WIKI iliyopita nilikatisha kidogo muendelezo wa maradhi ya Paraphilia kwa kuelezea gonjwa la Islamophobia (kuogopa Uislamu) ambalo limeenea duniani katika sehemu ya mwisho ya karne hii kutokana na sababu mbalimbali. Leo ninarudi tena kwenye maradhi aina ya Paraphilia kwa kuangalia ugonjwa wa kisaikolojia uitwao Sexual Masochism.
Katika moja ya matoleo yaliyopita niliongelea Paraphilia moja iitwayo Sexual Sadism, ambayo ni hali ya mtu kupenda na kuona raha kumdhalilisha mtu wa jinsia nyingine kijinsia, au mtu wa jinsia moja kuona raha mtu wa jinsia nyingine anapodhalilika kijinsia.
Sexual Masochism ni kinyume cha Sexual Sadism. Mgonjwa wa Sexual Masochism hupata raha, au hufurahia kuteswa na hasa kupata maumivu kutoka kwa mtu wa jinsia tofauti na yake.
Ugonjwa huu huwapata zaidi wanaume. Kwa wagonjwa mahututi, inakuwa kwamba hahisi raha yoyote mpaka ateswe kwa vyovyote vile, mfano kuchapwa viboko, au kung’atwa kwa meno, n.k. Kule Ulaya na Marekani ugonjwa huu na watu wenye maradhi haya huishi majumbani mwao wakiwa wana viboko au kitu chochote kinachoweza kuleta maumivu, vikiwa tayari vimewekwa kwa kutesewa wao wenyewe. Bila ya kuteswa kwanza hawezi kufanya lolote.
Wanasaikolojia wengi huiweka tafsiri hii ya Sexual Masochism hapa kwenye kiwango cha mtu kuona raha kuteswa na mtu wa jinsia nyingine ikiwa ni sehemu ya mahusiano yao kijinsia, lakini inabidi kuiangalia tafsiri hii kiupana, kwani maradhi huzidiana kwa kiasi. Kwa wagonjwa wengine ambao huwa hawafikii kiwango cha kujiweka tayari ateswe kwa kutandikwa viboko au vinginevyo, lakini wapo kwa mfano wale ambao hufurahi wanapomchokoza mtu wa jinsia tofauti na wao akikasirika na kuwatukana.
Katika jamii yetu, kuna wanaume hukaa mabarabarani, kazi yao kusubiri mwanamke akipita wamchokoze, na mwanamke huyo akipita kimya, hawafurahi, lakini akiwajibisha hasa kwa kuwatukana basi wao ndio hufurahi na hufurahi zaidi kama mwanamke atakuwa fundi wa kuporomosha matusi hasa ya mwilini.
Hakuna asiyefahamu kwamba kutukanwa ni aina fulani ya mateso, na wengine huona ni bora kupigwa kuliko kutukanwa. Ndio maana tunasema kuwa mtu anapoona raha kuvurumishiwa matusi na mtu wa jinsia tofauti na yake, basi yeye ni Masochist.
Wapo wanawake wenye maradhi haya ambao nao hupenda na huona raha kufanyiwa mambo ambayo kwa mtu muungwana hayavumiliki. Kuna wale ambao hupenda kupigwa, basi anaweza akafanya kisa cha makusudi kwa mwanaume ili apigwe lau kidogo au atukanwe.
Wapo wale wanawake ambao hufahamu labda kama mwanaume ambaye ni mgonjwa wa akili, na kwamba akichokozwa huvurumisha matusi. Basi wanawake hawa humchokoza makusudi ili awavurumishie matusi, na hasa anapovurumisha yale matusi ya maungoni basi wao hufurahi na roho zao wanavyotukanwa. Utashangaa mtu anaacha shughuli zake kwa vile kamuona mwehu mwenye hazina ya matusi anapita ili akamchokoze.
Mtu muungwana unapowaona watu wenye tabia hii huwakemea, labda kwa kuwaambia "acha utoto". Hii ni kwa sababu wapo watoto hasa wa kiume wenye tabia hii ya Kimasochist. Wao hupendelea kuwachokoza watoto wa kike, na lengo lao ni kuwafanya watoto wa kike wachukie na kulipizia kwa kuwatukana au kuwakimbiza na kuwapiga. Basi hupenda tu na kuona raha kukimbizwa na kupigwa.
Mfano mwingine wa wagonjwa wenye maradhi haya ni wale ambao wanafurahi kuteseka kisaikolojia hasa wanaume. Chukua mfano wa mtu mwenye njaa anavyoteseka akiona chakula kizuri chenye harufu na ladha nzuri ambacho anakiona tu na kupata harufu yake, lakini hakipati. Basi kuna watu ambao hufurahia kuteseka kwa kuwakodolea macho watu waliokaa au waliovaa vibaya. Wenye maradhi ya Exhibitionism (wendauchi) huona raha watu wanavyohemshwa na vile walivyovaa au huona raha watu wanavyoteseka. Basi kuna wale wanaoona raha kuteseka kwa kuwaangalia wendauchi wale. Hawa nao pia ni Masochists.
Maradhi haya vile vile chimbuko lake ni kukithiri kwa zinaa katika jamii, na watu kuwa na maradhi ya UKIMO (upungufu wa kinga moyoni). Dawa pekee ni Uislamu kushika hatamu.
|
|