Jihad katika Biblia

WAKRISTO wamefanya kampeni za makusudi kwa muda mrefu sana, ili kutoa picha kuwa Jihad (vita vitakatifu) vimeamuriwa na Allah (s.w.) katika Qur’an na kuwa katika Biblia hakuna sehemu yoyote iliyohalalisha vita hivyo vya "kikatili".

Kwa kuwa Jihad inaambatana na Uislamu, na kwa kuwa Uislamu umekuwepo tangu Nabii Adam (a.s.), makala hii itadhihirisha kwa ufupi vipi Waislamu wa zamani (Wayahudi) wamepigana vita hivi vitakatifu na walikuwa "wakatili" au "wapole" kiasi gani.

Katika kuwaandaa Waislamu kwa jihad, Yehova (s.w.) aliweka sheria ifuatayo: "Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope, kwa kuwa BWANA Mungu wako yu pamoja nawe, aliyekukweza katika nchi ya Misri. Na iwe msongeapo mapiganoni, Kuhani na kusema na watu, awaambie, sikizeni, enyi Israili, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu; mioyo yenu isizime, msiache wala msitetemeke, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao. Kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi". (Kumb. 20:1-4)

Jihadi rasmi ya kwanza kabisa iliongozwa na Nabii Yoshua (a.s) ili kuwaingiza Waisraeli katika nchi ya ahadi (Kaanani) wakitokea Misri. Mji wa kwanza kushambuliwa ulikuwa wa Yeriko. Kwanza Yoshua (a.s.) alipeleka wapelelezi ambao walijificha katika nyumba ya kahaba Rahabu (Yoshua 2:1-24). Kisha waliuvamia mji na kuuweka "Wakfu" kwa kuwa kile chenye uhai isipokuwa kahaba Rahabu na familia yake". "...Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee na ng’ombe, na kondoo, na punda kwa makali ya upanga". (Yoshua 6:21)

Utaratibu wa "kufyagia" miji uliendelea hadi Yoshua (a.s.) alipotawala miji yote aliyoitaka. (Tazama Yoshua 10:28 - 11:24). Wakuu wa nchi (wafalme) wao walikumbana na vifo vya aina yake". "Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemedari wa vita waliokwenda naye, haya jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao. Yoshua akawaambia., msiache wala msifadhaike, iweni hodari, na mioyo ya ushujaa, kwa kuwa ndivyo BWANA atakavyowafanyia adui zenu wote, ambao mwapigana nao. Baada ya Yoshua akawapiga na kuwaua, akawatundika katika miti mitano, nao wakawa wakitundikwa katika miti hiyo hata jioni". (Yoshua 10:24-26).

Aidha, wakati mwingine Yehova (s.w.) alishiriki yeye binafsi "kufyagia" watu wengi zaidi kuliko "walivyofyagiwa" kwa mikono ya Waislamu. "Kisha ikawa hapo walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao wakafa, hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko waliouliwa na wana wa Israeli kwa upanga". (Yoshua 10:11)

Jihadi ya kuikomboa nchi takatifu ilianza mwaka 1220 KK na kuendelea hadi mwaka 1010 KK ambapo Nabii Daud (a.s.) aliutwaa mji wa Yerusalem na kuwa makao makuu ya dola ya Kiislamu. Dola ya Kiislamu ilidumu kwa muda wa miaka 290 kwa dola ya Kaskazini (Samaria) na miaka 423 kwa dola ya kusini (Yuda). Dola hizi zilianguka na kutawaliwa na makafiri baada ya kumwasi Yehova (s.w.) kwa kufuata sheria zisizo za Kiislamu.

Baada ya kuteswa sana na makafiri Waislamu walianzisha tena jihadi ili kujikomboa wakati wa mfalme Mgiriki Antioko Epifani ( 175 - 163 KK). Vita hivi vilianzishwa rasmi na Sheikh Matathia mwaka 166 KK. Sababu ya kuanzishwa kwa jihad hii ilikuwa kurejesha sheria za Kiislamu (Torati) zilizofutwa na Antioko Epifani ili kuleta "Umoja na mshikamano wa kidola (Empire)".

"Mfalme Antioko akaziandikia milki zake zote, kwamba wote wawe taifa moja, kila mtu aache sheria zake za asili. Watu wote wa mataifa wakaikubali amri ya mfalme, hata wengi katika Israel (Waislamu) walifuata ibada yake, wakitoa dhabihu kwa miungu ya uongo na kutia najisi sabato. Mfalme akapeleka barua Yerusalemu na kwenye miji ya Uyahudi (dola ya Kiislamu) kwamba wazifuate desturi zilizo za kigeni kwao, waache kutoa sadaka za kutetekezwa a dhabihu na sadaka ya kinywaji hekaluni, wazinajisi sabato na sikukuu, na kulitia unajisi hekalu na waliotakasika. Tena, wajenge madhabahu na mahekalu na viwanja vitakatifu vya miungu ya uwongo, na kutoa dhabihu za nguruwe na wanyama wachafu, waache wana wao bila kutahiriwa, na kujitia nafsi zao unajisi kwa uchafu na ukafiri wa kila namna, kusudi waisahau sheria (Torati) na kuzibadili kawaida zao. Naye asiyelitii neno la mfalme atakufa". (1 Makabayo 1:41-50)

Sheikh (Kuhani) Matathia hakuvumilia kuendelea kuona fedheha hiyo dhidi ya Uislamu na akasema: "(Mathathia) akayaona mambo ya ukufuru yaliyotendeka katika Uyahudi na Yerusalemu, akasema, ole wangu! Kwa nini nalizaliwa kuuona uharibifu wa watu wangu na maangamizo ya mji mtakatifu, hata kukaa kimya unapotiwa katika mikono ya adui zake, na patakatifu pake (Msikiti mkuu - Hekalu) katika mikono ya wageni (Antioko aliteka hekalu na kulinajisi kwa kuingiza madhabahu yake ya kutambikia maarufu "chukizo la uharibifu"). Nyumba yake imekuwa kama ya mtu asiye na heshima vyombo vyake vya fahari vimetekwa na kuchukuliwa; watoto wake wameuwawa njiani, na vijana wake kwa upanga wa adui (rejea tukio la Mwembechai) taifa lipi lisiloyashiriki mateka yake? Ufalme upi usioziteka mali zake? Mapambo yake yote yameondolewa naye aliyekuwa muungwana amekuwa mtumwa! Naaam, vyombo vitakatifu vyetu na fahari yetu na utukufu wetu vimefanywa ukiwa; vimetiwa unajisi na watu wa mataifa (mapolisi). Mbona, basi, tuzidi kuishi? Matathia na wanawe wakararua nguo zao, wakajivika gunia, wakalia kwa majonzi (toba ya kweli) (1 Makabayo 2:6-14). Baada ya toba hiyo ya kweli akatangaza jihadi "kisha, Matathia alipiga mbiu mjini kwa sauti kuu, akisema, kila aliye na juhudi (mujahid) kwa ajili ya sheria (Torati) na kutaka kulitetea agano, na ANIFUATE! Naye na wanawe wakakimbilia, wakaviacha vyote walivyokuwa navyo mjini" (1 Mak. 2:27-28).

Kisha kazi ikaanza. Baadhi ya Wayahudi wapatao 1000 walienda kujificha jangwani. Askari wa mfalme waliwafuata katika siku ya sabato kwa kuogopa "kuinajisi" sabato walisita kupigana na wote wakachinjwa kama mbuzi (tazama 1Mak 2:29-38). Lakini Sheikh Matathia akaamua hivi, "Matathia na rafiki zake walipopata habari waliambana, kama sisi sote tutafanya kama walivyofanya ndugu zetu, tusipigane na watu wa mataifa kwa ajili ya nafsi zetu na amri (sheria) zetu, watatufata upesi katika nchi. Wakafanya shauri siku ile ya kuwa; kama mtu yeyote akituletea vita siku ya sabato TUPIGANE NAYE, tusife wote kama ndugu zetu waliokufa katika vificho vyao. Wakati huo kundi la Wahasidimu (mujahidina) walijiunga nao, Waisraeli (Waislamu) hodari wa vita waliojitoa kwa hiyari kuitetea sheria. Na wote (wasio Waislamu) waliyakimbia maovu walikuja kwao na kuwaongezea nguvu. Wakakusanya jeshi kubwa, wakawapiga wenye dhambi (makafiri) katika hasira yao na, (Waislamu) walioasi (wanafiki) katika ghadhabu yao; na (wanafiki) waliobaki waliwakimbilia mataifa (makafiri) wajisalimishe kwao. Matathia na rafiki zake wakazunguka zunguka wakizivunja madhabhu za miungu na kutahiri kwa shuruti watoto wote wasiotahiriwa katika mipaka ya Israeli; wakawafuata wana wa uovu na kazi ilifanikiwa mikononi mwao. Wakaiokoa sheria katika mikono ya mataifa na wafalme, wasikubali wenye dhambi wainue pembe zao". (1Mak. 2:39-48)

Sheikh Matathia alipokaribia kufa aliwausia wanawe yafuatayo: "Msiyaogope maneno ya mtu mwenye dhambi, maana fahari yake itakuwa samadi na funza. Leo atainuka na kesho hataonekana kamwe, amerudia udongo wake na mawazo yake yamepotea. Basi ninyi wanangu, muwe hodari, mfanye kwa kiume kwa ajili ya sheria (Torati), maana kwa hiyo mtatukuzwa. Tazama, Simon ndugu yenu, najua ya kuwa ya mtu wa shauri; msikilizeni siku zote; atakuwa baba kwenu. Yuda Makabayo, shujaa tangu ujana wake, atakuwa jemadari wenu na kuwapigania watu wenu. Nanyi, wapokeeni wote wanaoishika sheria, mkatoze kisasi cha maovu waliyotendewa watu wenu. Wapatilizeni mataifa na kuyaangalia (kuyafuata) maneno ya sheria. Akawabariki, akakusanyika kwa baba zake (akafa)" (1Mak. 2:64-69)

Mwanzoni tu, jemedari Yuda Makabayo akakumbana na mtihani mkali sana "Apolonio akakusanya mataifa pamoja na watu wengi kutoka Samaria, ili apigane na Israeli. Yuda akapata habari, akaenda kukutana naye, akampiga akamuua. Watu wengi wakanguka wametiwa jereha za mauti na wengine wakakimbia. Wakateka nyara, naye Yuda aliutwaa upanga wa Apolonio, akautumia siku zote.

Seroni, jemadari wa jeshi la Shamu, alisikia ya kuwa Yuda amekutanisha mkutano, jeshi la watu waaminifu (wacha Mungu) na walio hodari wa vita, akasema, nitalitukuza jina langu na kujipatia heshima katika ufalme kwa kupigana na Yuda na wale walioko kwake wanaoidharau amri ya mfalme. Na pamoja naye walikwenda jeshi kubwa la watu waovu ili wamsaidie kuwatoza kisasi wana wa Israeli. Akaja karibu na mipando ya Beth-horoni, Yuda akamwendea na kikosi kidogo. Nao walipoliona lile jeshi kubwa likija juu yao walimwambia Yuda, Je! Sisi kundi dogo tutaweza kupigana na umati huu mkubwa wa nguvu? Nasi tumedhoofu kwa sababu hatujaonja kitu leo. Yuda akasema, ni jambo rahisi watu wengi wazingiwe kwa mikono ya wachache. Kwa mbingu (Mwenyezi Mungu s.w.) ni mmoja tu, kuokoa kwa wengi au kwa wachache, maana kushinda vitani hakupatikani kwa wingi wa watu, ila kwa nguvu itokayo mbinguni. Wao wanatujia kwa wingi ni jeuri na udhalimu ili kutuharibu sisi na wake zetu na watoto wetu na kututeka. Lakini sisi tunazipigania maisha na amri zetu . Yeye (Yehova s.w.) atawafadhaisha usoni petu, basi msiwaogope. Akisha kusema hayo, aliwashambulia kwa ghafula, Seroni na jeshi lake wakapondwa mbele yake. Wakawafuatia katika mitelemko ya Beth-horoni hata uwandani chini wakaanguka watu kama mia nane na waliosalia walikimbilia nchi ya Wafilisti. Basi hofu na woga uliwaangukia mataifa ya jirani kwa sababu ya Yuda na ndugu zake, jina lake likajulikana hata kwa mfalme na mataifa yote walisimulia habari za vita vyake" (1Mak. 3:10-26). Jihadi hii iliendelea hadi dola yote ya Kiislamu ilipokombolewa na amani kurejea.

Katika kuthibitisha kuwa Yehovah (s.w.) yuko pamoja na mujahidina katika vita vyao, mujahidina watatu (3) walilishinda jeshi la makafiri zaidi ya elfu kumi. (Mujahid) Yonathan na jeshi lake wakapiga kambi penye ziwa la Genesareti hata asubuhi na mapema wakaondoka kwenda uwanda wa Hazori. Jeshi la mataifa lilikutana naye uwandani. Wengine wao walikuwa wakimwotea milimani, hali jeshi lenyewe lilipambana naye uso kwa uso Nao waliomwotea wakaondoka wakajitia katika vita, na wote wa upande wa Yonathani walikimbilia, asibaki hata mmoja ila Matathia bin Absolomu na Yuda bin Kalfi, wakuu wa vikosi. Yonathani akararua nguo zake akajitia mchanga kichwani (toba ya kweli) akasali. Akajitia tena vitani, akawarudisha nyuma, hata wakakimbia, watu wake walipoona hivi walimrudia wakafuatana naye wakiwakimbiza mpaka Kadeshi kwenye kambi lao, wakatua. Siku ile katika wageni walianguka (walikufa) watu kama tatu elfu. Yonathani akarudi Yerusalem". (1Mak 11:67-74)

Katika Qur’an (Katiba mpya) Yehova (s.w.) ameweka kipimo (ratio) cha 1:10 (Muislamu mmoja kwa makafiri kumi) katika hali ya kawaida (isiyo ya dharura) anasema: "Ewe Mtume (wa Mwenyezi Mungu)! Wahimize walioamini wende vitani. Wakipatikana kwenu watu ishirini wanaosubiri WATASHINDA mia mbili (katika hao makafiri). Na wakipatikana watu mia moja kwenu watashinda elfu moja ya wale waliokufuru, maana hao ni watu wasiofahamu". (Qur. 8:65)

Mwenyezi Mungu ni yule yule, juzi, jana, leo na kesho, isipokuwa hubadilika majina yake kulingana na wakati na lugha. Majina yafuatayo El, Ya, YHWH, Ya-Yahweh, Yehovah, Adonay (yote ya Kiebrania na Kiaramu) na Allah ( Kiarabu) yote yanamaanisha Mungu mmoja. Mtu anayetenganisha majina hayo na kusema kuna Mungu "Yehova" na "Allah" ni mgonjwa wa akili au mpagani. Kwani hata Wakristo wanaamini Mungu ni mmoja japo ana "nafsi tatu" hivyo Mkristo (mlokole) anayeamini kuwa kuna "mzimu" wenye nguvu na uwezo wa kuwaundia watu utaratibu wa maisha (dini) ni mpagani kwani anaamini miungu wawili (Yehova (s.w.) na "mzimu").

Cha kushangaza hata baadhi ya wahariri tena walokole nao wameshaamini itikadi hiyo ya kipagani katika gazeti moja la dini ya Kikristo ya madhehebu ya (Kipentekoste toleo Na. 050 la Februari 14 -2, 1999,) litokalo kila siku ya Jumapili katika kauli ya Mhariri; pana kichwa cha habari "Tuepuke kuiga mambo ya Kipagani". Bila kujua kuwa yeye Mhariri ndiye anayejithibitisha kuwa ni mpagani, anasema "... kila mtu anayo haki ya kuchagua dini lakini kuchanganya dini kuna hatari ya kujikuta HAKUNA MUNGU ANAYEKUTAMBUA", anaendelea, "Kwanini viongozi wa Makanisa wasimng’ang’anie Yehovah na mwokozi Yesu Kristo kama vile Waislamu wanavyomshikilia Allah (s.w) na Mtume wao Muhammad (s.w.), badala ya kuparamia imani za watu wengine ambazo hawajui mwanzo wala mwisho wake?" Sasa msomaji jiulize mwenyewe, nani ni mpagani na nani ni Mkristo kati ya Padre John asemaye, "Mimi nautambua mfungo wa Ramadhani, natambua kuwepo kwa dini ya Kiislamu na pia najua kuwa Waislamu ni watoto wa Mungu na Mungu anawapenda... ndio maana tukafanya ibada hiyo( Gazeti la madhehebu ya Pentekoste litokalo kila siku ya Jumapili Na. 048 Uk. 1) na Mhariri Paschal Dismas anayesema hicho alichokisema katika gazeti hilo hilo la Pentekoste Na. 050 Uk. 4.

Hivyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni yule yule, jihad itaendelea hadi dunia yote itawaliwe na sheria za Mwenyezi Mungu za sasa (Qur’an ma Sunnah) au kisimame kiama. Ni "biashara" ya enzi na enzi kama asemavyo Yehova (s.w.) "Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao (watoe nafsi zao na mali zao katika kupigania dini) ili na Yeye awape pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanauwa na wanauwawa. Hii ndiyo ahadi aliyojilazimisha (Mwenyezi Mungu) katika Taurati na Injili na Qur’an. Ni nani atekelezaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye (Mwenyezi Mungu) na huko n diko kufuzu kukubwa". (Qur 9:111)

Mwisho nawakumbusha Waislamu wenzangu wote maneno ya Sheikh Matathia aliyosema kuwa "Endapo sheria za Kiislamu hazitumiki, basi hakuna uhalali wa Muislamu yeyote kuwa hai", "... mbona basi tuzidi kuishi". (1Mak. 2:13)
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook