Maoni
 
Tutahadhari na akina ‘Milosovic’
 
Wataisambaratisha nchi yetu

KATIKA kukabili hatua ya baadhi ya wanafunzi Waislamu kuvaa Hijab shuleni kwake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani ya Jijini ameripotiwa akichagiza wanaotaka Hijab waende kwenye madrasa (shule za awali za kufundisha Uislamu).

Aidha, amewaita wanaopigania haki sawa kwa wananchi wote wa Tanzania kama Mh. Kitwana Kondo kuwa ni wachochezi. Cha kusikitisha zaidi kauli hiyo imekuwa ikitolewa kwa jazba na hali ya kujiamini iliyopea huku mtu akijinasibu kwa Ukristo wake.

Kutokana na sababu za kihistoria Waserbia ni watu wenye chuki dhidi ya Waislamu.

Baada ya kusambaratika Taifa la Kikomunisti la Yugoslavia ambalo liliwadhibiti Waislamu, Waserbia; Wacroatia n.k. chini ya Ukomunisti. Waserbia wamejiunga pamoja na kuanzisha harakati ya kujenga kile wanachokiita "Greater Serbia" na kuisafisha jamii yao asiwepo Muislamu (Ethnic Cleansing). Kilichokuwa kinatokea Bosnia ni "Holocaust" yaani mauaji ya kuangamiza ambayo yalilenga kuwaangamiza Waislamu wote ili asisalie Muislamu huko Bosnia Herzegovina.

Mauaji hayo sasa yamehamia Kossovo ambapo Rais Slobodan Milosovic anawaangamiza Waislamu huku akichoma vijiji vyao moto. Kupoteza lengo hutangazwa kwamba wanaouliwa ni watu wa asili ya Albania badala ya kusema Waislamu. Lengo ni Cleansing - kusafisha nchi asisalie Muislamu.

Sura inayojitokeza nchini hapa inatia wasiwasi. Isijefika mahali tukawa na akina Slobodan Milosovic wa kwetu. Wakati akina Milosovic wanaisafisha jamii, hapa yaelekea kuna harakati za kusafisha taasisi za elimu na nyingine nyeti katika nchi . Tofauti hii si muhimu kwani ni suala la muda tu maadhali tutakuwa na watu wenye mtazamo hasi dhidi ya Waislamu.

Serikali ya Kikoloni ya Kijerumani kutokana na mtazamo wake hasi dhidi ya Waislamu iliagiza kampeni kubwa ifanywe ya kufuga nguruwe wasambae kila mahali ili kuwakimbiza Waislamu katika miji yao na vijiji vyao.

Baada ya uhuru nguruwe wakafugwa sana katika mashule ya serikali kwa kisingizio cha "Elimu ya Kujitegemea". Mwanafunzi Muislamu akalazimika ama ahudumie nguruwe asome au achunge Uislamu wake akose shule.

Katika baadhi ya mashule nguruwe alifanywa sehemu ya mlo wa shule na wanafunzi Waislamu walipolalamika ikadaiwa kwamba huo ni uamuzi wa Baraza la Shule.

Yote haya yalifanywa ili kuyafanya mazingira ya kusoma kwa Muislamu yawe magumu sana akimbie au akibaki awe Muislamu jina atakayehudhuria hafla zenye ‘Kiti Moto’ ili mradi tu yeye hali.

Leo Mwalimu Mkuu wa shule kumwambia mwanafunzi akitaka kuvaa Hijab "nenda kwenye madrasa" ni yale yale ya akina Milosovic ya kujiona Waserbia ndio wenye haki na Yugoslavia na wengine ni wa kusafishwa. Aidha, ni yale yale ya kuwasafisha Waislamu mashuleni kwa kuwawekea mazingira hasi dhidi yao.

Si mahali muafaka kueleza chimbuko la hisia hizi za Waserbia dhidi ya Waislamu. Lakini tungependa tujue fikra hizi hasi za akina Paulina zimetoka wapi! Kujiamini huku kwamba wao ndio wenye haki na nchi hii na kuwapangia Waislamu kwamba wakitaka kusoma wafuate taratibu zilizo kinyume na dini yao, wameipata wapi!

Tulidhani kwamba baada ya Mh. Rais Benjamin William Mkapa kuonyesha nia njema ya kusafisha mwelekeo huu hasi ambao unaelekea kuisambaratisha nchi yetu; wenye fikra za akina Milosovic angalau wangefutika hisia zao kwa muda. Lakini kauli hizi zinadhihirisha jambo moja kubwa: Hatua iliyofikiwa ni kubwa.

Watu chuki zao dhidi ya Waislamu zishakubuhu. Na kama tunataka kuinusuru nchi hii basi kazi kubwa na ya haraka inahitajika. Tusidhanie akina Milosovic walianza na kuwasafisha wanaowaita Waalbania.

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
YALIYOMO | An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook