Historia: Form IV
Upinzani wakati wa Khalifa Ali

Vita vya wenyewe kwa wenyewe

Kipindi cha Ukhalifa wa Ali hakikuwa na wapinzani kutoka nje ya Dola ya Kiislamu. Na inaweza kusemwa kuwa hakukuwa na upinzani kwa sababu hapakuwa na kiongozi aliyechaguliwa kwa utaratibu unaokubalika na kwa sababu hii inakuwa vigumu kusema kulikuwa na upinzani ila kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ni vigumu kusema kuwa Ali alikuwa ameteuliwa kwa utaratibu wa Uislamu kuwa Khalifa. Wahaini wale baada ya kumuua Khalifa uthman, mji wa Madina na serikali yake ilikuwa chini yao kwa muda wa siku sita 94 na swala ya Ijumaa waliendesha wao. Siku ya sita Ali alitangazwa kuwa khalifa na wauwaji, na wauwaji hawa hawa ndio waliofundisha kuwa Ali ni waasi wa Mtume. Aisha, Talha Zubeir ni vigumu kusema kuwa waliupinga Uislamu walipopigana na Ali katika vita vya Ngamia, vile vile ni vigumu na haiwezekani Muawiya alipokataa kumtii Ali alikuwa amekosea hivyo alipinga Uislamu alipopigana na Ali katika vita vya Sifin. Tunachoweza kusema wakati wa Ali kulikuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika vita hivyo, nani alipigania Uislamu, nani alipigania kundi lake, au ukoo wake au udugu au kabila lake n.k. ni maoni ya kila mwana historia baada ya kujua mkondo wa matukio ya kihistoria.

Jambo la kusikitisha ni kuwa kipindi cha Khalifa Ali kilitawaliwa na mapigano baina ya wenyewe kwa wenyewe baina ya Khalifa na Aisha, Talha na Zubair, Khalifa na Khawarij na Khalifa na muawiya Gavana wa Syria. Matukio yalichukua mkondo ufuatao.

Baada ya kuuawa kwa Khalifa uthman na kutawazwa kwa Ali baadhi ya jamaa wa Khalifa walikwenda makka na kutawazwa kwa Ali baadhi ya jamaa wa Khalifa walikwenda Makka na kueleza tukio lilivyokuwa, mama wa waumini Bi Aisha alistushwa sana na tukio hili, lakini lililotisha zaidi ni hatua ya Khalifa ya kuahirisha adhabu ya waliyomuua Khalifa Uthman kwa hoja kuwa kwanza arudishe amani nchini kisha ndipo awaadhibu wauwaji. Hoja hii ilikuwa ni ngumu kueleweka hasa ukizingatia mambo matatu. Kwanza muanzilishi wa ghasia na hatimae kufikia kifo cha Khalifa Uthman alifundisha imani ya wasi wa Ali. Pili hilo ndilo lililomuweka Ali madarakani na tatu, wauwaji hawa pamoja na kuambiwa waondoke Madina siku ya tatu ya Ukhalifa wa Ali kundi la Saba lilikhalifu amri ya Khalifa na kubaki Madina kwa kisingizio cha urafiki.95 Mama wa waumini ambae alikuwa anarudi Madina kutoka kwenye Hija Makka alirudi Maka na kuwaomba watu kwenda kulipiza kifo cha Khalifa. Maswahaba maarufu Talha na Zubeir walimuunga mkono na wakawa nae. Wapiganaji 2000 walipatikana. Lakini walipokuwa wanakwenda Madina wakapata wazo la kupitia basra kupata watu wengi walipokuwa njiani kuelekea Basra watu wengi wakaungana nae na alipofika Basra alikuwa na watu 3000 chini ya Bendera yake.

Gavana wa Basra Uthman bin Hunif alituma watu ili kujua lengo la ziara ya Bibi Aisha Basra. Wajumbe wa Gavana walifahamishwa kuwa Yeye mama Aisha na Waislamu wengine walitaka kuwakumbusha Waislamu juu ya wajibu wao kwa Khalifa aliyeuawa. Na dhima yao ni kuwaadhibu wauwaji. Kusikia hivi Gavana alizuia msafara usiingie Basra. Kwa hiyo akaita mkutano na kuwaamuru watu wake wawapige Mama aisha na wenzake baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Khalifa Ali. Watu wake waligawanyika kuna waliomuunga mkono yeye na wapo waliomuunga mkono Gavana. Mama Aisha alitoa Hotuba ambayo iliwezesha kuwateka nusu ya watu ambao mwanzoni walimuunga mkono Khalifa. Kuona hivi mama aisha alitaka suluhu, lakini upande wa gavana kulikuwa na watu wa Saba ambao suluhu hawakuitaka - Hakim bin Hublan akiwa kiranja wa kundi hili lisilotaka suluhu alivamia jeshi la Mama Aisha hata kabla ya ruhusa ya gavana wake na uchokozi huu vita vikaanza, gavana akatekwa, Hublan na wenzake wengi wapatao 600 wakauawa na Basra ikatekwa na kuwa chini ya Bibi Aisha, Talha na Zubeir.

Vita kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali

Khabari za kutekwa Basra zilimchukua kwa mshangao mkubwa Khalifa Ali ambae alikuwa aende Syria kumrudi Muawiya alilazimika kwenda Basra kwanza kutuliza hali ya kule.

Alipofika Dhi-Qar’a mahali karibu na Basra-alituma ujumbe kwa Aisha, Talha na Zubeir wafanye mazungumzo ya amani. Nafasi ilipatikana mazungumzo yakafanywa na wakawa karibu kukubaliana baada ya Ali kuahidi kuwa atawaadhibu wauwaji wa uthman Dola itakapokuwa na amani. Lakini mpango wa amani haukuwa na maslahi kwa lile kundi la Ibn Saba ambalo lilifanya sehemu ya jeshi la Ali. Walinong’onezana kuwa Ali anataka kufikia makubaliano ya amani na ameahidi kuwaadhibu waliomuua Uthman. Kundi hili lilikuwa ndilo lililomuua Khalifa Uthman halikupendezwa na mpango huu wakaunda hila iliyochochea kutokea vita. Mbinu mbili walizitumia. Kwanza walipeleka umbea Basra kuwa Ali akiingia Basra atawafanya watumwa wakazi wote na atawaua vijana wote. Kwa sababu hii watu wa Basra lazima wapigane.96 Ibn Saba na wachochezi wake usiku usiku walivamia jeshi la mama Aisha ambae aliarifiwa na kwa namna hii vita vikaanza. Vita hivi vinajulikana kwa jina la vita vya ngamia.

Vita vilikuwa vikali kwa vile ukubwa wa jeshi ulilingana. Hata hivyo baada ya mapigano makali na kuuawa Waislamu wapatao elfu kumi. Hata hivyo ushindi ulikuwa wa Ali. Talha alikufa, Zubair aliacha kupigana na akawa anaelekea Madina ndipo akauliwa njiani, Talha aliuliwa vitani. Wakati wote wa vita mama Aisha alikuwa katika sehemu ya uwanja wa vita akiwa amepanda ngamia. Kuwepo kwake kulifanya mapigano yaende kwa kasi kubwa, bila kukoma, ndipo Ali alipoamuru ngamia wake akatwe miguu ya nyuma. Ngamia aliangukia miguu yake ya mbele na kwa heshima zote akatolewa ndani ya kikalio cha ngamia na vita vikaisha - ushindi ukawa upande wa Khalifa Ali. Mama Aisha akasinda
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook