Na Mwandishi Wetu
YAKIWA yamepita masiku kadhaa tangu kutolewa tuhuma dhidi ya Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, wasemaji Wizara ya Mambo ya ndani wameshindwa kusema chochote juu ya tuhuma hizo.
Mara kadhaa gazeti hili limejaribu kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje hata hivyo wasemaji hawakuwa tayari kukanusha au kuthibitisha madai ya mwanafunzi Athumani Duday aliyekuwa akisoma chuo cha Lumumba Kitivo cha Uhandisi.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti madai kwamba Maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi wamefitini hadi kupelekea kurejeshwa nchini Bw. Athman Duday.
Mwanafunzi huyo alimtuhumu aliyekuwa
Balozi Bwana James Kateka na aliyekuwa Mwambata wa Elimu Bwana Chabaka
kuwa ni wahusika wakuu wa fitna hiyo.
Na Mkagile M
BINTI wa Kiislamu Maua Issa (20) ambaye ni mfanyabiashara katika Soko Kuu Ifakara hivi karibuni alimwagiwa mchuzi wa nyama ya nguruwe na mfanyabiashara mwenzie Angella Sanga.
Akingea na mwandishi wa habari hivi, Bi. Maua alisema kwamba Bi. Angella akiwa na kijana aitwaye Vicent walikwenda kwenye meza yake wakiwa na bakuli lenye nyama ya nguruwe na kumtaka ale. Alipokataa kuligusa bakuli lenyewe Angella alimmwagia mchuzi huo.
Bi. Maua ameeleza alipeleka malalamiko yake kwa Mkuu wa Soko Bw. Ligegu ambaye naye alilipeleka kwa Mku wa Kituo cha Polisi Ifakara.
Katika barua yake kwa Polisi, Mkuu huyo wa soko alieleza kwamba Angella alipohojiwa alikiri kosa. Mkuu huyo wa Soko alisema kwa kuwa kitendo hicho kimegusa imani ya dini alionelea kulipeleka kwenye vyombo vya dola.
Wakati huo huo, imedaiwa kwamba Kanisa
Katoliki wilayani Kilombero limekuwa na mpango wa kuwahamasisha na kuwakopesha
waumini wake nguruwe. Jambo hilo limeelezwa kuchangia kuufanya mji huo
kuwa na nguruwe wengi.
|
|