Dr. Omar Abdul Rahmaan aongea na Jarida la Nidau’l lslam
 

Dr. Sheikh Omar Abdul Rahmaan ambaye amefungwa katika jela za Amerika ni alama ya jihadi dhidi ya ungandamizaji wa kimataifa. Sheikh huyu kipofu ameyatoa maisha yake yote katika kuwazindua Waislamu juu ya ulazima mkubwa wa kumpwekesha Allah (s.w) kwa kuitekeleza shariah na kuifuata njia yake (Allah). Tutamuacha mwanazuoni huyu mkubwa kabisa wa Kiislamu atuaeleze mwenyewe juu ya harakati zake kama alivyohojiwa akiwa jela na Jarida la Nidau’l Islam.

Alhamdullilah. Rehema na amani za Allah ziwe juu ya mjumbe wake (S. A. W). Ndugu zangu wapendwa, wa kike na wa kiume; As Salaamu alaykum wa Rahmafullahi wa Barakatuh.

Ni jambo ovu kwa mtu kujiongelea yeye mwenyewe, mafanikio yake na msimamo wake. Hata hivyo, maelezo mafupi tu yanatosha kueleza juu ya harakati zangu.

Mwanadamu (yaani yeye mwenyewe Sheikh) alipoanza maisha yake, Allah alimfundisha kujitahidi katika njia yake na akamuongoza katika njia iliyonyooka. Nimejaribu kusema neno la ukweli huko Misri na kukabiliana na ‘masanamu’ au udikteta wa mtawala mmoja aliyekuwepo, na ambao bado upo Misri, kupitia semina, mihadhara na darsa. Al Jamaa Al Islamiya (Kundi la Kiislam) liliweka jitihada kubwa kuwafanya watu waielewe vizuri dini yao. Nilishakamatwa na kutiwa ndani mara nyingi kutokana na hayo na kushtakiwa katika kesi ya Al Fayoumm, kesi ya mauaji ya Saadat, kesi ya kuupinga utawala wa kidikteta uliopo Misri n.k. Tulisingiziwa katika kesi nyingi tu lakini Allah (S.W) alitupa ushindi mkubwa dhidi ya utawala (wa Misri) katika kesi hizo.

Nilisafiri kwenda Ulaya nikipita Uingereza, Denmark, Sweden na nchi nyingi nyinginezo. Huko nilikutana na ndugu zangu wa kweli wa Kiislamu, nikafanya mihadhara kuwatanabahisha Waislamu juu ya jukumu la kuipigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali na nafsi zao na kukabiliana na maadui zao (na maadui wa Allah). Mwishowe tukafika Amerika ambapo nilitembea majimbo mbalimbali, nikiongelea juu ya majukumu ya Waislamu kwa dini yao, jinsi ya kuupa Uislamu kipaumbele muda wote na kujitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na usipite hata mwaka mmoja katika maisha ya Muislamu bila ya harakati hizi (kwa ajili ya Allah)

Kisha nikaenda katika nchi nyingi nyingine duniani lakini nikaishia kutupiwa kesi hii ya kusingiziwa na baadaye kifungo (cha maisha jela). Ninamuomba Allah atuwezeshe kusimama imara katika ukweli na atupe rehema na malipo ambayo huyatoa kwa waja wake wanaofungwa (wakifanya harakati kwa ajili yake). Kuna malipo makubwa ya rehema ambazo mtu huzipata kwa kufungwa jela (kwa ajili ya Allah) na tunamuomba (Allah) atunufaishe nazo.

Njia unayoifuata (katika dini na harakati zako) Sheikh imedhihirika kuwa ya usafi wa nia na kutomuogopa (binadamu yeyote isipokuwa Allah (S. W)) hivyo kukufanya uandamwe na maadui wa Mwenyezi Mungu. Je unaweza kutueleza (mambo) muhimu yanayoambatana na njia (unayoitumia)?

Njia hii ni sawa na ile ya maswahaba na ambayo imefafanuliwa katika Kitabu cha Allah (Qur’an) na hadithi za Mtume wetu (S.A.W). Na njia ninayoifuata haipo mbali na hapo (Quran na Sunnah). Na ndio njia iliyotumiwa na maswahaba na waliowafuata hao maswahaba ambao waliuchukua Uislamu katika ujumla wake, na hawakuruhusu kugawanya au kuchagua mambo ya kuyafuata katika dini. (Njia hii) inachukua maamrisho yote ya Uislamu, makatazo yote na haipuzii hata jambo moja. Kuna baadhi ya njia (zinazofuatwa na baadhi ya wanaharakati wa Kiislam) ambazo hulenga suala la imani pekee, au vitendo vya ibada pekee, mambo yanayohusiana na biashara pekee au njia moja au nyingine katika vifungu vingi vinavyohusiana na Uislam. Hizi njia zote ni za makosa. Allah (S.W.T) alisema katika aya za mwisho katika kuteremshwa Quran: "Leo hii nimekukaminishieni dini yenu, na kuitimiza neema yangu juu yenu, na nimeridhia Uislamu kuwa dini yetu. Qur’an 5:2.

Hivyo Allah (S.W.T) ametuletea mwongozo kamili wa maisha ambapo hakuna kipengele kinachozidi umuhimu kinginecho. Miongoni mwa vipengele vilivyopuuziwa na wanazuoni wengi, na baadhi ya wale wanasimamia harakati Kiislam, ni suala la Jihad (Kujitahidi katika njia ya Allah) kama vile kusema ukweli, kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kipengele hiki (Jihad) kinaambatana na matatizo mengi, mateso na maumivu. (Hivyo) kipengele hiki kimepuuziwa na wengi. Neno la kweli huja na matatizo na hatari yake. Kuamrisha mema, na hasa, kukataza maovu pia huambatana na mitihani na kusukwasukwa hivyo kupuuziwa na wengi. Baadhi ya watu hukishambulia kipengele hiki cha Uislamu na kuwashambulia wale wanaofanya Jihad. Kwa kweli kuamrisha mema na kukata za mabaya ndiyo ‘injini’ ya harakati za Kiislam. Ni kipengele kinachohifadhi kanuni na misingi ya dini. Hata hivyo wengi wameyapuuzia haya.

Haya ni baadhi ya mambo unayoweza kuyaambatanisha katika njia ninayoifuata katika harakati zangu. Hata hivyo, njia hii ni Uislamu kwa ujumla (wake) kama ulivyofuatwa na wale waliorithi mwenendo wa maswahaba ambao waliopokea Uislam bila kuugawa katika vifungu na bila kuchagua wapi ya kuyafuata na yapi ya kuyaacha.

Utawala wa Amerika (USA) majuzi vimetenga bajeti ya dola billioni 2.3 ili kuviangamiza vikundi vya Jihad. Je unadhani kwa maoni yako ni upi uwezekano wa kufanikiwa kwa vita hivi vipya vya msalaba dhidi ya ulimwengu wa Kiislam?

Makabiliano baina ya watu wa msalaba (Crusaders) na Uislam ni ya siku nyingi. Katika ya miaka ya mwanzo ya kuibuka Uislam kulikuwa na dola mbili kubwa, Waajemi na Warumi. Ilichukuwa mapigano kidogo tu, yakimalizikia na vita vya Al Qadeseya, kuivunja kabisa dola ya Kiajemi. Dola ya Kirumi, hata hivyo, ilichukua sura mpya katika karne tofauti zilizofuatia. Dola moja ya kirumi ilipoangamizwa, nyingine huja kwa sura mpya karne inayofuatia, kama ambavyo imedhihirishwa na hadithi moja ya Mtume (S. A. W). Na karne hizi za mabadiliko ya dola ya Kirumi ni zenye kuendelea. Na Dola ya Kirumi inamaanisha (Vita vya) Msalaba vya Kimataifa (International Crusade) na Uzayuni wa Kimaitaifa (International Zionism). Na vita vya msalaba vitaendelea mpaka siku ya malipo. Na jumla ya pesa ulizotaja ni sehemu kidogo tu ya kiasi halisi wanachotenga maadui wa Uislamu katika kuupiga vita. Hivi ni vita vinavyoendelea. Kila mara Waislam wanaposhikamana na dini yao basi huweza kuwashinda maadui zao. Lakini wanapogawanyika na kuvunja umoja wao, kama walivyo sasa, maadui zao huweza kuwashinda kirahisi.

Acha iwe dola bilion 2,3,10, hata zaidi wanazozitenga. Hii ni sehemu tu fedha ya wanayoitaja. Bajeti za siri zisizotangazwa ni kubwa zaidi. Nayo hii ni sehemu moja tu ya hazina yao. Hazina nyinginezo ni nyingi zaidi. Allah (S.W.) ametueleza kiasi wanachotenga katika kuupiga vita Uislam. "Makafiri hutumia pesa zao kuwazuilia watu katika njia ya Allah. Watatumia, lakini watajutia na mwishowe watashindwa. Makafiri watahudhurishwa motoni".

Pia Allah (S.W.) anasema "Waambie makafiri kwamba watashindwa kisha kutiwa motoni. Na huu ndio mwisho mbaya".

Hizi ni rasilimali ndogo tu kati ya nyingi nyinginezo walizotumia toka zamani na (ambazo watazitumia) baadaye lakini mwisho wake ni majuto.

Waliwatuma Wamishionari Afrika na kudai kuwa Afrika yote itaingizwa katika Ukristo katika karne chache au hata miongo michache (decades). Miongo na karne nyingi zimepita tayari hata hivyo Afrika ina hali nzuri zaidi kwa upande wa Uislam kuliko wakati wowote hapo nyuma. Kwanini basi? Pesa zao zimepotea, juhudi zao zimeruka patupu na wamishionari wamefanikiwa kidogo au pengine hawajafanikiwa chochote (kulinganisha na pesa walizotumia). Wanapomuingiza mtu mmoja katika Ukristo, kumi wapya husilimu, wanapowangiza watu 10 Ukristo , 100 wapya husilimu. Mapesa hayo wanayoyatenga hayatutii woga wowote. Na wala hatujali kiasi cha pesa walizokusanya na kiasi gani walizotenga (Kuupiga vita Uislam). Ngoja nikukumbushe, katika karne ya 19 na 20 wakati Waislamu walipokuwa wamesambaratishwa na wakiwa wamepoteza kabisa nguvu yao, wakati wakoloni wa Kingereza na Kifaransa walipokuwa wameshika hatamu na Uislam ukiwa bila nguvu yoyote, nani aliulinda Uislamu?. Nani aliwalinda Waislam? Allah (S. W.) anasema "Leo hii makafiri wamekata tamaa na dini yenu, hivyo msiwaogope ". Wamekata tamaa! walikata tamaa karne 14 zilizopita. Walikata tamaa karne ya 14, walikata tamaa karne ya 13, ya 12 n.k. Makafiri wamekata tamaa na dini yenu hivyo msiwaogope. Niogopeni Mimi. Kukata tamaa ndio jambo linaloendelea sasa. Kukata tamaa katika kuubadilisha Uislam (kama walivyofanikiwa kuiubadilisha Ukristo na Uyahudi). Walitenga fedha nyingi kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya idadi ya watu uliofanyika Cairo, Misri na kujenga maazimio yenye kuruhusu zinaa, utoaji mimba na ushoga. Maazimio ya kuwashawishi wasichana kupoteza heshima na usafi wao, maazimio ya kudhoofisha mamlaka na uwezo wa wazazi dhidi ya watoto wao. Walitumia mabilioni ya fedha kufanya mkutano ule. Na walitenga bajeti kubwakubwa kutimiza malengo yale. Hili halitupi woga. Kinachotuogopesha sisi na kugawanyika sisi wenyewe ndani kwa ndani. Hatuwezi kushindwa toka nje, hatujui idadi ya maadui wetu au mali waliyonayo. Tunachohofia ni mgawanyiko wetu ndani kwa ndani, kwa miongoni mwetu wenyewe kuwa maadui zetu, na kutangaza vita miongoni mwetu. Sisi Waislamu tunapaswa kushikamana na dini yetu na kusimama imara na kuungana pamoja katika imani yetu. Qibla yetu (Makka) ni moja na zaidi ya yote (tumeunganishwa na) Kitabu cha Allah na mafundisho ya Mtume (S.A.W.).

Sasa tuelekee katika vita vya msalaba vya vyombo vya habari dhidi ya Uislam ambayo mara kwa mara hutumia maneno kama ugaidi, siasa kali na imani kali. Je unaweza kufasiri maneno hayo kutikana na mtazamo wa shariah?

Sitayatafsiri maneno hayo katika mtazamo wa shariah. Kinachonigusa mimi ni kwamba wanayachukulia maneno haya imani kali, ugaidi na siasa kali kumaanisha kila Muislamu anayeshikamana na dini yake. Hilo ndilo ninalojali mimi. (Wanachosema wao) chanzo chake ni lugha iliyotumika katika meneno ya Allah (S.W.) yanayosema "… na ziandaeni nguvu zenu na nguvu nyinginezo katika kila mtakachoweza katika farasi n.k. ili muwaogopeshe maadui wa Allah na maadui zenu" . Kilicho muhimu ni matumizi yao ya maneno haya. Kila mmoja ambaye ameshikamana na dini ya Allah, kila aliye imara katika dini ya Allah na kila anayeitetea dini ya Allah huwa gaidi (Kwa mtazamo wao) na pia ni siasa kali na imani kali.

Neno siasa kali (Fundamentalism) limechukuliwa toka katika matumizi ya Ukristo wenyewe. Lakini (Kinyume chake) tunakuta vyombo vyao vya habari vikiwashambulia Waislamu ambao hawataki kuachana na dini yao, ambao hushikamana na dini yao, wanafanya kazi (Ya daawa) kwa ajili ya dini yao, na wanainusuru dini yao. Watu wa Nchi za Magharibi na zile zinazoitwa serikali za Kiislamu huvipiga vita kwa nguvu zao zote vikundi vya ‘siasa kali’ na vikundi vya ‘imani kali’ kama wanavyoviita wao. Nini maana ya vikundi vya siasa kali? Ni vikundi vinavyofanya harakati ya kuihifadhi dini yao na kushikamana na Kitabu cha Mola wao na mafundisho ya Mtume (S.A.W.). Hawa ndio walengwa wa vyombo vya habari vya Kimagharibi na wale walio nyuma yao.

Vipi uliyaonaje madai ya demokrasi na uhuru wa kutoa mawazo pamoja na uhuru wa kuabudu katika nchi zinazojiita za kidemokrasia na ulimwengu huru wa Kimagharibi?

Kama nikisema kwamba nchi za Afrika ya kati zina uhuru zaidi (wa mambo uliyoyataja) kuliko Marekani sitakuwa nimekosea. Maneno hayo (demokrasia, uhuru wa kuabudu n.k.) ni mfano wa pipa tupu ambalo kutokana nalo unasikia mwangwi na sauti ya juu bila ya kuwa na maana yoyote au manufaa (yoyote kwa msikilizaji). Haya ni maneno matupu, kwa sababu ni uhuru kwa ajili yao wenyewe lakini hawaruhusu uhuru huo kwa wengine. Ni demokrasia ya kuifurahia wao lakini hawaruhusu wengine kuwa na maoni au fikra tofauti na wao. Nilikuja hapa nikiimbia jela kuja kwenye nchi ya uhuru, lakini badala yake nikafungwa. Nilikuja (hapa) nikikimbia (hali ya) kunyimwa uhuru na kuzuiliwa kutoa mawazo, lakini nilistushwa na hali mbaya zaidi Amerika. Maneno haya (ya uhuru na demokrasia) ni kwa ajili ya tabaka fulani kunufaika nayo lakini wengine wananyimwa.

Vipi kuhusu haki za binadamu ambazo wanaziimba usiku na mchana, unavyoziona wewe hali ya kuwa umefungwa jela?

Hali yangu katika jela ni mbaya zaidi ya hali yangu iliyokuwa katika jela za Misri, ni mbaya kuliko hali katika jela zingine katika nchi nyingi. Katika jela ya Amerika hakuna uhuru wa kutoa mawazo, uhuru wa kufanya ibada na uhuru wa kukutana na wafungwa wengine. Siwezi kutimiza wajibu wangu katika kuabudu kwani hakuna sala ya Ijumaa, hakuna mkusanyiko, hakuna kuchanganyika na waislam wengine, hakuna kusherehekea sikukuu za Kiislam na hakuna udhihirisho wowote dini ya Kiislam. Yote hayo nimenyimwa. Wanahalalisha kuninyima (uhuru huo) kwa sababu za na zisizokuwa na msingi. Ama kuhusu kuchanganyika, nipo katika kifungo cha ndani ambapo nimetengwa peke yangu (solitary confinement) toka nilipofungwa mwaka 1993 mpaka leo. Nimeishi peke yangu bila ya mtu yeyote wa kuniangalia. (Hivyo) mimi ndiye ninayefua nguo zangu. Wanahalalisha haya kwa kusema kwamba mtu kipofu anapaswa kutengwa…Mtu ambaye hataki kujifunza Kiingereza anahitaji kutengwa peke yake. Kwa hiyo sababu ambazo zinahitaji mtu kuchanganyika na wenzake (ili ajifunze Kiingereza) wao wanazifanya kuwa sababu za kumtenga mtu!. Huo ndio uungwana wanavyodhani wao. Ninateseka humu jela kwa kukosa kabisa mawasiliano na nje, hakuna radio, hakuna kinasa sauti, hakuna mfasiri. Yote haya wananinyima. Hakuna kusoma, hakuna wa kunisomea magazeti, vitabu au chochote kile. Katika kifungo hiki cha kutengwa ninapata mateso makubwa. Wameweka juu ya selo yangu sauti kubwa zenye kusumbua ambazo hunifanya nisilale usiku kucha. Vile vile wameweka ugumu katika ratiba yangu ya kutembelewa na mambo mengine ya kawaida katika maisha.

Cha kuzingatia kuhusiana na nilichokisema katika haki za binadamu, ni kwamba jumuiya nyingi za haki za binadamu zilipeleka taarifa katika utawala wa jela na wakuu wa magereza wa Amerika wakiuliza juu ya madai ya kwamba nilikuwa nikinyimwa uhuru na kufanyiwa mambo mengi mabaya hapa jela. Waliuliza utawala wa jela wakitaka majibu ya maswali yao. Lakini nini jumuiya hizi za haki za binadamu zilipata?. Hawajapata jibu lolote mpaka sasa. Ziko wapi basi hizo haki za binadamu wanazojitapa nazo?. Na ziko wapi haki wanazowapa Waislamu? Kila mara ninagonga mlango mfululizo ili labda waniletee kitu ninachokihitaji, lakini sipati majibu. Mara nyingine ninagonga kwa masaa mengi tu hali ya kuwa baadhi ya wafungwa wanagonga mara chache au wanamwita askari wa jela ambaye huja mbio kuleta wanachokitaka, wakati mimi inanichukua masaa kadhaa kupata ninachotaka. Ubaguzi wa rangi upo katika namna wanavyotuhudumia. Na bado utakuta watu wanatamba kuhusu uhuru na haki za binadamu!

Nini jukumu la Waislamu wanaoishi nchi za Magharibi juu ya dini yao?

Majukumu ya Waislamu wanaoishi nchi za Magharibi katika dini yaoni kuungana na kujiendeleza kiuchumi na kifedha. Lazima wawe na pesa. Pesa (kwa wakati tulionao) ndio yenye kuendesha mambo mengi katika maisha. Muislamu mwenye nguvu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko Muislamu dhaifu. Hivyo Waislamu lazima wajijenge kifedha, wawe na vyombo vyao vya habari, wawe wazalishaji wazuri (wa bidhaa) na waungane katika vyama na jumuiya za viwanda na kilimo. Lazima wainusuru na kuilinda dini yao, familia zao na wasichanganyike na wengine katika namna ambayo itawalazimu waachane na dini yao. Lazima watambulikane na wawe na utambulisho wa nguvu wa Uislamu wao na wasipoteze chochote katika hivi.

Je kuna neno la mwisho unalotaka kuwapa Waislamu wasomaji wa Jarida hili?

Neno langu la mwisho ni kwa Waislamu kuacha kulala na watupilie mbali uvivu uliozunguka vichwa vyao. Tukumbuke maneno ya Mtume (S. A. W) kwa mkewe: "Ewe Khadija! Muda wa kulala umekwisha". Lazima (Waislamu) wajikusanye kama kitu kimoja, na wafanye sana kazi kwa ajili ya dini, kuupa Uislamu kipaumbele katika maisha yao na wasilisahau jambo hili. Mtu akiwa na jambo linalomshughulisha basi hulala na kuamka akiwa bado anafikiria jambo lile. Hivyo basi Waislamu waufanye Uislamu kuwa jambo linalowashughulisha. Basi mioyo yao iumie kwa mabalaa yanayowapata Waislamu wengine. Waumie roho zao kwa Waislamu wa Bosnia, Afaghanistan, Uturuki, Phillipines na kabla ya hapo, Palestina. Nyoyo zao ziume kwa ajili ya kutaka kuwasaidia Waislamu hawa na walie kwa kutokutimiza wajibu wao kwa Waislamu hawa. Waislamu lazima wawajali ndugu zao popote walipo., lazima wajali wale waliofungwa na lazima wajaribu kuwafanya waachiliwe na kuwa huru, waendelee kuandamana kudai uhuru wa watu hawa, wamuandikie kila mmoja (katika wanasheria) ili kuziweka habari za waliofungwa kama mimi katika maandishi na katika mambo wanayoyafanya kuwa muhimu kwao.

Na Waislamu lazima waendelee kumuomba Allah (S. W.) na wala wasichoke, wafanye jihadi kwa ajili yake na wala wasiache kufanya hivyo. Na iwapo Waislamu wataacha kufanya Jihadi kwa ajili ya Allah (S. W), Mwenyezi Mungu ayaepushe hayo, basi Allah atawafanya waadhirike na kupoteza heshima yao na hatawaondolea hali hiyo mpaka mpaka wairudie Jihadi kwa ajili ya Allah. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe rehema na amani Mtume wetu Muhammad (S. A. W), familia yake, maswahaba na wafuasi wake. Amin.

Waislamu wanaombwa kuwasiliana na utawala wa jela iliyopo Springfield, Missouri, USA wakilalamikia mambo mabaya wanayomfanyia Dr. Sheikh Omar AbdulRahmaan kwa kutumia anuani ifuatayo:

Mr. Marty Anderson
MCFP - P. O. Box 4000
Springfield, MO, 65801-4000, USA.
Phone: (417) 862-7041
Fax: (417) 837-1777.

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
YALIYOMO | An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook