Maongezi ya Ijumaa toka Msikiti
Mtakatifu wa Al Aqsa.
Imetolewa na wanachama wa Hizb ut Tahrir
Maongeza haya kwa Kiarabu yanaweza kusikika katika mtandao wa Kompyuta katika anuani ifuatayo: http://www.al-aqsa.com.
Ijumaa -12 Februari 1999.
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
Sifa zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu (S. W) na rehema na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad (S. A. W), familia yake, maswahaba na wanaomfuata mpaka siku ya malipo.
" Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu.
Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi." Al-Tawba (128, 129).
Enyi Waislamu,
"Yeyote anayemuabudu Hussein (Mfalme Hussein) basi Hussein Ameshakufa, lakini anayemuabudu Allah, basi Allah yu hai na hafi kabisa" Kauli hiiilitolewa kwa mara ya kwanza na Khalifa wa kwanza Abu Bakr akirejea kifo cha Mtume Muhammad (S. A. W).
Kama kauli hii ilisemwa kurejea kifo cha mbora wa walimwengu wote, kwanini basi isirudiwe kwa mtu ambaye ndio msaliti mkubwa katika dunia hii?. Hatukusikia kauli kama hii ikitolewa na wale wanaoitwa wanazuoni. Na hakuna mmoja wao ambaye aliwaeleza watu kwamba huyu ndiye aliyeiuzaPalestina kwa Wayahudi.
Mfalme huyu alishirikiana (na makafiri) dhidi ya Waislamu katika ‘Septemba Nyeusi’, wakati ambapo makumi ya maelfu ya Waislamu walichinjwa. Aliwapora pesa zao na kuzihamishia katika akaunti yake ya benki iliyopo Uswisi ili yeye na familia yake waiweke kwa ajili yao. Hata katika hatua ya mwisho karibu na kifo chake alimuita mkubwa wa dini ya Kiyahudi (rabbi), Israel ben Laow, amsomee aya toka katika Torah (Biblia ya Kiyahudi), badala ya kumuita Sheikh amsomee Surat Al Yasiin. Hakuna manufaa kwa taifa kuwatukuza viongozi wake. Sisi Waislamu tunatakiwa tusimtukuze yeyote isipokuwa Allah. Hairuhusiwi katika Uislamu hata kumsifia mtu. Katika hadithi Mtume Muhammad (S. A. W) alisema, "Ukiwaona watu kazi yao ni kusifu (watu) basi warushie vumbi kwenye nyuso zao". Lakini angalia Waarabu na Waislamu wanavyofanya kwa viongozi wao.
Vilevile angalia jinsi Wayahudi na Wamarekani wanavyowafanyia marais wao. Hata wakati yule kijana wa Kiyahudi alipomuua kiongozi wao Rabin, Wayahudi walimfunga, wakamruhusu rafiki wake wa kike amtembelee, na wamemruhusu kuendelea na masomo yake ya chuo kikuu akiwa jela. Wakati Mfalme Abdallah (Babu yake Mfalme Hussein) alipouawa hapa kwenye msikiti huu (mnamo miaka ya 1950), jeshi lake liliwaadhibu vikali watu wote hapa. Waliua na kutesa, na kama hiyo haitoshi, waliyachafua maji ya kunywa na dizeli; wakachanganya ngano na shayiri; na wakachangala mafuta ya petroli na siagi. Lakini watu bado wanazidi kumtukuza Abdallah na Hussein. Kitu gani watu hawa walikifanya kwa ummah huu kustahili utukufu wanaopewa?
Nchi zilizopo katika dunia ya Kiislamu zilipatikana baada ya kukomeshwa kwa Ukhalifa wa Ottoman mwanzoni mwa karne hii, ambapo ni karibu wakati huo huo ilipoanzishwa dola ya Israel.
Mfalme Hussein alikuwa mmoja wa matajiri kumi wakubwa kabisa duniani. Utajiri huu ulilimbikizwa kwa kuiba fedha za watu wake na kutoka katika misaada toka nchi za kigeni waliyoletewa watu wake.
Katika Hijaz (Saudi Arabia), wanaendelea kushereherekea kuvunjwa kwa utawala wa Kiislamu ambao nafasi yake ilichukuliwa na taifa la Kiarabu lililoitwa Ufalme wa Saudi Arabia. Na wale wanaoitwa wanazuoni wa Kiislamu huenda kwa ndege hadi Najd na Hijaz kuwapongeza kwa ushindi huo.
Mpaka lini tutaendelea kuwatukuza watawala ambao wanafanya kazi kuwafurahisha makafiri?
Tazama jinsi ambavyo viongozi wa nchi za magharibi walivyofurika kwenye mazishi ya Hussein.
Wakati mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Ahmed bin Hanbal alipofariki, Waislamu milioni moja waliandamana kwenda kumzika na watu 25,000 walisilimu kuingia Uislamu.
Hivi unapowaona viongozi hawa wa kufr katika mazishi ya Hussein, kitu gani kinakujia akilini?
Ni dhahiri kwamba viongozi hawa makufari walifurahishwa na utawala wake. Allah anasema, "Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu". Al Baqarah 120. Tunaweza kusema kwamba mtu huyu (Mfalme Hussein) alifuata ‘mfumo wao wa maisha’.
Kama haturidhishwi na watawala hawa mpaka lini tutaendelea kuogopa?. Watawala hawa wanatuletea kufr kwetu sisi, na wanashirikiana kwa karibu na mabeberu hawa waliokufuru.
Na hali katika Jordan itakuwa mbaya katika siku zijazo kwa sababu Marekani inataka kuiweka Jordan upande wake. Hata hivyo Uingereza nayo itajitahidi kwa kila hali kuongeza nguvu zake kuitawala kisiasa Jordan. Mfalme Hussein aliliweka hilo wazi alipokuwepo London kwa mara ya mwisho. Alisema "Nilipochukuwa utawala kwa mara ya kwanza niliongelea toka London na sasa naongea na ninyi toka London kwa mara ya mwisho". Kwa hiyo kutakuwa na mapambano kati ya Jordan na Amerika kwa upande mmoja, Uingereza kwa upande wa pili na wale wanaopigania kurejeshwa ukhalifa kwa upande mwingine.
Tunamuomba Allah awasaidie wanaopigania kurejeshwa ukhalifa na Allah awape ushindi dhidi ya wapinzani wao.
Amin
|
|