Vipi uliyaonaje madai ya demokrasi na uhuru wa kutoa mawazo pamoja na uhuru wa kuabudu katika nchi zinazojiita za kidemokrasia na ulimwengu huru wa Kimagharibi?
Kama nikisema kwamba nchi za Afrika ya kati zina uhuru zaidi (wa mambo uliyoyataja) kuliko Marekani sitakuwa nimekosea. Maneno hayo (demokrasia, uhuru wa kuabudu n.k.) ni mfano wa pipa tupu ambalo kutokana nalo unasikia mwangwi na sauti ya juu bila ya kuwa na maana yoyote au manufaa (yoyote kwa msikilizaji). Haya ni maneno matupu, kwa sababu ni uhuru kwa ajili yao wenyewe lakini hawaruhusu uhuru huo kwa wengine. Ni demokrasia ya kuifurahia wao lakini hawaruhusu wengine kuwa na maoni au fikra tofauti na wao. Nilikuja hapa nikiimbia jela kuja kwenye nchi ya uhuru, lakini badala yake nikafungwa. Nilikuja (hapa) nikikimbia (hali ya) kunyimwa uhuru na kuzuiliwa kutoa mawazo, lakini nilistushwa na hali mbaya zaidi Amerika. Maneno haya (ya uhuru na demokrasia) ni kwa ajili ya tabaka fulani kunufaika nayo lakini wengine wananyimwa.
Vipi kuhusu haki za binadamu ambazo wanaziimba usiku na mchana, unavyoziona wewe hali ya kuwa umefungwa jela?
Hali yangu katika jela ni mbaya zaidi ya hali yangu iliyokuwa katika jela za Misri, ni mbaya kuliko hali katika jela zingine katika nchi nyingi. Katika jela ya Amerika hakuna uhuru wa kutoa mawazo, uhuru wa kufanya ibada na uhuru wa kukutana na wafungwa wengine. Siwezi kutimiza wajibu wangu katika kuabudu kwani hakuna sala ya Ijumaa, hakuna mkusanyiko, hakuna kuchanganyika na waislam wengine, hakuna kusherehekea sikukuu za Kiislam na hakuna udhihirisho wowote dini ya Kiislam. Yote hayo nimenyimwa. Wanahalalisha kuninyima (uhuru huo) kwa sababu za na zisizokuwa na msingi. Ama kuhusu kuchanganyika, nipo katika kifungo cha ndani ambapo nimetengwa peke yangu (solitary confinement) toka nilipofungwa mwaka 1993 mpaka leo. Nimeishi peke yangu bila ya mtu yeyote wa kuniangalia. (Hivyo) mimi ndiye ninayefua nguo zangu. Wanahalalisha haya kwa kusema kwamba mtu kipofu anapaswa kutengwa…Mtu ambaye hataki kujifunza Kiingereza anahitaji kutengwa peke yake. Kwa hiyo sababu ambazo zinahitaji mtu kuchanganyika na wenzake (ili ajifunze Kiingereza) wao wanazifanya kuwa sababu za kumtenga mtu!. Huo ndio uungwana wanavyodhani wao. Ninateseka humu jela kwa kukosa kabisa mawasiliano na nje, hakuna radio, hakuna kinasa sauti, hakuna mfasiri. Yote haya wananinyima. Hakuna kusoma, hakuna wa kunisomea magazeti, vitabu au chochote kile. Katika kifungo hiki cha kutengwa ninapata mateso makubwa. Wameweka juu ya selo yangu sauti kubwa zenye kusumbua ambazo hunifanya nisilale usiku kucha. Vile vile wameweka ugumu katika ratiba yangu ya kutembelewa na mambo mengine ya kawaida katika maisha.
Cha kuzingatia kuhusiana na nilichokisema katika haki za binadamu, ni kwamba jumuiya nyingi za haki za binadamu zilipeleka taarifa katika utawala wa jela na wakuu wa magereza wa Amerika wakiuliza juu ya madai ya kwamba nilikuwa nikinyimwa uhuru na kufanyiwa mambo mengi mabaya hapa jela. Waliuliza utawala wa jela wakitaka majibu ya maswali yao. Lakini nini jumuiya hizi za haki za binadamu zilipata?. Hawajapata jibu lolote mpaka sasa. Ziko wapi basi hizo haki za binadamu wanazojitapa nazo?. Na ziko wapi haki wanazowapa Waislamu? Kila mara ninagonga mlango mfululizo ili labda waniletee kitu ninachokihitaji, lakini sipati majibu. Mara nyingine ninagonga kwa masaa mengi tu hali ya kuwa baadhi ya wafungwa wanagonga mara chache au wanamwita askari wa jela ambaye huja mbio kuleta wanachokitaka, wakati mimi inanichukua masaa kadhaa kupata ninachotaka. Ubaguzi wa rangi upo katika namna wanavyotuhudumia. Na bado utakuta watu wanatamba kuhusu uhuru na haki za binadamu!
Nini jukumu la Waislamu wanaoishi nchi za Magharibi juu ya dini yao?
Majukumu ya Waislamu wanaoishi nchi za Magharibi katika dini yaoni kuungana na kujiendeleza kiuchumi na kifedha. Lazima wawe na pesa. Pesa (kwa wakati tulionao) ndio yenye kuendesha mambo mengi katika maisha. Muislamu mwenye nguvu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko Muislamu dhaifu. Hivyo Waislamu lazima wajijenge kifedha, wawe na vyombo vyao vya habari, wawe wazalishaji wazuri (wa bidhaa) na waungane katika vyama na jumuiya za viwanda na kilimo. Lazima wainusuru na kuilinda dini yao, familia zao na wasichanganyike na wengine katika namna ambayo itawalazimu waachane na dini yao. Lazima watambulikane na wawe na utambulisho wa nguvu wa Uislamu wao na wasipoteze chochote katika hivi.
Je kuna neno la mwisho unalotaka kuwapa Waislamu wasomaji wa Jarida hili?
Neno langu la mwisho ni kwa Waislamu kuacha kulala na watupilie mbali uvivu uliozunguka vichwa vyao. Tukumbuke maneno ya Mtume (S. A. W) kwa mkewe: "Ewe Khadija! Muda wa kulala umekwisha". Lazima (Waislamu) wajikusanye kama kitu kimoja, na wafanye sana kazi kwa ajili ya dini, kuupa Uislamu kipaumbele katika maisha yao na wasilisahau jambo hili. Mtu akiwa na jambo linalomshughulisha basi hulala na kuamka akiwa bado anafikiria jambo lile. Hivyo basi Waislamu waufanye Uislamu kuwa jambo linalowashughulisha. Basi mioyo yao iumie kwa mabalaa yanayowapata Waislamu wengine. Waumie roho zao kwa Waislamu wa Bosnia, Afaghanistan, Uturuki, Phillipines na kabla ya hapo, Palestina. Nyoyo zao ziume kwa ajili ya kutaka kuwasaidia Waislamu hawa na walie kwa kutokutimiza wajibu wao kwa Waislamu hawa. Waislamu lazima wawajali ndugu zao popote walipo., lazima wajali wale waliofungwa na lazima wajaribu kuwafanya waachiliwe na kuwa huru, waendelee kuandamana kudai uhuru wa watu hawa, wamuandikie kila mmoja (katika wanasheria) ili kuziweka habari za waliofungwa kama mimi katika maandishi na katika mambo wanayoyafanya kuwa muhimu kwao.
Na Waislamu lazima waendelee kumuomba Allah (S. W.) na wala wasichoke, wafanye jihadi kwa ajili yake na wala wasiache kufanya hivyo. Na iwapo Waislamu wataacha kufanya Jihadi kwa ajili ya Allah (S. W), Mwenyezi Mungu ayaepushe hayo, basi Allah atawafanya waadhirike na kupoteza heshima yao na hatawaondolea hali hiyo mpaka mpaka wairudie Jihadi kwa ajili ya Allah. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe rehema na amani Mtume wetu Muhammad (S. A. W), familia yake, maswahaba na wafuasi wake. Amin.
Waislamu wanaombwa kuwasiliana na utawala
wa jela iliyopo Springfield, Missouri, USA wakilalamikia mambo mabaya wanayomfanyia
Dr. Sheikh Omar AbdulRahmaan kwa kutumia anuani ifuatayo:
Mr. Marty Anderson
MCFP - P. O. Box 4000
Springfield, MO, 65801-4000, USA.
Phone: (417) 862-7041
Fax: (417) 837-1777.
|
|