne
Na Mwandishi wetu

Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa

Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa

Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS

Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa

Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station

Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Na BERNARD B. MWENDA

Wakereketwa CCM wawakosha wauaji wa Mwembechai
Na Idd Kikong’ona, Morogoro

Ufugaji holela wa nguruwe waikumba Dodoma
Na Abu Zubeir, Dodoma

Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha

Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh ofisini kwake
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Kutoka magazeti ya zamani

Sayansi na Teknolojia 
[Windows: Mambo Mazuri ya Kuyajua] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi

Chakula na Lishe 
[Kauli hii ya serikali itatumaliza Watanzania kwa njaa] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai 
[Maazimio ya Maimamu Dar]
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita